Kila mmoja wetu kwenye maisha ni mshindi kama akiweza kuacha kufanya vitu vifuatavyo;
Moja uvivu, Kama ukiacha uvivu, ukiwa mtu wa kujituma kufanikiwa kwako ni suala la muda tu.
Unajua unapaswa kufanya nini, hivyo fanya ACHA uvivu. Uvivu ndiyo unawafanya watu wengi kushindwa kufanikiwa kwenye jambo lolote lile.
Binadamu ni kwa asili ni wavivu, hivyo ACHA uvivu utatoboa lakini usipoacha uvivu utaishia kutoboa masikio tu.
Kitu cha pili ni kuacha uzembe. Watu wengi hawana umakini, wanaendesha maisha yao kizembe.
Sababu nyingi watu kushindwa kufanya vitu kwa usahihi ni uzembe. Usikubali kuwa mtu mzembe na badala yake jitume kufanya kazi.
Kitu kingine ni ujinga. Kila mmoja wetu ana ujinga hilo halina ubishi.
Ujinga unatoka kwa mtu kuchukua hatua ya kujifunza.
Kama hujui kitu, chukua hatua haraka ya kujifunza. Usikae mbele za watu na kusema kwamba wewe hujui kitu fulani wakati unao uwezo wa kukijua.
Hatua ya kuchukua leo; Ili ufanikiwe epuka ujinga, uzembe na uvivu.
Fanya kazi kwa bidii, ongeza umakini kwenye kila unachofanya na jitume kujifunza zaidi.
Ujinga, uzembe na uvivu ni adui mkubwa wa maendeleo yako.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog