Mambo 36 Muhimu Unayopaswa Kuyajua Kwenye Kitabu Cha Trump University

Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessydeo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri katika maisha yako. Leo ni siku nyingine bora na ya kipekee kwetu, ni zawadi muhimu sana katika maisha kwenda kufanya kilicho bora na kutegemea kupata kilicho bora. Tuitumie siku hii ya leo kwa nidhamu, uadilifu na kujituma kwenye yale tunayoyafanya.

Image result for TRUMP UNIVERSITY

Rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza wote kwa pamoja yale mazuri niliyokuandalia. Kupitia kona yetu ya uchambuzi wa kitabu leo nitakwenda kukushirikisha uchambuzi wa kitabu cha Trump University. Hiki ni kitabu kizuri mno kilichoandikwa na waandishi zaidi ya watano na miongoni mwa waandishi hao ni kama vile Donald Trump, John R. Burley, Michael E. Gordon, PhD na wengine.

Mambo muhimu niliyojifunza katika kitabu cha Trump university wealth building 101 ni kama ifuatavyo ;
Kitabu hiki Trump anajaribu kuelezea mbinu na uzoefu wake mpaka kufikia Uhuru wa kifedha pamoja na waandishi wenzake.
Karibu tujifunze rafiki;

1. Ili uweze kufanikiwa unatakiwa uwe na shauku kwenye unachokifanya.
Je unafanya nini? Kama unakipenda kile unachokifanya hakuna mtu atayeweza kukukatisha tamaa. Kuwa na mawazo halafu yafanyie kazi ndiyo utafanikiwa kwenye jambo lolote lile. Fanya na penda kile unachokifanya utafanikiwa.

2. Kuwa mtu wa kumililki vitu, kuwa mtu wa kutokata tamaa, kuwa mtu wa kusonga mbele.
Usiwe mtu wa kuruhusu woga Bali jiamini na songa mbele.

3. Fikiri kiupana na kuwa na ndoto kubwa. Unapofikiria kiurefu na kuwa na ndoto kubwa ndiyo upo sehemu sahihi.
Unafikiria kizakayo yaani kufikiria kiufupi na kuwa na ndoto ndogo ni kujiwekea mipaka ya kutofanikiwa.
Fikiri kiukubwa ndiyo mafanikio na kuwa na ndoto kubwa.

4. Wanaposema kuwa maarifa ni nguvu hawajakosea. Yaani knowledge is power. Unatakiwa kuwekeza katika kujifunza kwanza chimba kwa undani kwenye kile unachokifanya au unachotaka kukifanya.
Einstein aliwahi kusema kuwa taswira au maono ni muhimu kuliko maarifa.
Kuwa na maono makubwa lakini usiache kuwa na maarifa pia.

SOMA; Kabla Ya Kusema Ilikuwaje Fanya Kitu Hiki Muhimu Sana Kwenye Maisha Yako

5. Jifunze kile kitu unachopenda kwa undani. Kama unasomea kilimo basi somea kweli kilimo siyo  kusoma ili ufaulu mtihani.

6. Hata siku moja usije ukajidharau huwezi mpaka ujaribu mwenyewe. Jaribu kwa vitendo ndiyo mafanikio yalipo.
Usiseme huwezi kama hujafanya kwa vitendo.

7. Usiogope kuchukuwa vihatarishi yaani take risk, kwani wale wanaogopa changamoto ni wale tu waliojiandikishia kushindwa. Nenda kathubutu na wala usiogope ukindwa utajifunza na hautakuwa kama ulivyo mwanzo.

8. Jifunze kujua hadhira yako. Hadhira yako ndiyo wateja wako kwa mfano, kama uko ofisini na mpo watu wanne basi hao ndiyo hadhira yako.
Ijue vizuri hadhira yako wanataka nini , jifunze, jua na onesha.
Tumia haya maneno, jifunze, jua na onesha.

9. Makubaliano ndiyo biashara na Maisha yetu. Maisha yetu na biashara tunafanya yamebebwa na makubaliano yaani negotiation.
Kwa sababu makubaliano ni kitu muhimu hivyo hatua ya kwanza jua kwanza unataka nini. Jua lengo lako na siku zote lenga kushinda katika makubaliano yako yaani win to loose.

10. Unapofanya makubaliano hakikisha pia unaujua vizuri upande wa pili yaani yule au wale unaofanya nao makubaliano.
Kabla ya kuingia kwenye makubaliano jiandae kwanza na jiandae kushinda.

