Miaka 20 Ijayo

Mchekeshaji Mark Twain aliwahi kunukuliwa akisema, miaka 20 Ijayo utajutia zaidi vitu ambavyo hujafanya leo kuliko vitu ambavyo umevifanya. Acha kuahirisha kufanya vitu kwa sababu yoyote ile kwa sababu baadaye utakuja kujuta zaidi. Acha kuogopa changamoto au kushindwa na jaribu vitu vingi uwezavyo. Ni bora ukashindwa ukiwa umejaribu, kuliko usifanye kabisa halafu ukajiambia umeshindwa. Usisubiri …

Mawimbi Yakitulia Ndiyo Tutajua Nani Anaoga Uchi

Ni kauli ya Bilionea na mwekezaji Warren Buffett. Maana halisi ya hii kauli ni kama vile kusema, muda ukifika utasema ukweli wote. Mtu anaweza akakuambia kitu kwamba anafanya na kumbe hafanyi lakini muda ukifika matokeo yataonekana tu.Mawimbi yakitulia ndiyo tutajua nani anayeoga uchi. Mtu anaweza kukuambia yeye ni mwaminifu lakini ukitaka kuamini hilo, subiri mawimbi …

Tambua Michango Ya Watu Wengine

Rafiki, Hakuna jeshi la mtu mmoja kwenye maisha yako. Isifikie mahali ukasema umefika hapo ulipo wewe mwenyewe. Kuna watu ambao wamekusaidia wewe kufika hapo ulipo. Tambua michango ya watu wengine kwa namna ambavyo wamekusaidia wewe hapo ulipo sasa. Wako ambao wanafanikiwa kwa bahati, kwa sababu bahati nayo inahusika katika mafanikio lakini hujaipata bahati hiyo bure …

Epuka Kuwa Mzigo Kwa Wengine

Rafiki, Sehemu yoyote ile unayokuwepo, penda kuonekana mtu wa msaada na siyo mzigo.Kuwa mzigo ni ile hali ambayo watu wanakuona kama vile huna thamani.Mtu ambaye hana thamani maana yake ni mtu ambaye hana mchango anaotoa sehemu fulani. Kuwa mtu wa thamani na siyo mzigo.Anzia kwa mwenza wako, asikuone ni mzigo kuwa na wewe bali akuone …

Ukijua Kitu Hiki Basi Umeshafanikiwa

Huwezi kutatua tatizo usilolijua, ukijua kile kinachokuzuia wewe kuwa hivyo ulivyo ni rahisi sana kupata suluhisho lake. Mtu mmoja alishawahi kusema, jua ni wapi ukienda utakufa na kisha epuka kwenda sehemu hiyo.Kwa lugha rahisi ni kwamba jua ni kitu gani ukifanya kitakuletea shida na kisha epuka kufanya kitu hicho. Jua nini ukifanya kinapelekea biashara yako …

Ni Bora Kuonewa Wivu Kuliko Kuonewa Huruma

Rafiki, Kila unapoamka asubuhi na umepata bahati ya kupumua, shukuru na kisha nenda kaitumie hiyo pumzi uliyopata vizuri sana. Usipojituma kwenye kitu chochote kile, utajiweka katika mazingira ya watu kukuonea huruma, kulingana na hali unayopitia unatengeneza mazingira watu wakusaidie kwa kutia huruma. Usikubaliane na hilo, pambana kuhakikisha unakuwa bora ili usije kupata fedhea ya kutaka …

Unapaswa Kuwa Na Hasira Hii

Mtakatifu Agustino wa Hippo, aliwahi kunukuliwa akisema, Mungu aliyekuumba pasipo wewe kupenda hawezi kukubadilisha pasipo wewe kupenda. Kwa kauli hiyo, tunajifunza kwamba, hapa duniani kuwa hivyo ulivyo sasa ni machaguo yako. Ukitaka maisha mazuri au mabaya ni maamuzi yako wewe mwenyewe.Hakuna mabadiliko yoyote yatakayokuja kwako pasipo wewe mwenyewe kupenda mabadiliko hayo. Ukiamua kuwa yoyote yule …

Kinachotoa Mrejesho Kuhusu Thamani Tunayotoa

Rafiki, Asili haina huruma kabisa na mtu, ikiamua kufanya inafanya vile inavyotaka. Kuna wakati unaweza ukaandaa na kutoa thamani juu ya kitu fulani lakini soko likakataa. Unakuwa na shauku kubwa katika mchakato wa kufikia malengo fulani lakini unapofika sokoni, soko linaamua tofauti na ulivyopanga. Tunapaswa kuelewa kwamba, tunaweza kujiandaa vizuri lakini soko likaamua vingine. Tunaweza …

Usiwe Na Makasiriko

Rafiki, Ukitaka maisha yako yaende vizuri, usiwe na makasiriko na maisha au mafanikio ya watu wengine. Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa kama kuchukia mafanikio ya wengine. Badala ya kuwachukia watu waliofanikiwa pambana na wewe uweze kufanikiwa kwa sababu inawezekana pia. Hivi unajua kwa nini masikini wengi huwa hawawi matajiri, kwa sababu wanawachukia matajiri, kwa sababu …

Usiogope Mabadiliko Kama Utakutana Nayo

Rafiki, Mabadiliko ni kitu ambacho hakikwepeki kwenye maisha, kama wewe utagoma kubadilika, basi mazingira yanayokuzunguka yatabadilika.Na pale unaposhtuka na kugundua mazingira yamebadilika, basi jua umeshaachwa nyuma. Watu wengi wamekuwa wanaogopa kufanya mabadiliko kwenye maisha yao kwa sababu mabadiliko ni magumu. Mabadiliko huwa yanaleta hali fulani ambayo hatujaizoea. Pia mabadiliko yanamaanisha kuachana na kitu ambacho mtu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started