Nadharia Iliyopitwa Na Wakati Katika Uongozi

Kila mmoja wetu ni kiongozi, Kama siyo kiongozi katika familia yako, taasisi basi ni kiongozi wa maisha yako mwenyewe. Kama unaweza kujiongoza basi unaweza kuwaongoza wengine. Iko njia rahisi sana katika uongozi ambayo kila kiongozi anatakiwa kuitumia ambayo ni ishi kile unachosema. Ukiwa ni mtu tu wa kusema halafu na wewe huishi kile unachosema watu …

Ukitaka Kupata Shida Kwenye Mahusiano Yako Fanya Hivi

Kama ukikaa chini na kuchunguza basi utagundua hakuna mtu ambaye yuko salama katika wito aliochagua kuishi yaani kama wewe umechagua kuwa mwanandoa au utawa lazima utakutana na changamoto katika maisha yoyote yale uliyochagua kuishi. Matatizo tunayokimbia katika mahusiano yetu au miito tuliyochagua kuishi ndiyo inatufanya tusiwe bora. Wale ambao wanakimbia changamoto katika maisha yao ni …

Kama Unataka Watu Wakutafute Bila Ya Wewe Kujisumbua

Iko njia rahisi sana ya kujiuza yaani kujitangaza ili watu wajue yale tunayofanya yanaweza kuwa na mchango gani katika maisha yao. Kila mtu huwa ana kitu anachofanya na wengine wanataka kujulikana na watu na hata kupata umaarufu. Haya yote yanaweza kuja kwa njia rahisi, bila kumhonga mtu yeyote yule, huenda hata kwa sasa wanakukataa lakini …

Hii Ndiyo Hali Itakayokuwezesha Kufanya Maamuzi Bora

Bila kuwa na maamuzi bora hatuwezi kuwa na ufanisi bora kwenye vile vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu. Maamuzi bora ndiyo msingi wa matokeo bora, ukiharibu kwenye kuamua umeharibu mchezo mzima. Dunia iko hivi ilivyo, hata wewe uko hapo ulipo leo kwa sababu ya maamuzi ambayo uliwahi kufanya. Hakuna mtu ambaye yuko hapo alipo kwa bahati …

Kitu Muhimu Cha Kuwafundisha Watoto Wako Kwenye Zama Hizi

Iko kauli moja ambayo wazazi wengi wanapenda kuitumia, kwamba siwezi kukubali mtoto wangu apate shida kama nilizopata mimi. Kama Mimi nilipata shida sitokubali na watoto au mtoto wangu apitie shida hii. Kama wazo lako ni hilo basi tayari umeshashindwa mchezo mzima kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kumdhibiti mtu yeyote yule asikutane na changamoto. Kifupi, …

Kama Unataka Kuanza Kufanya Biashara Yoyote Hakikisha Unakuwa Na Hiki

Tafiti za biashara nyingi mpya zinazoanzishwa zinasikitisha sana. Biashara nyingi zinazoanzishwa nyingi zinakufa kabla hata ya miezi sita. Ni watu wengi sana huwa wanaanzisha biashara lakini wanashidwa kukuza biashara zao. Wengi wanaanzisha miradi lakini miradi au hicho walichoanzisha wala hakidumu baada ya muda kina kufa. Nimeshashuhudia katika jamii ninayoishi, wengi wanaanzisha biashara na hazijachukua hata …

Jinsi Ya Kujijengea Nidhamu Ya Muda

Watu ambao bado hawajajitambua na kujua nini haswa wanataka katika maisha yao ni vigumu sana kujua thamani ya muda wao. Masikini anatafuta namna hata ya kupoteza muda na tajiri atafuta namna ya kupata muda zaidi. Masikini wa kwanza ni yule ambaye hajui thamani ya muda wake. Mtu ambaye anajua thamani ya muda wake huyo tayari …

Usipendelee Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Kuna watu katika maisha wanapenda sana mafanikio lakini hawako tayari kulipia mafanikio hayo wanayoyataka.Ukiona mwenzako anafanya vizuri zaidi jua kuwa kuna kitu anakijua zaidi yako au kuna hatua anazochukua halafu wewe huchukui. Kwenye hii dunia ya leo, usipende sana vitu vya bure kwanini nasema hivyo? Vitu vya bure huwa vinakuwa havina thamani. Kama unataka kitu …

Waepuke Marafiki Wa Aina Hii

Siyo kila mtu ni mtu sahihi kwako kuwa naye katika urafiki. Inahitaji umakini kuwa na marafiki sahihi kwako. Iko njia rahisi ya kupata watu sahihi kwako na njia hiyo ni wewe kuwa mtu sahihi. Utakapokua mtu sahihi wale ambao wanahisi wataweza kuambatana na wewe wataambatana na wewe na wale ambao wanahisi hawawezi kuambatana na wewe …

Hiki Ndicho Kinachoweza Kukunyang’anya Mafanikio Uliyonayo

Iko wazi kuwa sisi ni wa miliki wa muda wa vile ambavyo tunavyo. Hakuna kitu ambacho tunacho tunaweza kukimiliki milele. Falsafa inatufundisha kuwa, sisi ni wamiliki wa muda tu wa vile ambavyo tunavyo na iko siku tutakuja kunyang'anywa. Ni kawaida yetu sisi binadamu pale unapopata mafanikio makubwa basi unazalisha kitu kinachoitwa majivuno. Na majivuno haya …

Design a site like this with WordPress.com
Get started