Rafiki, Vitu vyote unavyofanya kwenye maisha yako, ni zao la tabia. Mambo mengi unayofanya kila siku ni kwa sababu ya tabia. Watu huwa wanafanya vitu walivyozoea kila siku na siyo nje ya hapo.Huwa tunatengeneza tabia, kisha tabia zinatutengeneza. Chochote kile ambacho unataka kiwe sehemu ya maisha yako, jenga tabia tu. Hakuna kinachoshindikana mbele ya tabia. …
Kama Mambo Hayawezekani
Rafiki, Kama hayawezekani basi fanya kile kinachowezekana. Hata mambo yawe magumu kiasi gani, kuna mahali pa kuanzia. Anzia hapo ulipo, fanya kile kinachowezekana na baada ya muda utajikuta unafanya kisichowezekana. Angalia kila changamoto kama fursa kwako kufanya kile kinachowezekana.Kwenye maisha, ugumu unakuwepo pale unapokuwa hujaanza. Kuanza huwa kunatoa njia.Kuanza ni ufunguo wa kuondoa laana ya …
Jiandae
Rafiki, Kila anayeamka asubuhi hajui nini kitakwenda kutokea kwenye siku yake. Tunakuwa na mipango yetu mizuri tunapoamka, lakini dunia nayo inakuwa na mipango yake pia. Jiandae kwa mipango yako lakini jua kabisa dunia nayo ina mipango yake. Usije ukapata kisirani pale dunia inapoingilia mipango yako. Jua asili ndivyo ilivyo. Kuna wakati mambo yanaenda tofauti na …
Njaa Inayowasumbua Watu Wengi Zama Hizi
Rafiki, Kama unataka ukubalike na kujenga ushawishi kwa watu unaohusiana nao basi jenga tabia moja, ambayo ni jenga tabia ya kusifia yale mazuri unayoyaona kwa mtu. Wasifie watu, kwa sababu watu wanapenda kusifiwa na ndiyo njaa yao kuu. Unapowasifia watu, watu wanajisikia vizuri na hata kukubaliana na wewe kirahisi kwenye kile unachopendekeza. Watu huwa wanafanya …
Jinsi Ya Kuwa Bora Kwenye Zama Za Mambo Mengi
Rafiki, Muda tulionao ni mchache sana ukilinganisha na mambo ya kufanya. Lakini, Seneca aliwahi kunukuliwa akisema, tuna muda mwingi mpaka tunautumia katika mambo yasiyo kuwa na maana. Hii ina maana kwamba, mtu hawezi kusema hana muda kufanya jambo lenye maana kwake wakati anao muda wa kufanya mambo yasiyo na maana kwake. Katika zama hizi za …
Continue reading "Jinsi Ya Kuwa Bora Kwenye Zama Za Mambo Mengi"
Hujazaliwa Kwa Ajili Yako
Rafiki, Hujazaliwa peke yako, bali umezaliwa kwa ajili ya wengine.Kama uko hai, ni kwa sababu unatakiwa kuwasaidia wengine.Kuna watu wanakuhitaji wewe, ili wao waendelee kuishi. Maisha ni ushirikiano. Watu wanategemeana, peke yako huwezi. Bado unahitaji wengine ili kufanikiwa. Timu ya mpira wa miguu nchini Uingereza Liverpool FC, wana kauli mbiu yao inayosema, you can't walk …
Kama Hupati Matokeo
Rafiki, Siku zote njia sahihi lazima ilete majibu sahihi. Kama unaona hupati matokeo basi kuna kitu hiki;Njia unayotumia siyo sahihi auUnafanya kwa namna ambayo siyo sahihi. Ili upate matokeo mazuri kwenye kile unachofanya, hakikisha njia unayotumia ni sahihi. Wote tulisoma katika hisabati kwamba, njia sahihi lazima ilete jibu sahihi.Kama unatumia njia sahihi kufanya hesabu na …
Jinsi Ya Kufika Pale Unapotaka Kufika
Rafiki, Ukiwa unatoka nyumbani na unataka kwenda kazini huwezi kukaa chini na kufikiria kwamba utafikaje kazini.Ni kitendo tu cha kutoka na kuanza mchakato wa kwenda kazini. Huenda unajiuliza, je, utafikaje kule unakotaka kufika? Jibu ni anzia hapo ulipo sasa. Hakuna mtu ambaye hana mahali pa kuanzia. Kwa sababu unapumua, kitendo tu cha kupumua ni mahali …
Hakuna Kushindwa Bali Kuna Hiki Hapa
Kwenye maisha chochote kile unachofanya na matokeo yoyote yale utakayoyapata ni ushindi kwako. Kwa nini ni ushindi kwa sababu umepata mahali pakuanzia na kuboresha kitu.Matokeo yoyote yale utakayoyapata, utayatumia kuboresha kule unakotaka kwenda. Kama huna matokeo yoyote yale utakosa pa kuanzia.Ni bora ufanye na matokeo yoyote yale utakayoyapata, utayatumia kuboresha zaidi kule unakotaka kwenda. Mafanikio …
Mtu Anayekupenda
Mtu anayekupenda kweli kutoka moyoni, hawezi kukuangusha hata siku moja.Atajitoa kwako kwa hali na mali. Upendo wa kweli hauna kipimo. Mtu anayekupenda anakuwa hana kipimo ndani yako.Mtakatifu Agustino wa Hippo aliwahi kunukuliwa akisema, kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Mtu anayekupenda atakupenda bila kipimo. Ukiona mtu anakupenda kwa masharti, jua hapo hakuna kipimo. Tujifunze …