Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hawa Ndiyo Watu Ambao Hupaswi Kuwakasirikia

Rafiki,

Kukasirika ni asili ya binadamu, hatuwezi kuzuia kutokuwa na hisia za hasira bali tunaweza kuzikabilia au kuzitawala hisia zetu ili tusiweze kufanya mambo ya ajabu. Wote tunajua kuwa tunapokuwa na hisia za hasira huwa fikra zinakuwa chini yaani uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo sana hisia zinakuwa juu.

Ikitokea mtu mzima amekuja na kukufanyia kitu ambacho siyo sahihi kwako lazima utakasirika lakini katika tukio hilo hilo la mtoto akija kukufanyia kitu huwezi kukasirika kwa sababu utajua tu ni akili za kitoto ndiyo zimepelekea kufanya hivyo.

Sasa katika malezi ya watoto, wazazi wengi huwa wanakuwa wanaadhibu watoto kwa hisia. Kama mzazi ukiwa ni mtu wa kukasirika sana kwa watoto basi utakua ni wa kukasirika kila siku na kuwaadhibu vibaya.

Watoto huwa wako katika hatua ya kujaribu kila siku, hivyo wewe utaona wanafanya makusudi kumbe wanajifunza kwa namna yao. Kama mzazi au mlezi yeyote yule hapaswi kuwa mtu wa kuwakasirikia watoto maana utachoka hata kukasirika huko.

HABARI RAFIKI, NAKUKUMBUSHA OFA YA KITABU CHA IJUE NJAA YA WANANDOA INAKARIBIA KUISHA MWISHO NI KESHO. FANYA MALIPO SASA ILI USIPITWE NA OFA HII YA KITABU, BADALA YA KUKIPATA KWA SHILINGI ELFU KUMI LEO NA KESHO UTAKIPATA KWA NUSU BEI YAANI ELFU TANO TU. FANYA MALIPO YAKO KWA NAMBA 0717101505/0767101504. KISHA TUMA EMAIL YAKO ILI UWEZE KUTUMIWA KITABU. ASANTE SANA NA KARIBU SANA

Watu ambao hutakiwi kuwa na hasira nao ni watoto, kwa kuwa wameitwa watoto hivyo wachukulie hivyo hivyo kama watoto na usiwe mwepesi wa hasira wa kutoa adhabu. Mtoto akukufanyai jambo ambalo unastahili kumwadhibu, mwache akae mbali na wewe na subiri kwanza mpaka hisia za hasira ziache ndiyo  uongee naye na utaona huruma baada ya hapo na kuishia tu kumsamehe.

Tusiwe ni wazazi wa hasira, wa kutaka kuwaadhibu watoto kadiri ya misongo ya mawazo ambayo watu wanayo hivyo hasira zinahamia kwa watoto. Tusiwe watu wa kuwaambia watoto maneno mabaya, tuwe marafiki wazuri sana kwa watoto. Tushirikiane nao katika ukuaji wao na kuwaelekeza njia sahihi na wewe tambua kuwa yale anayofanya mtoto nawe ulifanya hivyo unatakiwa kumuelewa.

Hatua ya kuchukua leo; usiwe mtu wa kuwakasirikia watoto, bali wasamehe kadiri walivyo.

Rafiki,Kama mzazi au kiongozi siyo kila kosa unalotoa linastahili adhabu kwa mtoto, muda mwingine mzazi unapaswa kusamehe bila masharti. Msamaha unaleta uhusiano wa awali uliopotea lakini upendo unaongezeka.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: