Jinsi Ya Kuinunua Dunia

Mpendwa rafiki, Hongera sana kwa mwezi julai, natumaini umeshaona mpaka sasa unakwenda wapi na unatoka wapi hivyo ni siku nzuri sana leo kukaa chini na kutafakari kama unabadilisha gia au unaendelea na gia yako kama unaona inakupa kile unachotaka. Kazi kubwa ya kila mmoja wetu hapa duniani ni kuijaza dunia. Kila mmoja wetu ana thamani …

Njia Mbili (2) Za Kuongeza Mauzo katika Biashara Unayofanya

Mpendwa rafiki, Najua kuna kitu unauza kwani maisha yetu ili tupate kitu au thamani katoka kwa mwingine ni kuuza. Kuuza ndiyo habari ya kila biashara, hata kama umeajiriwa au umejiajiri kuna kitu unauza kama siyo bidhaa basi unauza ujuzi wako na watu wanakulipa kadiri ya thamani unayoitoa sokoni. Katika biashara mteja ndiyo mfalme kwani bila …

Hakuna Juhudi Ya Aina Hii Iliyowahi Kupotea Bure

Mpendwa rafiki, Natumaini kila mtu kuna juhudi fulani anaziweka katika maisha yake ili aweze kupiga hatua kubwa katika maisha yake. Maisha ambayo mtu haweki juhudi yoyote ya kuwa bora yanakuwa maisha ya hovyo na ya kawaida sana.  Na hakuna kitu kibaya kama watu kukuchukulia wewe ni mtu wa kawaida, kawaida maana yake huna jipya wewe …

Hiki Hapa Ndiyo Kitu Kinachogharimu Watu Wengi

Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na mengi sana, yapo ambayo yanakuja yakiwa ndani ya uwezo wetu na yale ambayo yako nje ya uwezo wetu. Haya yote yanatokea katika maisha yetu ni ya kwetu sote. Wako watu ambao wanapoteza hata uhai wao au kukosana na rafiki, ndugu,kwa sababu tu ya kuonyana na kuambiana ukweli. …

Mambo Manne(04) Muhimu Ya Kumfundisha Mtoto Wako

Mpendwa rafiki, Tunaishi katika zama kiasi kwamba mtoto mdogo ana uwezo wa kuona kila kitu anachotaka kuona kama akiishi katika mazingira wezeshi. Wazazi wanajitahidi kweli kuzaa watoto lakini katika malezi huwa wanajisahau sana na ubize huu wa kila siku unawafanya watu washindwe hata kukaa na watoto wao kujua hata maendeleo yao. Ni kweli dunia imetukamata …

Kuanzia Leo Acha Kuimba Wimbo Huu

Mpendwa rafiki yangu, Unafikiri ni wimbo gani huo rafiki nao kuambia acha kuimba? Natumaini kuna wimbo unaopenda kuimba na kama siyo kuimba basi hata kusikiliza kwa sababu dunia yetu ni dunia ya kifasihi hivyo kwa namna yoyote ile hatuwezi kukwepa fasihi kwani fasihi ndiyo maisha yetu ya kila siku yanayoelezea uhalisia wake. Ziko nyimbo nyingi …

Ifahamu Sumu Inayoua Biashara Nyingi

Mpendwa rafiki, Mfumo wa biashara unafanya kazi kama vile mwili wa binadamu unavyofanya kazi. Mwili wa binadamu ukikosa damu basi binadamu naye ataweza kufa. Vivyo hivyo kwa biashara kama imekosa fedha za kujiendesha lazima itakufa pia kama ilivyo katika mwili wa binadamu. Kuna kitu ambacho wafanyabiashara wengi wanafanya wakijua kuwa wanawafurahisha wateja kumbe ndiyo wanawafukuza …

Kuwa Na Uvumilivu Wa Vitu Vyote Lakini Cha Kwanza Kiwe Hiki

Mpendwa rafiki, Kila mtu katika safari yake ya mafanikio kuna magumu anayopitia na usione watu wako kimya ukazani hawana matatizo bali wanayo ila hawatangazi kwa kila mtu. Unapata magumu kadiri ya mambo makubwa unayojaribu kufanya katika maisha yako. Kama unafanya mambo ya kawaida sana utaendelea kupata matokeo yale yale ya kawaida. Tunafanya mambo kwa kawaida …

Je Umechoshwa Na Nini Kati Ya Hivi Hapa

Mpendwa rafiki yangu, Ni kawaida yetu sisi binadamu na hata kitu chochote kuchoka pale kinapotumika kufanya kazi fulani. Binadamu sisi asili yetu ni kufanya kazi na siyo kuongea tu. Kila kiumbe kinafanya kazi ili kiweze kujipatia chakula na mahitaji mengine mengi kadiri ya mtu. Kama tunavyojua kazi ndiyo msingi wa maendeleo yako kam hutaki kazi …

Usikubali Kitu Hiki Kikuharibie Utulivu Wako Wa Akili

Mpendwa rafiki, Unaweza ukaamka ukainza siku yako vizuri kabisa lakini kikaja kitu kidogo kikakuharibia asubuhi yako na ukaiona siku mbaya. Lakini kama mwanafalsafa hutakiwi  kuyumbishwa na kitu chochote kile hata kama unamepata changamoto gani bali unatakiwa ubaki katika hali yako bila kutaharuki. Hakuna anayeifanya siku yako iwe mbaya au nzuri bali wewe mwenyewe ndiyo unaamua …

Design a site like this with WordPress.com
Get started