Kumbuka wewe ni binadamu. Kuna wakati unateleza na kufanya kile ambacho unajua kabisa siyo sahihi. Kukosea ni sehemu ya maisha ya binadamu.Dunia isikukulaghai kwa kukujengea hatia katika hali ya kukosea na kujiona haufai. Katika maisha ni muhimu kuwa na nidhamu. Nidhamu ni daraja la mafanikio. Lakini unapaswa kutambua kuwa masharti yakiwa mengi sana yatakubana na …
Hii Ndiyo Aibu Yenyewe
Aliyekuwa mwanafalsafa wa ustoa na mtawala wa Roma Marcus Aurelius katika kitabu chake cha meditations anatushirikisha kauli hii, "Aibu: roho kukata tamaa wakati mwili bado una nguvu" Hii kauli imenitafakarisha sana na mwandishi Robin Sharma anasema ni moja ya mstari anaoupenda sana. Kumbe, ukikata tamaa wakati una nguvu hiyo ni aibu kubwa. Je, ni mara …
Eneo Ambalo Watu Wengi Wanaliibia Muda
Ni eneo la mapumziko. Watu wanalala lakini wakiamka wanakuwa wamechoka na wanakuwa wanasinzia kwenye magari hata makazini. Mwili wako unahitaji mapumziko ya kutosha ili uweze kupata ufanisi na kupambana na mafanikio yako. Heshimu muda wako wa mapumziko, ukipanga kulala basi lala kweli. Uwe na muda maalumu wa kulala kila siku, kama wewe ni wa masaa …
Kuwa Na Kwanini Kubwa Kama Unataka Kufika Mbali
Watu Wanapenda Kusikia Vitu Hivi Kwenye Safari Ya Mafanikio
Wanapenda kusikia vitu vizuri na vya kuhamasisha.Lakini kwenye uhalisia wa mafanikio mambo ni tofauti kabisa. Watu wanapenda kuona matokeo mazuri lakini hawataki kusikia mchakato wa mafanikio makubwa. Mchakato wa mafanikio yoyote yale una maumivu ndani yake. Hakuna mafanikio utakayopata bila kuwa na maumivu ndani yake. Mafanikio pia yana maana tofauti, mafanikio yana maana pana sana, …
Continue reading "Watu Wanapenda Kusikia Vitu Hivi Kwenye Safari Ya Mafanikio"
Sifa Kubwa Ya Maandalizi Mazuri
Kila mmoja wetu huwa anafanya maandalizi kwenye maisha yake. Jambo lolote lile linalokuwa mbele yetu, kibinadamu lazima tuandae mazingira ya namna ya kukabiliana na jambo hilo. Maandalizi ni kitu muhimu sana kwa sababu kupitia maandalizi mazuri ndiyo yanaweza kutuwakilisha sisi vizuri. Bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi mazuri. Hivyo basi, ili uweze kukutana na …
Jifunze Namna Ya Kuwa Na Fedha Nyingi
Kila mmoja anapenda fedha kwa sababu fedha ni muhimu inatusaidia kuendesha maisha yetu pamoja na kulipa bili mbalimbali. Kwenye kitabu cha Biblia kinasema fedha ni jawabu la mambo yote. Lakini, fedha ni ulinzi. Kumbe basi, fedha ni muhimu sana kwetu na hilo halina ubishi. Usisubiri mpaka uwe tajiri tayari ndiyo uanze kujifunza kuwa na fedha …
Kuwa Makini Na Kitu Hiki
Na kile unachokiwaza sana. Kwa nini?Kwa sababu kile unachokiwaza au kukifikiria sana huwa kinakuja katika uhalisia wa kawaida. Mawazo yako huwa yanaumba kile unachotaka kwenye maisha yako. Kama unakitaka kitu, kifikirie sana kile kitu na utashangaa kinatokea. Akili zetu ni kama sumaku huwa zinavuta kile tunachokifikiria muda mwingi. Usipoteze nguvu zako kuwaza kitu ambacho hukitaki. …
Hakuna Kilichokamilika
Kifupi rafiki yangu, hakuna kitu chochote kile ambacho kimefikia ukamilifu ambao hakiwezi tena kuboreshwa. Kila kitu kinaweza kikaboroshwa na kuwa bora zaidi. Hata hapo uliposema kuwa umefikia ukomo, unaweza ukaenda hatua ya ziada tena. Hakuna kazi ya sanaa iliyokamilika, unaweza ukaiboresha kila siku na ukapata matokeo bora. Kiasili kila kitu ni kazi endelevu, ambayo unaendelea …