Vitu vyote ulivyonavyo, kuanzia mali, watoto, mke, mume, mama, baba na vingine vyote umeazimwa au kukopeshwa kwa muda.
Asili imekupa kwa muda, inakuambia tu tumia lakini siku ikivihitaji itavichukua.
Kwa mfano, ukiazima kitu cha mtu, unakitumia tu lakini unajua siyo chako na hata ukiambiwa urudishe haitakuuma kwa sababu unajua siyo chako.
Kwa mtazamo huo hapo juu ndiyo dhana ya kifalsafa unayopaswa kuiishi kwenye maisha yako kwa sababu kwa chochote kile ulichonacho, jua siku moja utakirudisha kwa wenyewe, yaani umekopeshwa tu kwa muda.
Unapotegemea kitu kitokee, unakinyima nguvu pale kinapotokea. Hivyo kwa kila ulichonacho sasa, kuanzia watu, mali, kazi, biashara na mengine, jua upo uwezekano wa kuyapoteza muda wowote.
Na hilo linapotokea hutaumia sana kama ikitokea nje ya mategemeo yako.
Na Mwanafalsafa Seneca na Wastoa wamekuwa wanasisitiza, kila kitu tulichonacho ni mkopo kutoka kwa asili. Siku moja tutahitajika kurejesha mkopo huo.
Hivyo wakati wa marejesho unapofika, hatupaswi kushtukizwa. Ndiyo tutaumia maana tulishazoea, lakini maumivu hayo hayapaswi kuwa ya mshtuko kwetu.
Hatua ya kuchukua leo; ishi kwa dhana hii kwamba kila ulichonacho sasa kuanzia watu, mali, biashara, kazi na mengine jua upo uwezekano wa kuyapoteza muda wowote.
Na hata siku ya kitokea yasikuumize wala kukushtua kwa sababu ulishajua yatatokea.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog