Hata Kama Hujisikii Kufanya

Kuna siku unaamka ukiwa na hamasa ya kufanya kile ulichopanga kufanya. Kuna siku unaamka wala hujisikii kufanya kazi na huna hamasa. Ni kawaida kabisa kwa binadamu kupitia hali kama hiyo. Huwezi kuwa vizuri kila siku. Hamasa huwa hazidumu. Wewe kama mtu makini, hautakiwi kuripoti sababu, bali kuripoti matokeo mazuri. Hata kama hujisikii kufanya, wewe fanya …

Bado Hujashindwa

Mara nyingi watu wanaposhindwa kufanya kitu, huwa wanajiona wao ndiyo wameshindwa. Wanaanza hata kujichukia wao wenyewe.Lakini hilo siyo kweli. Kushindwa kwako ni tukio na siyo wewe. Kushindwa mara nyingi ni tukio na siyo mtu. Unapofanya kitu na hakijaenda au hujapata matokeo unayotaka, wala usijione kama wewe ndiyo umeshindwa bali ni tukio ndiyo limeshindwa. Wewe hujashindwa …

Uvumilivu Ukiwa Kwenye Mchakato

Waswahili wanasema, mvumilivu hula mbivu. Au subira ya vuta heri. Haya yote ni sawa, na uvumilivu ni mzuri ukikukuta ukiwa kwenye Mchakato. Uvumilivu unakuja na matokeo fulani. Kama unakitu unafanya basi ni vema ukaendelea kwa sababu unajua mwisho wa siku utavuna. Huwezi kuvuna kama hujapanda. Uvumilivu unalipa pale ukiwa na kitu cha kufanya. Hakikisha unavumilia …

Fuatilia, Usilalamike

Watu wengi pale wanapoona wamepata changamoto ambayo imesababishwa na watu wenye mamlaka ya kitu fulani, huishia tu kulalamika. Usiishie tu kulalamika, bali fuatilia.Matatizo mengi yanashindwa kutatuliwa katika jamii zetu kwa sababu ya watu kushindwa kufuatilia kwa watu mwenye mamlaka husika wa kutatua shida zao. Badala yake wanaishia kulalamika kwa watu wasiokuwa na mamlaka na matokeo …

Usikubali Kushindwa Kirahisi

Kukubali kushindwa kirahisi, siyo sifa nzuri. Sifa nzuri ni kuwa king'ang'anizi na kutokubali kushindwa kirahisi. Unapambana mpaka unapata matokeo unayoyataka.Hata pale unapoona umefikia mwisho, usikubali kukiri udhaifu, pambana kupata matokeo. Hujatumwa kutoa mrejesho wa visingizio, bali matokeo. Matokeo mazuri huwa yanakuja na maandalizi mazuri yenye ufanisi. Kama unataka kupata matokeo mazuri, jiandae na maandalizi mazuri. …

Kama Siyo Muhimu Usiongee

Kwenye maisha usiwe muongeaji sana. Ongea yale ambayo ni muhimu tu. Unapoongea sana, utajikuta unaongea yale yasiyokuwa na maana.Kama watu walikuwa wanakuheshimu, wanaweza kukushusha kwa yale unayoongea. Hata mpumbavu akikaa kimya, huwa anaonekana mwenye hekima. Ongea kama ni muhimu tu na kama siyo muhimu usiongee. Changia pale unapoona usipochangia mambo yataenda kuwa vibaya. Mara zote …

Usiogope Kushindwa

Kama bado hujapata kile unachotaka, endelea kuweka kazi. Usiishie njiani, atafutaye hachoki na akichoka ameshapata. Je, wewe unataka kuchoka umeshapata?Pambana ufanikiwe na mafanikio yako yatafuta kabisa kushindwa kwako ambako umepitia. Ni kupitia kushindwa ndiyo utafanikiwa na ukishafanikiwa hakuna atakayekumbuka yale uliyoshindwa. Hatua ya kuchukua leo; Nenda kawaoneshe wale wote ambao wanakuambia umeshindwa kwa kufanikiwa zaidi. …

Vitu Viwili Vya Kuzingatia Kwenye Mauzo

Biashara nyingi zinakabiliwa na changamoto ya MAUZO. Na matatizo yote kwenye biashara yanatatuliwa na kitu kimoja tu nacho ni mauzo. Mauzo ndiyo suluhisho la matatizo yote kwenye biashara. Kama unataka kipato zaidi, ongeza mauzo zaidi. Kama unataka watu wazuri, ongeza mauzo na utawapata watu wazuri kwa kuwaajiri. Ili kuongeza mauzo hakikisha unapata wateja wapya kila …

Mtu Anayependa Wengine Wafanikiwe

Mtu aliyefanikiwa, huwa anapenda wengine wafanikiwe. Ni mtu asiyefanikiwa, ndiyo huwa hapendi kuona wengine wakipiga hatua. Mtu aliyefanikiwa kwa njia sahihi, huwa anapenda kuwawezesha wengine kupiga hatua.Huwa wanapenda kuwaelimisha wengine mbinu za kufanikiwa zaidi. Wakati mwingine huwa wanajitoa kwa ajili ya wengine pasipo hata kulipwa ili watimize lengo lao la kuona watu wanafanikiwa. Kuwa mtu …

Jinsi Ya Kuiona Hela Kwenye Maisha Yako

Kwenye kitabu cha Mhubiri 10 mstari wa 19 anasema, fedha ni jawabu la mambo yote. Hilo halina mjadala. Kinachofanya fedha iishe,ni matumizi. Na hatuwezi kuzuia matumizi kwa sababu tunafanya kazi ili kazi itusaidie. Fedha inatusaidia kulipa bili mbalimbali.Ili uweze kuiona hela fanya yafuatayo.Kwanza dhibiti matumizi, kumbuka kinachomaliza fedha zako ni matumizi. Na hapa nazungumzia matumizi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started