Mazuri Unayofanya Yanadumu Milele

Rafiki, Kuna mazuri mengi unayofanya na wakati mwingine unaweza kuona hakuna anayejali.Hata kama watu hawakuambii kuhusu mazuri unayofanya jua mazuri yako wanayaona na wananufaika nayo. Kuna wengine hata uwaguse vipi kamwe hawawezi kushukuru. Kuwa kama asili au Mungu anatufanyia mengi lakini siyo wote wanaomshukuru kwa mazuri hayo.Hata wewe unapaswa kulielewa hivyo. Ng'ombe wanazalisha maziwa kila …

Naomba Unisaidie Kitu Kidogo

Rafiki yangu nikupendaye, Sisi binadamu ni viumbe vya ushirikiano. Hakuna jeshi la mtu mmoja. Ili mambo yako yaende, yanahitaji watu wengine.Maisha ni watu. Hivyo tunaishi kwa ushirikiano. Ushindi au mafanikio unayoyatafuta kwenye maisha yako utayapata kutoka kwa wengine. Kuna vitu ambavyo wewe unavyo mwingine hana. Vivyo hivyo kwa mwingine. Mwingine ana kitu, ila hana fedha. …

Siri Kuu Ya Kufanya Makubwa

Rafiki, Kila mmoja wetu anapenda kufanya makubwa. Na wakati mwingine tunapokuwa tunaangalia makubwa waliyofanya wengine, tunaona na sisi hatuwezi kufanya. Lakini iko njia rahisi ya kufanya makubwa. Na siri kuu ya kufanya makubwa ni ; Moja ni kuwa na ndoto kubwa. Mbili ni anza kidogo. Na tatu chukua hatua. Acha kufikiria ukomo au unachokosa na …

Ondoa usumbufu Huu ili kupata Ufanisi Kwenye Kile Unachofanya

Rafiki, Tunaishi kwenye zama za usumbufu. Usipokuwa makini na zama hizi utajikuta unahangaikia vipaumbele vya wengine na kusahau vya kwako vile muhimu. Bila kuwa na mbinu sahihi za kuweka kujitawala na zama hizi utajikuta kila siku unapata ufanisi hafifu kwenye kile unachofanya. Watu hawapumziki wala hawafanyi kazi. Muda wa kazi watu wanawaza kupumzika na muda …

Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Zaidi Kwa Watu

Rafiki yangu nikupendaye, Njia ya kujenga uaminifu zaidi kwa watu ni kwa njia ya kutimiza ahadi. Unapoahidi kitu, timiza kama ulivyoahidi na siyo kuja na visingizio. Kwa kila ahadi unayotimiza,unajenga uaminifu zaidi kwa watu. Siyo kujenga uaminifu, lakini pia kuaminika, kuheshimika kiasi cha kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wale unaohusiana nao. Timiza ahadi unazojiwekea …

Fanya Kilicho Sahihi

Rafiki Kwenye maisha ukitafuta umaarufu bila kutoa thamani utaupata kweli lakini utaupoteza muda siyo mrefu. Njia nzuri ya kupata umaarufu ni kutoa thamani kupitia kile ulichochagua kufanya. Unaweza ukashangaa wale ambao wanafanya vitu visivyo sahihi na kupata umaarufu wa ghafla kama vile tunavyoona kwenye mitandao ya kijamii yanayoendelea. Usije ukashawishika hata siku moja kufanya vitu …

Kwani Watu Wanasemaje?

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye haya maisha jitahidi sana usiwe mjinga. Kwa sababu watu wanaendesha maisha yao kwa sababu ya ujinga fulani ulikuwa nao. Sehemu yoyote ukienda, kama hakuna mtu wa KUTAPELIWA, basi wewe ndiyo utatapeliwa. Unapaswa kuwa makini sana. Ni aibu kwa mtu makini ambaye unapata maarifa mazuri na chanya halafu ukaendelea kuwa kama wengine. …

Jinsi Ya Kupata Fedha Za Kuwekeza

Rafiki, Kama unataka kwenda kununua kitu fulani huwa unajua kabisa bei yake ni kiasi fulani. Unapoenda kununua kitu hicho, hakikisha unaomba punguzo la bei. Dai punguzo la kitu chochote kile unachotaka kununua na ukipata hilo punguzo kile kiasi unachopata kwenye punguzo, nenda kakiwekeze. Kwa mfano, ulijiandaa kwenda kununua simu ya laki mbili na nusu na …

Haya Ndiyo Mambo yanayozalisha matokeo makubwa

Mwandishi Robin Sharma  anatukumbusha msingi mkuu wa ushujaa ambao amekuwa anafundisha kwa muda mrefu na kutaka kila mtu aukariri; hatua ndogo ndogo zinazochukuliwa kwa msimamo kila siku bila kuachwa ndiyo zinazozalisha matokeo makubwa sana. Kumbe basi, mambo yanayozalisha matokeo makubwa ni yale mambo madogo madogo ambayo tunayadharau. Unataka kupata mafanikio makubwa, ila jua hayatakuja mara …

Kufika Muda Kamili Ni Kuchelewa

Kama umepanga kwenda sehemu yoyote ile, kufika muda kamili ni kuchelewa. Ili uweze kujenga ushawishi kwa watu na kuaminika, jitahidi kufika sehemu kabla ya muda mliopanga. Fika nusu saa kabla au dakika 15 kabla ya kukutana na mtu.Utamaduni wa watu wengi kwa hapa Tanzania ni kuchelewa kufika sehemu husika kwa muda uliopangwa. Wewe usiwe hivyo. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started