Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuishinda Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Watu

Kila mmoja wetu ni muuzaji. Hivyo katika kuuza lazima ujifunze sana namna ya kuongea na watu vizuri ili waweze kukuelewa kile unachouza.

Watu wengi wanafikiria kuuza ni mpaka uwe na bidhaa hapana, hata kuwa tu na wazo lako na ukaweza kushawishi wengine hapo tayari umefanikiwa kumuuziwa mawazo yako.

Kuuza ni kumshawishi mtu aweze kukubaliana na kile unachomuuzia, aidha unatoa bidhaa, mawazo, kuongea yote hayo kwa pamoja yanaleta mantiki ya mauzo.

Ukitaka kuwa mnenaji mzuri unatakiwa usiwe na hofu katika kuomgea. Na hofu namba moja duniani wanayoiogopa watu ni kuongea mbele ya watu. Watu wengi wanapoambiwa kuongea mbele za watu wanaona ni bora hata kufa kuliko kuongea mbele za watu. Wako ambao jasho linawatoka, wanahisi kubanwa na haja, wanatetemeka na nk.

Je unawezaje kuishinda hofu?

Kwanza unatakiwa ujiamini. Unapojiamini utaweza kuongea mbele za watu vizuri. Usiogope ongea na watu elfu 1 kama unaongea na mtu mmoja. Yaani wewe chukulia unaongea na mtu mmoja hata kama unaongea na watu wengi hii itakupunguzia hofu.

Jipe mazoezi ya kuongea pale mnapokutana zaidi ya wawili na unapoongea ongea vizuri na kuhusisha lugha ya mwili pia.

Pili, fikiria kile unachokwenda kuongea tu. Watu wengi huwa wanafikiria vitu tofauti na vile wanavyokwenda kuongea ndiyo maana watu wengi huwa wanajisahau na kwenda nje ya mada au kusahau hata kile ambacho alipanga kuongea.

Usianze kufikiria vitu kama vile sauti yako wanaisikiaje, nguo ulizovaa, nadhalika. Usiweke akili yako kwenye mavazi bali fikiria tu kile unachotaka kuongeana utakua bora.

Tatu usitumie lugha ngumu, tumia lugha rahisi ili uweze kueleweka na hadhira yako. unapoongea lugha rahisi utafikisha ujumbe kwa urahisi hata wewe mwenyewe utakua unajiamini.

Hatua ya kuchukua leo; jiamini ili uweze kuongea mbele za watu, fikiria kile unachotaka kuongea tu, tumia lugha rahisi unapoongea mbele za watu, waangalie wale unaoongea nao.

Kwahiyo, jifunze namna ya kuuza, na kuongea na watu ni kuuza. Hivyo unapokuwa vizuri kwenye eneo la mauzo ni rahisi watu kukubaliana na wewe na kuwauzia kile unachotaka kuuza. Jifunze kushawishi watu kwa lugha nzuri.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki Na Mwalimu Wako,

Mwl, Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

http://kessydeo.home.blog

deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com

Asante sana

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: