Haya Ndiyo Matokeo Ya Kutowaambia Watu Kile Unachofanya

Bilionea na raisi wa Marekani Donald Trump kwenye moja ya nukuu zake anasema hivi, Kama hutowaambia watu juu ya mafanikio yako basi hakuna atakayejua. Mimi leo nataka nikuambie hivi rafiki yangu, kama hutowaambia watu kile unachofanya au unachouza hakuna atakayejua unafanya nini hivyo ni wajibu wako kuwaambia watu kile unachofanya au unachouza ili upate wateja. …

Hiki Ndicho Kinawafanya Watu Wengi wasifanikiwe

Sheria ya asili inatufundisha kuwa hatuwezi kufanikiwa bila kutoa. Kumbe basi, unapotoa ndiyo unapokea na watu wengi hawaijui siri hii ya mafanikio. Toa nikupe ndiyo asili ya dunia na kama mtu huwa anataka kupokea tu huwa anabaki kama alivyo maana huwezi kupiga hatua kubwa kama wewe ni mtu wa kutaka kupokea bila kutoa. Kinachowafanya watu …

Jenga Tabia Hii Moja Itakayosaidia Kuboresha Mahusiano Yako

Kwa zama tunazoishi sasa kumekuwa na kelele nyingi sana kiasi kwamba zinaweza kukusaulisha hata mambo muhimu unayopaswa kuyafanya katika mahusiano tuliyokuwa nayo. Kwanza kila mtu yuko bize na maisha yake hivyo usipokuwa makini katika kujenga mahusiano yako unaweza kuwapoteza wengi. Leo tunakwenda kujifunza tabia moja tunayopaswa kuwa nayo ili tujenge mahusiano yetu na tabia hiyo …

Hii Siyo Kazi Yako Kujua

Katika misingi ya falsafa tunaalikwa kuishi maisha yetu vizuri kama vile leo ndiyo siku yetu ya mwisho.Tunaalikwa kuishi kikamilifu kila siku badala ya kupoteza muda kufikiri juu ya kesho itakuwaje. Wako watu ambao wanajikuta wanafikiria kesho itakuwaje hii inawafanya washindwe kuishi leo vizuri. Ukweli ni kwamba hakuna anayeijua kesho hivyo kuihofia kesho ni kupotezamuda. Wewe …

Nadharia Iliyopitwa Na Wakati Katika Uongozi

Kila mmoja wetu ni kiongozi, Kama siyo kiongozi katika familia yako, taasisi basi ni kiongozi wa maisha yako mwenyewe. Kama unaweza kujiongoza basi unaweza kuwaongoza wengine. Iko njia rahisi sana katika uongozi ambayo kila kiongozi anatakiwa kuitumia ambayo ni ishi kile unachosema. Ukiwa ni mtu tu wa kusema halafu na wewe huishi kile unachosema watu …

Ukitaka Kupata Shida Kwenye Mahusiano Yako Fanya Hivi

Kama ukikaa chini na kuchunguza basi utagundua hakuna mtu ambaye yuko salama katika wito aliochagua kuishi yaani kama wewe umechagua kuwa mwanandoa au utawa lazima utakutana na changamoto katika maisha yoyote yale uliyochagua kuishi. Matatizo tunayokimbia katika mahusiano yetu au miito tuliyochagua kuishi ndiyo inatufanya tusiwe bora. Wale ambao wanakimbia changamoto katika maisha yao ni …

Kama Unataka Watu Wakutafute Bila Ya Wewe Kujisumbua

Iko njia rahisi sana ya kujiuza yaani kujitangaza ili watu wajue yale tunayofanya yanaweza kuwa na mchango gani katika maisha yao. Kila mtu huwa ana kitu anachofanya na wengine wanataka kujulikana na watu na hata kupata umaarufu. Haya yote yanaweza kuja kwa njia rahisi, bila kumhonga mtu yeyote yule, huenda hata kwa sasa wanakukataa lakini …

Hii Ndiyo Hali Itakayokuwezesha Kufanya Maamuzi Bora

Bila kuwa na maamuzi bora hatuwezi kuwa na ufanisi bora kwenye vile vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu. Maamuzi bora ndiyo msingi wa matokeo bora, ukiharibu kwenye kuamua umeharibu mchezo mzima. Dunia iko hivi ilivyo, hata wewe uko hapo ulipo leo kwa sababu ya maamuzi ambayo uliwahi kufanya. Hakuna mtu ambaye yuko hapo alipo kwa bahati …

Kitu Muhimu Cha Kuwafundisha Watoto Wako Kwenye Zama Hizi

Iko kauli moja ambayo wazazi wengi wanapenda kuitumia, kwamba siwezi kukubali mtoto wangu apate shida kama nilizopata mimi. Kama Mimi nilipata shida sitokubali na watoto au mtoto wangu apitie shida hii. Kama wazo lako ni hilo basi tayari umeshashindwa mchezo mzima kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kumdhibiti mtu yeyote yule asikutane na changamoto. Kifupi, …

Kama Unataka Kuanza Kufanya Biashara Yoyote Hakikisha Unakuwa Na Hiki

Tafiti za biashara nyingi mpya zinazoanzishwa zinasikitisha sana. Biashara nyingi zinazoanzishwa nyingi zinakufa kabla hata ya miezi sita. Ni watu wengi sana huwa wanaanzisha biashara lakini wanashidwa kukuza biashara zao. Wengi wanaanzisha miradi lakini miradi au hicho walichoanzisha wala hakidumu baada ya muda kina kufa. Nimeshashuhudia katika jamii ninayoishi, wengi wanaanzisha biashara na hazijachukua hata …

Design a site like this with WordPress.com
Get started