Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jinsi Ya Kuwa Na Familia Bora

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa KESSY DEO? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana rafiki kwa zawadi nzuri ya siku hii ya leo kwani kuamka salama ni ushindi mkubwa katika maisha yako hivyo tumia ushindi huo wa uhai kuacha alama siku hii ya leo kumbuka kuwa maisha ni muda. Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa kauli mbiu yetu ya wakati sahihi ni sasa, usisubiri kupewa ruhusa.

Image result for GOOD FAMILY

Mpendwa rafiki, napenda kutumia nafasi kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyoweza kukuandalia. Hivyo basi, kwa namna ya pekee karibu sana tusafiri pamoja kimawazo hadi pale tamati ya kipindi chetu cha leo.

Rafiki, ili tuweze kuwa na jamii bora tunatakiwa tujenge kwanza familia bora. Lakini tunawezaje sasa kuwa na familia bora ili tupate jamii bora? Kitu cha kwanza  tunachotakiwa ni kujenga misingi imara katika familia zetu.

Kila mtu anatamani kuwa na familia bora, hakuna mtu anayeamka asubuhi na kuomba familia yake iwe dhaifu. Jinsi ya kuwa na familia bora ni mchakato mkubwa ambao unaanzia katika misingi iliyojengwa ndani ya familia.

Kama unataka kuwa na familia bora anza sasa kujenga misingi imara katika familia yako. tunafahamu kwamba nyumba bora na imara ni ile yenye misingi imara hivyo hata katika kuwa na familia bora wale waanzilishi wa familia ambao ndiyo wanandoa wanaalikwa kuwa na misingi imara.

Mpendwa msomaji, familia ambayo haina misingi imara haiwezi kuwa bora kabisa kwa sababu kwa dunia ya sasa kama mtu au familia hamna msingi mliyojiwekea wa kuufuta ni lazima utatekwa na ulimwengu. Kanuni ni muhimu sana kama familia inaishi tu haina kitu cha kusimamia ni rahisi kuyumba na kuanguka.

SOMA; Vitu Viwili (02) Vinavyoongeza Mahusiano Katika Familia

Misingi ni kama nguzo katika familia hivyo ukitaka kuwa na familia bora anza kutengeneza misingi bora na familia yako itasimama vizuri. Familia bila kuwa na misingi au kanuni mnazosimamia ni kama bendera fuata upepo haina mwelekeo inasubiri upepo uje ipelekwe tu.

Rafiki, kukosa mwelekeo maana yake mwelekeo wowote utakuchukua. Kuwa na mwelekeo mzuri ambao ndiyo msingi utakaokuwezesha kuufuta lakini bila ya hivyo utajikuta unaingia kwenye kila mtindo wa maisha bila kutegemea.

Hatua ya kuchukua leo, ukitaka kuwa na familia bora , tengeneza misingi bora ya familia yako na usitegemee kuwa na familia bora kama unaishi kienyeji bila kuwa na misingi imara. Misingi imara ya familia inatengenezwa na wanandoa kwa sababu wanandoa ndiyo chimbuko au chemchem ya familia kumbe  basi, tukiwa na ndoa imara na bora tutapata familia bora.

SOMA; Jambo Linaloleta Mpasuko Katika Familia

Kwahiyo, ili tuweze kuwa na jamii bora, familia bora tunatakiwa kwanza tujenge ndoa imara. Chimbuko la jamii tunayoiona leo ni ndoa na hakuna familia bora bila kuwa na ndoa bora. Wito wangu ni kuwaomba watu wote tupende kujisumbua kujifunza tusome vitabu vimeandikwa kwa ajili ya watu na siyo wanyama. Kujipitia kusoma tunaweza kujifunza mengi na kutengeneza falsafa bora katika familia zetu.

Rafiki, kupata vitabu vya mafundisho mazuri yatakayokupa mwongozo mzuri wa kuishi maisha ya furaha na mafanikio makubwa tafadhali BONYEZA HAPA au wasiliana nasi kupitia namba hizi tuweze kukuhudumia 0717101505/0767101505 NA KUJIUNGA NA KUNDI LA MIMI NI MSHINDI BONYEZA HAPA Kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email tafadhali jiunge na kwa kujaza fomu hapo chini ya makala. karibu sana na asante sana.

Nikutakie kila la heri rafiki yangu na fanyia kazi haya uliyojifunza leo.

Ni mimi rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

3 Comments

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: