Jinsi Ya Kuteka Mioyo Ya Watu

Ni kuwa bora kuliko wao.Fanya kile ambacho wao hawawezi kufanya. Wala hawategemi hata wewe kama ungeweza kufanya. Unapoteka mioyo ya watu wanakuwa wanakuheshimu sana. Wanakuona wewe siyo mtu wa kawaida, na huenda wakakuogopa kwa mambo unayofanya. Kama kuna mtu anakusimamia kazi, fanya kwa ubora kuliko anavyotegemea. Kama kuna mtu unamfanyia kazi ifanye kwa ubora zaidi, …

Jinsi Ya Kuepuka Kuzaa Roho Wivu

Pale tu unapoanza kuangalia yule ana nini na wewe una nini utaanza kuzaa roho ya wivu. Kwa mfano, Kaini alimuonea wivu mwenzake kwa sababu ya kumtolea Mungu sadaka iliyompendeza. Pale tu unapoanza kujilinganisha na mwingine, iweje yule ana hiki na mimi sina. Unajikuta unazaa roho ya wivu. Wivu ukishazaliwa inazaliwa roho ya chuki. Chuki ikiwepo …

Haya Ndiyo Mambo Unayopaswa Kuhangaika Nayo Siku Ya Leo

Kabla hujaianza siku yako, jipe vipaumbele vyako kwenye siku hiyo. Orodhesha yale unayokwenda kufanya siku hiyo. Ukishamaliza kufanya hivyo sasa jiambie haya ndiyo mambo ninayopaswa kuhangaika nayo siku hii ya leo. Chochote ambacho sijakiandika hapa kwenye orodha yangu, sitajisumbua kuhangaika nacho hata kidogo. Kwa sababu muda wako ni mchache, na huna muda wa kuhangaika na …

Mtu Huyu Akikuita Acha Kile Unachofanya Nenda Kamsikilize

Kuna watu wawili muhimu sana hapa duniani. Hao ni watu ambao wanafanya maisha yetu ya kila siku yaende. Siyo kwamba watu wengine siyo muhimu hapana, kila mtu ana umuhimu wake. Kuna watu ambao wakikuita tu, unatakiwa kuacha mara moja kufanya kile ulichokuwa unafanya na kwenda kuwasikiliza. Watu hao ni bosi au mteja wako. Bosi na …

Hii Ndiyo Raha Ya Kuanza Kile Ulichopanga Kufanya

Tumekuwa ni watu wa kuweka malengo lakini siyo watu wa kufanya. Kama ungekuwa unaweka kazi kwenye kile ulichopanga kufanya leo hii ungekuwa mbali sana. Huenda ukawa unajilaumu muda huu kwa kujiambia laiti ningelijua. Lakini laiti ningelijua haina msaada wowote kwako, kitu pekee cha kufanya ni kufanya maamuzi ya kuanza upya pale ulipokosea. Kuna raha kubwa …

Jinsi Mabadiliko Yanavyokuua

Leo asubuhi nilivyokuwa nasoma kwenye kitabu 5 ZA MAJUMA 50 YA MWAKA nilikutana na tafakari ya kufikirisha kutoka kwa Ray Norda. Ray Norda anasema, sababisha mabadiliko na ongoza mabadiliko.Kubali mabadiliko na utapona kwenye mabadiliko hayo.Kataa mabadiliko au yapinge mabadiliko na mabadiliko yatakuua na kukupoteza kabisa. Mwandishi wa kitabu cha 5 Za Majuma 50 YA MWAKA …

Kabla Hujalala Leo Usiku Jiulize Swali Hili

Watu wengi huwa hawapendi kujifanyia tathimini binafsi je ulishawahi kujiuliza ni kwanini? Kwa sababu, watu wengi hawapendi kujua ukweli. Wanapenda waendelee kujidanganya kwa kujikimbia kila siku. Ukiwa unajifanyia thathimini lazima utakua unajua ni wapi unaenda? Ni bora ujifanyie tathimini halafu ukaujua ukweli. Ukishajua jua ukweli utakusaidia sana kwenye safari ya maisha yako hapa duniani. Watu …

Changamoto Kubwa Ya Mafanikio Iko Hapa

Kila mmoja wetu ana maana tofauti tofauti ya mafanikio. Kila mmoja anapenda kufanikiwa kwenye kile alichopanga kufanikiwa. Leo ni tarehe 4 Januari , huenda umeshaweka malengo yako na mipango yako mbalimbali. Hivi tarehe 4 Disemba utakua bado umesimama kwenye malengo uliyojiwekea? Au utakua umeshaachana nayo? Kumbuka mipango siyo matumizi. Siyo kila kitu kitaenda kama ulivyopanga. …

Hivi Ndivyo Familia Yako Inapaswa Kuwa Mwaka 2021

Kila mmoja wetu ametokea katika familia. Ni nani kati yetu ambaye hajatokea katika familia? Unafikiri ni kwanini kila mtu anatokea katika familia? Kwa sababu ni mpango wa Mungu kila mmoja wetu kutokea katika familia. Lakini sasa, watu wengi hawauenzi mpango huu wa Mungu kiuaminifu. Familia ndiyo mlango mkuu wa maadili duniani. Familia ikioza na jamii …

Huu Ndiyo Mtaji Ambao Tayari Unao Wa Kuongeza Kipato Chako

Aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa John Paul wa pili, enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema,”Hakuna mtu ambaye ni masikini sana ambaye hana kitu cha kutoa, na hakuna mtu ambaye ni tajiri sana ambaye hana kitu cha kupokea” Kwanza kabisa, nikupe siri moja ambayo ulikuwa huijui, duniani hakuna mtu masikini bali kuna akili …

Design a site like this with WordPress.com
Get started