11. Baada ya kuwajua vizuri upande wa pili utagundua udhaifu wao na uimara wao ni nini.
Kufanya makubaliano bila kujua upande wa pili itakupa ugumu katika makubaliano kwani itakuwa ni ngumu wewe kujua udhaifu wao na uimara wao uko wapi.

12. Muda mwingine unatakiwa kuwa mwanasaikolojia ili uweze kufikia muafaka katika makubaliano. Soma akili za upande wa pili na usijiwekee mipaka mwenye bali jaribu kuangalia shauku na sababu zako. Jifunze kuangalia msawazo wa kila upande ili muweze kufikia muafaka. Muda mwingine kubali kushuka ili uweze kujenga mahusiano endelevu badala ya kujiwekea nafasi ya kushinda kila siku na wengine wanaumia. Kwa mfano, kama ni mteja wako wa kila siku na unajua kama ukitaka ushinde wewe kila siku utaweza kumpoteza inabidi siku nyingine ukubali kushinda ili msibomoe uhusiano.

SOMA;Mambo Saba (07) Muhimu Niliyojifunza Kutoka Kwa Donald Trump

13. Sikiliza dhamira au sauti yako ya ndani inataka nini. Kuna kitu huwa kinakujia bila hata kufikiria kwa kina juu ya kitu Fulani. Kuna ile dhamiri ya ndani inakuambia juu ya kitu Fulani kwa mfano, unaweza kupanga kwenda sehemu Fulani lakini kuna kitu kinakuambia usiende huko au unataka kusafiri roho inakuambia usiende. Kwahiyo, kusikiliza sauti yako ya ndani inasaidia kupata kile unachotaka.

14. Kile unachofanya kweli kinaakisi jinsi ulivyo? Liamini jina lako pale unapofanya kazi watu wajue kweli hili ni jina la fulani. Kazi yako ndiyo utambulisho wako hivyo unatakiwa kujijengea jina yaani Brand yako mwenyewe, kuwa bora. Be your own best Asset.

15. Hela ni hesabu, Abraham Lincoln alisema akitaka kuangusha mti kwa SAA moja atatumia dakika 40 kunoa shoka lake. Kama wewe unataka kufanya jambo Fulani basi, noa kwanza shoka lako, ujifunze sana kabla ya kufanya. Unapaswa kuutumia muda wako vizuri na kama umeamua kujinoa sijui kama utapata muda wa kupoteza na kuangalia TV.

16. Ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi zaidi ya masaa elekezi. Unatakiwa hata kununua muda kutoka kwa watu wengine.
Wote tumepewa masaa 24 kwa siku hivyo kufanya kazi masaa machache huwezi kufanikiwa na kujilinganisha na mamilionea au mabilionea. Muda ni Mali na fedha ni hesabu.

17. Unalipwa kulingana na thamani unayoitoa sokoni.
Kama unazalisha mawazo yenye thamani basi utalipwa na kupokea kulingana na thamani yako.
Chochote unachofanya zingatia kitu kikubwa ambacho ni ubora. Na ubora siku zote lazima uwe na thamani ndani yake.

18. Jifunze mauzo, jifunze masoko kwenye kile unachofanya. Zingatia kuongeza thamani Sana kuliko kufanya kazi sana bila thamani ni kupoteza muda.

19. Kuwa bossi,kuwa mjasiriamali. Anza kufikiria kimilionea ,kibilionea, fikiria makubwa hata kama sasa huna hela.

20. Ujasiriamali ndiyo njia ya kukupeleka kwenye utajiri.
Fanya biashara bora ndiyo njia ya kukupeleka kwenye utajiri.
Biashara na ujasiriamali ni njia bora ya kukupeleka kwenye utajiri.

21. Ili uweze kufurahia utajiri wako ni lazima ujiwekee msingi mzuri wa kuwa na afya na furaha.
Mafanikio yako yatakuwa hayana maana kama huna afya bora. Mafanikio yako yatakuwa hayana maana kama huna afya bora.

22. Afya ya kiroho ni moja ya misingi muhimu unatakiwa uwe nayo. Kuna nguvu kubwa ya afya ya kiroho inayokuwezesha kufanikiwa. Kuwa vizuri katika eneo hili.

23. Fanya kazi unayoipenda. Fanya kazi unayoifurahia pale unaifanya. Utumwa wa siku hizi ni watu wengi kufanya kazi wasizozipenda na hatimaye huzaa manung’uniko makubwa kwenye Maisha.
Kama unafanya usichokipenda basi tambua ya kuwa hakikufikishi mbali.

