Ni ung’ang’anizi. Chagua nini unataka kwenye maisha yako, kisha amua kujitoa maisha yako yote kwenye kile unachotaka mpaka unakipata. Jifunze hata kwa Yakobo, alimwambia malaika wa Mungu sikuachi mpaka unibariki. Siri yake ya ushindi hapa ni ung’ang’anizi, alijua anataka baraka hivyo akang’ang’ana na akapata kile anachotaka. Usitegemee kupata ushindi wowote ule kama hujaweka kazi ya …
Category Archives: Uncategorized
Muombe Mteja Wako Akusaidie Kufanya Haya
Kwenye kazi, biashara au kile unachofanya hakikisha unajua mahitaji ya mteja wako.Hii ndiyo hatua ya kwanza kabisa katika mauzo. Ukishajua mteja wako anataka nini ni rahisi kumhudumia vizuri. Pili mwelekeze mteja kuhusu kile unachouza. Mwambie ni namna gani kile unachomuuzia kinakwenda kuwa suluhisho la changamoto inayomkabili. Mweleze mteja thamani atakayokwenda kuipata pale tu atakaponunua kwako …
Usiache Kumsalimia Mtu Huyu Hapa Kila Mkoa Unapoenda
Kila mmoja wetu huwa ana safiri kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.Mara nyingi tukishafika safari zetu huwa tunaenda kuwasalimia watu mbalimbali lakini tunamsahau mtu mmoja muhimu sana. Kwa kuwa tunao utamaduni wa kutembeleana basi usisite kwenda kumsalimu mtu huyu muhimu. Mtu muhimu unayepaswa kumsalimia kila mkoa unakoenda ni maktaba. Kwenye maktaba zetu za mkoa huwa …
Continue reading “Usiache Kumsalimia Mtu Huyu Hapa Kila Mkoa Unapoenda”
Jinsi Ya Kujishusha Kiroho
Kila mmoja wetu anapenda kuwa na uamsho wa kiroho ndani yake.Kuwa na uamsho wa kiroho ndani yako unahitaji ufanye mageuzi. Sisi wenyewe ndiyo tunakuwa watu wa kujiwekea vizuizi vya kiroho. Tumejiwekea vikwazo na vizuizi vingi. Viko vitu ambavyo tumejiambia tunaweza kuvifanya na kuna vitu vingine hatuwezi kuvifanya. Viko vitu pia ambavyo tunavikubali sana na vingine …
Hivi Ndivyo Unavyojipoteza Mwenyewe
Kwenye haya maisha kama hujajitambua hakika utateseka. Watu ambao hawajitambua kiakili, kimwili na kiroho ndiyo wale ambao wanakuwa chambo kila siku kuwasaidia watu wengine kupata kile wanachotaka kwenye maisha yao. Watu hawataki kuisikia kweli, ndiyo maana uwongo unawaumiza sana kila siku. Ukimwambia mtu ukweli atakuchukia lakini ukimwambia uwongo anafurahia. Hapa ndiyo naposema asiyejitambua ni mtu …
Jitenge Na Fedha Hizi
Hata kama biashara ni yako lakini siyo kigezo cha kukustahilisha wewe kutumia fedha za biashara vile unavyotaka wewe. Biashara na wewe ni vitu viwili tofauti. Unatakiwa utofauti kati ya wewe na fedha za biashara. Jitenganishe kati ya wewe na fedha za biashara. Ukiwa na biashara yako hakikisha unafuatilia namba muhimu sana.Jua mtaji unaozunguka kwenye biashara …
Faida Ya Kucheza Uwanja Wa Nyumbani
Ukiwa unaishi kwa misingi uliyojiwekea maisha yanakuwa bora sana. Usipokuwa na misingi unayoisimamia maisha yanakuwa ya hovyo sana. Kilichowasaidia wanafalsafa kuwa bora ni kuwa na misingi inayowaongoza kwenye kile wanachofanya. Kama unasoma hapa na huna misingi inayokuongoza kwenye maisha yako, hakikisha unakuwa nayo ili uweze kujiongoza vizuri. Dunia ya leo bila misingi utachelewa kufika kule …
Jibu Hili Swali Na Utapata Hamasa Kwenye Kile Unachotaka
Njia ya kwanza ya kupata hamasa kwenye maisha yako ni kupitia kile unachotaka kwenye maisha yako. Ili uweze kufanikiwa hatua ya kwanza ni kujiuliza nini haswa unataka kwenye maisha yako? Majibu utakayopata hapa yatakuwa yanakusukuma kukupa hamasa ya kuendelea kufanya kwenye kile unachotaka. Swali lingine kubwa ambalo unapaswa kujiuliza baada ya kujua nini haswa unataka, …
Continue reading “Jibu Hili Swali Na Utapata Hamasa Kwenye Kile Unachotaka”
Kanuni Ya Almasi Inayotufanya Tusiwe Sawa
Kuna kanuni moja ya dhahabu iliyoandikwa sana kuanzia kwenye vitabu vya dini mpaka vya kawaida. Ni kanuni nzuri, ambayo inasema hivi, mtendee mwingine kile ambacho wewe unapenda kutendewa. Kanuni hii imekuwa inahubiriwa kwenye nyumba za ibada na nk. Ukiitafakari kanuni hii kwa undani ina mapungufu yake. Kwa sababu kile unachopenda wewe hakiwezi kuwa sawa na …
Continue reading “Kanuni Ya Almasi Inayotufanya Tusiwe Sawa”
Haya Ndiyo Maumivu Ambayo Unaweza Kuyavumilia
Kila mtu anapitia maumivu katika maisha yake. Na hakuna mtu anayeishi bila maumivu. Lakini siyo kila maumivu unaweza kuvumilia. Maumivu ambayo unaweza kuyavumilia ni yale ambayo yana maana kwako. Kama maumivu hayana maana kwako huwezi kuvumilia kitu. Lakini yakiwa yana maana utaweza kuvumilia. Ni mara ngapi kwenye maisha yako unakutana na changamoto?Lakini kuna changamoto nyingine …
Continue reading “Haya Ndiyo Maumivu Ambayo Unaweza Kuyavumilia”