Mpendwa rafiki yangu,
Sisi binadamu ni viumbe wa hisia, na karibu maisha yetu ya kila siku yanaendeshwa na hisia, huwa tunafanya maamuzi kwa hisia mara nyingi sana lakini tunakuja kuhalalisha kwa kufikiri, ukitaka kuamini hilo angalia ni vitu vingapi unavyo ndani ulinunua tu kwa hisia na kwa sasa wala hata huvitumii.
Vitu vingi tunavyofanya tunakua tunafanya kwa sababu hisia zimetutuma kufanya hivyo na siyo kukaa chini na kufikiri kwa kina kwenye kila jambo tunalotaka kufanya.
Ziko hisia mbili ambazo zimewatawala watu kwenye maisha yao. Hisia hizo ni kama ifuatavyo;
Tamaa; kila binadamu anatamaa, na hata juhudi unazoweka kupata kitu fulani ni kwa sababu ya tamaa. Tamaa zinatusukuma sana bila kufikiria kwa umakini tunajikuta tunafanya mambo ambayo hata hatukupangilia kufanya.
SOMA; HIZI NDIYO HISIA MBILI ZINAZOWAONGOZAWATU KUCHUKUA HATUA
Hivyo hisia zetu za tamaa zinatupelekesha bila kufikiria lakini kama ukikaa chini na kukubali kufikiria utaokoa vitu vingi sana. Uwe mtu wa kuhoji kwenye kila tamaa inayokujia na siyo kukubali tu kuendeshwa kama bendera.
Hofu; ziko hofu nyingi sana zinazotutawala, hofu ya kukataliwa, hofu ya kutokuwa na fedha, hofu ya kupoteza nk. Watu wanaamka na kwenda kufanya kazi wakiamini kuwa wakishapata fedha hofu zao zitaondoka. Watu wengi hofu inawasukuma kufanya vitu kwa sababu wasipofanya watapatwa na kitu fulani. Na hata watu wanafanya kazi ili wapate hela, wanajua wasipofanya kazi maisha yao hayataenda vizuri.
Rafiki yangu, hatuwezi kuzizuia hizi hisia mbili za hofu na tamaa bali tunaweza kuzitawala tu. Usikubali kuwa mtu wa kuongozwa na hisia badala yake kuwa mtu wa kutumia akili kwanza. Jambo likitokea tumia kichwa na akili yako kufikiri na siyo kukimbilia kufanya maamuzi bila kufikiri kwanza.
Hatua ya kuchukua leo; hisia zako zisitawale ubongo wako. Hisia yoyote inayokuja kwako unapaswa kuituliza kwanza kwa kufikiri vizuri na siyo kuongozwa na matukio kama yanavyokuja.
Kwahiyo; usiwe mtu wa kukimbizana na hisia maisha yako yote. Amua kufanya mambo kwa njia ya kufikiria na siyo kwa sababu hisia zimekusukuma kufanya hivyo na wewe unafanya. Unao uwezo wa kutawala mambo yote ambayo yako ndani ya uwezo wako.
Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki Na Mwalimu Wako,
Mwl, Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeoblog@gmail.com
Asante sana