Binadamu wote tuna asili ya uvivu na uzembe. Ili maisha yako yaende vizuri lazima kwanza uzikatae dhambi hizi mbili ambazo ni uzembe na uvivu.
Unakuta mtu analalamika hana fedha, mauzo ni madogo kwenye biashara, mshahara ni mdogo lakini hachukui hatua yoyote itakayomwezesha kuwa bora.
Kwa wale ambao ni wauzaji, najua hata wewe ni muuzaji kwa sababu kila mtu ni muuzaji kwa namna moja au nyingine kwa sababu kuna kitu unauza ndiyo maana unapata fedha za kuendesha maisha yako.
Sasa pata picha umekaa kwenye eneo lako la biashara siku nzima, halafu hujapata mteja wa kuja kununua unaanza kulalamika biashara ngumu.
Kupitia mfano huo, kama muda ambao hauna wateja ungeutumia muda huo kuwapigia simu wateja wako wa zamani, au wateja tarajiwa si ungekuwa mbalimbali?
Habari njema ni kwamba, tayari una majina kwenye simu yako, anza nao hao kuwapigia simu wale wote ambao umekuwa na majina yao, waambie kwamba una uza kitu fulani na anapokuwa na uhitaji akaribie kupata huduma au muombe msaada akusaidie watu wengine ambao wanaweza kunufaika na huduma au biashara yako.
Mteja akija kununua kwako, usiache kupata namba ya simu na kuwa na utaratibu wa kuwapigia simu wateja wako, jua wanaendeleaje au kile walichonunua maendeleo yake yakoje.
Tumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako. Fanya masoko na masoko ni kuifanya biashara yako kujulikana.
Kila wakati fikiria umpigie simu nani ambaye utaweza kumshawishi na kununua kile unachouza.
Hatua ya kuchukua leo; Tangaza kile unachouza, hakika watu wanaijua biashara yako ili uweze kuwashawishi na kuwauzia.
Kitu cha mwisho, mauzo ndiyo moyo wa biashara hivyo na ustaarabu pekee kwenye biashara ni kuuza zaidi.
Jitahidi kufanya masoko na uuze zaidi. Kila mtu ambaye anafahamiana na wewe ajue kile unachouza au huduma au biashara unayofanya. Watu wengi hawajui kile wanachofanya.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog