Haya Ndiyo Maisha Ya Laana Unayopaswa Kuacha Kuishi

Vipi ile mipango na malengo uliyojiwekea mwaka huu umefikia wapi? Ni kipi ambacho unaweza kujivunia tokea mwaka huu uanze umekifanya kila siku? Je ile hamasa uliyoanza nayo mwaka huu kwa sasa iko wapi? Yako maisha ya laana unayoishi ndiyo maana hufanikiwi kwenye maeneo mengi ya maisha yako. Maisha hayo ya laana ni yale ambayo unajidanganya …

Huyu Ndiye Mtu Muhimu Unayepaswa Kumheshimu Sana

Ni asili ya binadamu kupenda kuheshimiwa na kuthaminiwa kama mwanadamu. Pale mtu anapostahili heshima yake mpatie na asipoipata anakuwa anajihisi kama vile hayuko sawa. Watu wengine usipowapa heshima yao kadiri ya vyeo, nyazifa au nafasi walizonazo katika jamii wanaweza wakakuletea shida. Wengine huweza kutumia hata nafasi yao waliyonayo kukukomesha kwa sababu hujawapa ile heshima yao …

Kitu Pekee Unachopaswa Kukitawala Badala Ya Kuruhusu Kikutawale

Tumepewa mamlaka ya kutawala vitu vingi lakini cha ajabu ni kwamba viko vitu ambavyo watu wanashidwa kuvitawala na vinaishia kuwaendesha. Muda mwingine tunakubali Kuruhusu kitu hicho kitutawale na matokeo yake tunafanya makosa ambayo hatukutegemea kuyafanya. Na baadaye huwa tunajihisi wenye hatia baada ya kutenda. Kitu ambacho watu wameshindwa kukitawala katika zama hizi ni hasira. Hasira …

Jinsi Unavyojinyima Haki Yako Ya Kupata Kile Unachotaka

Iko zawadi ambayo Mungu ametoa sawa kwa watu wote. Masikini na tajiri wote wamebarikiwa kupata zawadi hiyo sawa bila upendeleo wowote. Zawadi hiyo siyo nyingine bali ni muda. Muda ndiyo zawadi pekee ambayo haina upendeleo na mafanikio yetu yote yamelala katika muda. Mtaji wetu wa kwanza wa kufanya chochote kile tunachotaka kwenye hii dunia ni …

Kuwa Wa Kwanza Kwenye Jambo Hili Hapa

Mahusiano yetu huwa yanakosa ladha kwa sababu ya kuangalia udhaifu wa mtu na siyo uimara wa mtu. Kuna wale watu ambao huwa hawajui kupongeza hata mtu akifanya vizuri yeye huwa anaangalia mabaya tu na siyo mazuri. Hatuwezi kuwa watu wenye mahusiano mazuri kama tutakua ni watu wa kuangalia mabaya tu ya wenzetu na hatuoni mazuri. …

Huyu Ndiye Anayeumia Pale Unapofanya Kitu Chini Ya Kiwango

Mara nyingi tunapofanya jambo lolote lile, liwe baya au zuri wale wanaotenda ndiyo wanakuwa wa kwanza kuathirika. Kwa mfano, ukimtendea mtu ubaya yule unayemtendea hatoumia sana kama wewe unayetenda. Vivyo hivyo katika utendaji, sisi wenyewe huwa tunajua uwezo wetu, hivyo tunapofanya kitu kwa kiwango cha chini kuliko uwezo wetu huwa tunaumia kwa ndani. Tunapata maumivu …

Haya Ndiyo Malengo Ambayo Hupaswi Kuwa Nayo

Kila binadamu ana malengo yake, na furaha kubwa ya mtu ni pale anapoona lengo aliloweka amefanikiwa na hili ndiyo hitaji la watu wengi kwenye malengo, kuwa na malengo ni sawa na kuwa na shamba, haitoshi kuwa na shamba tu ndiyo utaweza kuvuna mazao, bali utahitaji maandalizi ya shamba, kupanda, kufanya palizi mbalimbali na hatimaye kuvuna. …

Hii Ndiyo Kazi Yako Kubwa Katika Mahusiano

Binadamu wote ni viumbe wa hisia na kila mmoja wetu yuko katika mahusiano kadiri ya vina saba.Hakuna mtu ambaye yuko hai halafu hana mahusiano na watu wengine.Kila mmoja wetu amejikuta amezaliwa katika mahusiano ya vina saba. Katika mahusiano ambayo tunayo, yana kitu kimoja cha uhakika ambacho ni udhaifu. Ni kawaida yetu sisi binadamu kuona madhaifu …

Pale Mtu Anapokuambia Jambo lake…

Msaidie kama liko ndani ya uwezo wako, katika maisha yetu vile tunavyoishi tunajikuta tunatengeneza jamii ya wale watu wanaoendana na sisi bila hata sisi kujua. Ila hivi ndivyo asili ilivyo, kama vile sumaku inavuta vitu vyenye asili ya chuma tu huwezi hata siku moja ukakuta imekamata vitu vya asili ya plastiki. Mtu anapokuja kwako kukuomba …

Usijione Mjanja Kwenye Hili

Huwa tunajiona sisi ni wajanja pale tunapokuwa tunamshawishi mtu na kukubaliana na sisi vile tunavyotaka. Tunafikiri kuwa kwa kuwa wameshakubaliana na sisi hivyo tayari tumeshawatawala kwa kila kitu. Unaweza kumtawala mtu kwenye vitu vyote lakini iko sehemu moja pekee ambayo huwezi kumtawala ni kwenye fikra. Usijione mjanja eti unaweza kumtawala mtu kiakili kwa sababu ni …

Design a site like this with WordPress.com
Get started