Watu wengi hawana uvumilivu katika kuchangia mambo kwa hoja. Wengi wanapenda kushindikiza kitu ambacho wao wanaona kinafaa kwa mabavu na siyo hoja. Kokote pale utakapokuwa usishawishi watu kwa mabavu bali kwa hoja. Muoneshe mtu faida ya kile unachotetea na kwanini akubaliane na wewe. Pia ni rahisi kumshawishi mtu lakini maamuzi bado yako mikononi mwake kuamua …
Category Archives: Uncategorized
Hivi Ndivyo Unavyopaswa Kuwa Imara
Kama mpaka leo unalalamika juu ya magumu au changamoto, jiambie kuwa magumu au changamoto ni sehemu ya maisha ya kila binadamu ambaye anavuta pumzi.Hivyo , kukwepa changamoto ni kukwepa maisha yako. Hivyo basi, unapaswa kuwa imara kama vile maji. Maji ni kitu cha ajabu sana kina nguvu kupita maelezo. Kizuizi chochote utakachokiweka kwenye maji, maji …
Umiza Kichwa
Kama unataka kufanikiwa basi kuwa mtu wa kuumiza kichwa, yaani siyo uchukue kitu ujipige kichwani hapana, bali kuwa mtu wa kufikiri kwa kina. Kuna mambo ambayo yanatokea katika maisha yetu ni kwa sababu ya watu kutokuumiza kichwa. Kwa mfano, mtu akijiona hana fedha, hafikirii namna nyingine ya kupata fedha bali anafikiria kukopa. Watu wengi wana …
Kitu Chochote Unachotegemea Kutoka Kwa Wengine Hakikisha Unakuwa Hiki
Huwa tunaweza kupanga sisi wenyewe lakini tunapangua sisi wenyewe. Tunakuwa tunaweka mipango yetu huku tukiamini kuwa mambo yataenda kama vile tunavyotaka sisi. Tunapoweka malengo yoyote, au kitu chochote ambacho tunahitaji kukikamilisha lakini kinafanywa na wengine jiwekee nafasi ya mambo kutokwenda kama vile unavyotaka wewe. Jiwekee nafasi ya kuangushwa, usijiwekee uhakika kabisa kwamba kile nilichopanga kitaenda …
Continue reading “Kitu Chochote Unachotegemea Kutoka Kwa Wengine Hakikisha Unakuwa Hiki”
Huyu Ndiye Mtu Masikini Duniani
Huwa tunafikiria kuwa mtu masikini ni yule ambaye hana fedha mfukoni. Kwanza , umasikini hauanzii mfukoni wa mtu, bali unaanzia kwenye akili. Akili huwa ikilala basi na mwili unalala. Unapotumia akili yako vizuri itakusaidia vizuri. Mtu masikini kuliko wote duniani ni yule ambaye hana maono makubwa. Dunia iko hivi ilivyo leo kwa sababu ya watu …
Haya Ndiyo madhara Ya Kujikata Wewe Mwenyewe
Watu wa nje hawawezi kukukataa isipokuwa wewe mwenyewe ukijikataa kwa ndani. Ukishajikatalia kwa ndani hata nje watu watakuchukulia hivyo hivyo. Mafanikio yoyote yanaanzia ndani yetu, usipokuwa ndani vizuri basi hata nje utakua vibaya. Unakuwa vile unavyoonekana ndani kadiri ya wewe unavyojichukulia. Unaweza kujiona huna maana, kama wewe mwenyewe umejiwekea mtazamo huo. Unaweza kujiona wewe kuwa …
Continue reading “Haya Ndiyo madhara Ya Kujikata Wewe Mwenyewe”
Funguka Leo
Kama umekuwa na akili iliyofungwa basi leo funguka.Akili yako unaifunga kwa kufikiria vitu vidogo sana na kujishusha chini. Fikiri nje ya box na fikiri mambo makubwa na usiipe akili yako mipaka katika kufikiri mambo. Jione ni mtu ambaye unaweza bila kujali cheo, umri au wadhifa ulionao pale ulipo. Tunajiwekea mipaka kwa kusikiliza watu wengine, kwamba …
Usishindande Bali Fokasi Katika Mtu Huyu
Kushindana katika mafanikio ni njia rahisi ya kusahau malengo yako na kujiandaa kushindwa. Unaweza ukashindana na mtu ambaye wala hashindani wewe na pia malengo yake na yako hayafanani hata kidogo. Badala ya kushindana na watu, wewe shindana na wewe mwenyewe. Pambana na malengo uliyojiwekea. Angalia vipau mbele vyako na pambana navyo. Katika ushindani wa kibiashara …
Waambie Wengine Changamoto Zako
Hakuna changamoto mpya hapa duniani, kila changamoto unayokutana nayo basi kuna mtu tayari alishaipitia na ana suluhisho nayo. Rai yangu ni kwamba, ukiwa na changamoto usiwe kama bubu kwa kukaa kimya bali jaribu kuongea na wenzako.Unaweza kukiona kitu ni kigumu sana kwako lakini kwa mwenzako ni rahisi sana. Ndiyo maana leo nakusihi sana usikae na …
Hiki ndiyo kitu pekee cha kufanya au kujali pale tu unapopata Mshahara au Fedha
Heri ya mwezi Februari rafiki yangu, Wote tunajua kuwa fedha ni muhimu sana katika maisha yetu, na hilo halina ubishi. Huwa tunafanya kazi kwa shida lakini cha ajabu tunakuja kutumia fedha tuliyoipata kizembe. Cha ajabu ni kwamba, pale tunapopata mshahara, fedha au kipato chochote kile huwa tunafikiria kuwalipa watu wengine na kujisahau sisi wenyewe. Sasa …
Continue reading “Hiki ndiyo kitu pekee cha kufanya au kujali pale tu unapopata Mshahara au Fedha”