Kwanini Hupaswi Kumuonea Mtu Wivu Pale Anapopewa Heshima

Rafiki, Falsafa ya ustoa inatufundisha mengi , mwanafalsafa Epictetus katika kitabu chake cha hand book of Epictetus ametufundisha kitu kimoja kizuri ambacho mimi na wewe tunaalikwa kujifunza. Ni kawaida binadamu kuwa na wivu, kwa sababu binadamu wengi wanaendeshwa na hisia kuliko akili. Hatupaswi kuwaonea wivu wale waliofanikiwa kwa sababu vile walivyo jua kuna gharama ya …

Hii Ndiyo Sehemu Pekee Ambayo Upendo Huwa Unapenda Kukaa

Mpendwa rafiki yangu, Hakuna falsafa kubwa duniani kama upendo, ukiweza kuishi kwa upendo utaweza kushika amri zote. Karibu dini zote duniani zinashikilia falsafa ya upendo. Katika upendo tunapata kila kitu, upendo ndiyo asili ya dunia na tunapokwenda kinyume na upendo huwa tunapata shida. Kila mtu anajua ni kwa jinsi gani upendo ulivyokuwa na nguvu, kama …

Jinsi Ya Kuishi Muda Mrefu

Mpendwa rafiki yangu, Kila mmoja wetu anapenda kuishi muda mrefu hapa duniani. Licha ya kuwa tunapenda kuishi muda mrefu hapa duniani tukae tukijua kuwa iko siku tutakufa. Iko mbinu ya kuishi muda mrefu ambayo ukiitumia kwenye maisha yako kuanzia sasa utakapojifunza hapa utafanikiwa sana. Aliyekuwa mwanafalsafa wa falsafa ya ustoa Seneca  enzi za uhai wake …

Jinsi Ya Kujenga Tabia Yoyote Ile

Mtu mmoja alishawahi kusema, tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengeneza sisi. Jinsi ulivyo ni matokeo ya tabia ambazo umejitengenezea wewe mwenyewe. Tabia yoyote ile haijengwi kwa siku moja. Bali yale mazoea tunayoanzisha ya kupendelea kufanya mara kwa mara unajikuta tayari imeshakuwa tabia. Kwa mfano, huna tabia ya kuweka akiba, unachukua hata shilingi mia mbili unakuwa …

Hiki Ndicho Kinachokufanya Ujiumize Kwenye Jambo Fulani

Huwa tunajiumiza sisi wenyewe kwa kujua au kutokujua. Tunatengeneza picha ya vitu ambavyo siyo vya uhalisia kisha zile picha zinakuja kututengeneza. Hakuna tofauti na vile mtu anapotengeneza tabia yeye mwenyewe kisha tabia zile zile alizozitengeneza zinakuja kumtengeneza na yeye. Huwa tunajipa maumivu sisi wenyewe, pale ambapo tunapoona tukio fulani limetokea basi tunaanza kujihukumu sisi wenyewe …

Kitu Muhimu Cha Kujifunza Kutoka Nelson Mandela

 Aliyekuwa raisi wa south Africa Nelson Mandela  ni moja mtu muhimu ambaye tunaweza kujifunza kutoka kwake juu ya msamaha. Alifungwa gerezani kwa miaka 27 lakini baada ya kutoka gerezani aliweza kuwasamehe watesi wake waliomfunga. Hakutaka kulipa kisasi juu yao bali kisasi aliamua kumwachia Mungu. alisema kuwa asipowasamehe wale waliomfunga atakuwa bado yuko gerezani. Ni mara …

Jinsi Ya Kukuza Kipato Chako

Mpendwa rafiki yangu, Ni kawaida ni sheria kuwa mtu unalipwa kadiri ya thamani unayoitoa sokoni. Kama kipato chako ni kidogo basi huenda thamani unayotoa ni ndogo pia. Bila kuwa na kipato kizuri huwezi kufanya kile unachotaka kufanya, muda mwingine una mawazo mazuri lakini unashindwa kuyafanyia kazi kwa sababu ya kipato kidogo. Licha ya wengine kuwa …

Utaacha Vitu Gani Kati Ya Hivi Viwili Pale Utakapokufa

Mpendwa rafiki yangu, Kila mtu atakufa hilo liko wazi. Je tukifa tutawaachia nini wale ambao tumewaacha duniani? Kama hakuna kitu ulichofanya, dunia itakusahau haraka sana ila kama kuna kitu umekifanya dunia itakulilia sana na kukukumbuka kwa yale mazuri uliyofanya. Je ukifa utaiachia nini familia yako? Kuna watu wakifa wanaiachi familia zao shida. kwa mfano, wanaziachi …

Jinsi Ya Kumjua Mtu Anayetaka Au Asiyetaka Kufanya Jambo Fulani

Tunaishi  na viumbe wenye akili sana ambao ni binadamu. Kuishi na binadamu vizuri inahitaji akili sana, ukishawajua watu ni rahisi sana kuishi nao hawatakuumiza kichwa hata siku moja. Ziko njia mbili za kumjua mtu anayetaka au asiyetaka kufanya jambo fulani, ni rahisi sana tu kwani ukishamsoma mtu utajua yuko upande gani. Kwanza, kama mtu anataka …

Sehemu Tatu Unazopaswa Kujifunza Zaidi Ili Kuwa Bora

Mpendwa rafiki yangu, Zama zimebadilika sana, kama usipokuwa bora utashindwa kuishi kwenye dunia ya leo. Unatakiwa kujifunza kila siku kadiri ya mabadiliko yanayoendelea kutokea. Kuna maeneo matatu ambayo kama kila mmoja wetu akiweka nguvu ataweza kufanikiwa sana. Ni maeneo ya kawaida kabisa ambayo kila mmoja wetu anaweza kujifunza na kuwa bora kisha akafanikiwa kwenye kile …

Design a site like this with WordPress.com
Get started