24. Weka vipau mbele vyako vya siku. Usianze siku kama huna kipaumbele chochote. Kumbuka nidhamu ndiyo itakusaidia kufanikisha yote hayo.

25. Kuwa na maono makubwa. Unapokuwa na maono Makubwa inakuhamasisha na kukupa shauku kubwa. Mawazo ya laki huleta laki na mawazo ya milioni huleta milioni.

26. Soma mipango yako kila siku. Ifanye ndiyo kitu unachokipenda. Uzuri wa kupitia maono ni kukaa kichwani nakuendelea kujikumbusha una deni la kitu fulani.

27. Kusoma kila siku inakuongezea wa mawasiliano na ubunifu mkubwa. Siyo kuongeza misamiati Bali kuwa na uelewa mpana wa mambo hivyo maarifa yanakusaidia kuwasaliana na watu vizuri.

SOMA;Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika kitabu cha Think Like A Champion

28. Changamoto ni kwamba watu wengi hawajui kile wanachohitaji mpaka uwaambie kwanza.
Ukitaka kufanikiwa jua kile unachohitaji kwanza.

29. Katika mauzo jenga uaminifu na uhusiano kwa wale unaowauzia.
Uaminifu unalipa siku zote. Ukijenga mahusiano mazuri ya kujuana kwa kila mmoja ni rahisi sana kumuuzia MTU kwani anakuwa ana imani na wewe.

30. Waelekeze watu kupata kile wanachokitaka katika mauzo, kwa mfano, una uza ving’amuzi vya star times, zuku, na Azam mwelekeze mteja wako kuwa ukinunua king’amuzi cha azamu unapata vitu hivi na hivi siyo kumtajia bei na kumuacha bila uelekeo.

31. MPE mteja wako maelezo ya kutosha pale anapokataa. Maelezo ya kutosha na yakina yatampa mwanga mkubwa. Maelezo yako yawe yanamshawishi juu ya hicho kitu.

32. Baada ya kumpa maelezo ya kutosha kwenye kile unachouza MPE mwongozo wa kuchukua hatua. Kama tulivyoona katika mfano wa king’amuzi, angalia mteja wako ana umri gani, na anapenda nini halafu mchagulie sasa kile king’amuzi kinachoendana na yeye. Kama ni mpenzi wa mpira basi mchagulia kile kinachoonesha mpira.

33.  Noa kwanza shoka lako, ujifunze sana kabla ya kufanya. Unapaswa kuutumia muda wako vizuri na kama umeamua kujinoa sijui kama utapata muda wa kupoteza na kuangalia TV.

32. Baada ya kumpa maelezo ya kutosha kwenye kile unachouza MPE mwongozo wa kuchukua hatua. Kama tulivyoona katika mfano wa king’amuzi, angalia mteja wako ana umri gani, na anapenda nini halafu mchagulie sasa kile king’amuzi kinachoendana na yeye. Kama ni mpenzi wa mpira basi mchagulia kile kinachoonesha mpira.

33. Maono ni ile picha unayoijenga akilini kwako kwa wakati ujao baada ya kufanikiwa kufikia lengo ulilojiwekea. Maono huwa ni mazuri kwani yanakaa na kujengeka akili.

34. Kitu kimoja muhimu kinachochangia kujenga kuwa na mali ni kujiamini wewe mwenyewe na maono yako.
Kuamini huwa inakuja kabla ya kitendo. Wanamafanikio wengi huwa wanaamini kabla ya kufanya kwa vitendo ndoto za Kuamini ni nguvu ya mafanikio.

35. Zungukwa na watu waliofanikiwa. Ili ndoto yako iweze kutimia unatakiwa kukutana na wale watu waliofanikiwa. Kaa na watu chanya wenye malengo ya kufanya mageuzi kwenyeMaisha yako. Ukikaa na watu ambao hawaendani na ndoto yako watakukatisha tamaa.

36. Wengi wanakosa kuwa watu wa msaada ni kwa sababu ya wivu. Wivu ni kujiona wewe ndiyo unastahili kuwa na kitu fulani kuliko mtu mwingine.
Jamii zetu zimetawaliwa na wivu unaoendelea kuwa tafutana kila siku. Ili uwe mtu chanya na wa mafanikio epuka wivu kwani shimo baya kama ukiingia huko.
MUHIMU; KUPATA VITABU VYA KUJISOMEA BONYEZA HAPA.

Kila la heri rafiki,
Rafiki Na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started