Maana Halisi Ya Thamani

Rafiki yangu nikupendaye, Huwa tunasema sana au umeshasikia watu wakisema kwamba ili ufanikiwe unapaswa kutoa thamani. Swali la kujiuliza je, unajua nini kuhusu thamani? Unasikia ukiambiwa kwamba, toa thamani kwa mteja.Ni kweli, kwenye biashara, kazi au huduma, unapaswa kutoa thamani kwanza ndipo uweze kupokea. Watu kwa asili ni wabinafsi, hivyo usipokuwa mtu wa kujali maslahi …

Vitu Viwili Vinavyokuzia Kupata Unachotaka

Rafiki yangu nikupendaye, Kwa haya yote unayojifunza, kwamba unaweza kupata chochote unachotaka, mawazo yako yanavuta chochote unachofikiria, unaweza kuhisi ni uongo kwa sababu labda wewe umejaribu lakini hujapata ulichokuwa unataka. Kama hivi ndivyo unavyofikiria, basi kuna vitu viwili vinakuzuia usipate kile unachotaka; Moja; hujakomaa na kitu hicho kwa muda mrefu kiasi cha kuweza kupata unachotaka, …

Laiti Ungelijua Hili

Rafiki yangu nikupendaye, Kila mmoja wetu kuna hali ya majuto fulani anayo ndani yake.Majuto haya tukiyafikiria, yanatufanya tuumie zaidi. Majuto haya yamekuja kwa sababu mbalimbali, labda pengine ulipaswa kuchukua hatua fulani na hukufanya hivyo.Labda ulipaswa usichukue hatua fulani na hukufanya hivyo. Kuna wakati tunawaahidi watu ambao tunahusiana nao kwamba tutawasaidia katika hitaji walilotuomba, na tuna …

Rudi Kwenye Mstari

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha kuanguka siyo dhambi. Bali dhambi ni kubaki kwenye anguko.Ukishajikuta umeanguka kwenye kitu fulani, usione aibu kutoka, kwa sababu ujinga ni kuendelea kubaki. Sehemu yoyote ambayo umejikuta umeanguka, wahi haraka kurudi kwenye mstari. Kila mmoja wetu ana utashi wa kujua mema na mabaya.Kuna wakati unaweza kwenda ndivyo sivyo, hivyo unapojikuta katika …

Tatizo Ni Mawazo Yako

Rafiki yangu nikupendaye, Tatizo siyo dunia wala tatizo siyo watu, tatizo ni mawazo watu waliyokubali. Pamoja na siri za mafanikio kuwa wazi kwa kila mtu, bado watu wengi hawafanikiwi. Ni rahisi kuona labda kutakuwa na tatizo na watu au dunia itakuwa na matatizo. Lakini ukweli ni kwamba, watu siyo wabaya, wala dunia siyo mbaya. Tatizo …

Biashara Inayolipa Zama Hizi

Rafiki, Ukiangalia maisha ya watu wengi kwa nje utaweza kusema kwamba wametulia. Lakini, maisha ya watu wengi kwa ndani hawajatulia. Ukifanikiwa kutulia kwenye maisha yako, utaona raha ya maisha.Kama hujatulia kiroho, kimwili na kiakili, unaweza ukajikinai hata wewe mwenyewe na kuona hakuna maana ya maisha. Kwa kuwa watu wengi hawajatulia kwenye maisha yao, hawajutulia kwenye …

Wakikupa Fedha, Watakupangia Cha Kufanya

Rafiki yangu nikupendaye, Hakuna njia ya hovyo kama ya kuingiza kipato bila kutoa thamani.Kinachoingia kirahisi, kitaondoka kirahisi. Pata hela kwa njia ya kutoa thamani na siyo vinginevyo.Msingi mkuu wa kupata fedha, ni kutoa thamani.Kipato au fedha ni zao la thamani.Kumbe basi, unalipwa kulingana na thamani unayotoa.Thamani yako ndiyo inaamua wewe ulipwe kiasi gani lakini hata …

Kitumie Kujituma Zaidi

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha kila mtu huwa ana ndoto zake. Na kuwa na ndoto ni kitu kizuri, kwa sababu bila ndoto unakuwa huna kitu kinachokusukuma. Mpaka hapo ulipo utakua na ndoto kubwa kwenye maisha yako si ndiyo?Sasa basi, tumia msukumo wa ndoto uliyonayo ili uweze kufanikiwa kwenye kile unachotaka. Yaani kile unachotaka, kikufanye uamke …

Itume Dunia Ikuletee

Rafiki yangu nikupendaye, Dunia tayari ina kila kitu, ni wewe kuituma na kuielekeza. Dunia imekamilika kwa kuwa na kila ambacho kinahitajika kwa maisha ya mafanikio. Kinachotakiwa ili mtu kupata kile anachotaka ni kuiambia dunia anataka nini kupitia mawazo yake, kisha kuweka juhudi katika kupata kile anachotaka. Ni wewe uchague kupokea kile unachotaka kwa kuielekeza dunia …

Kama Hujajipata Fanya Haya Hapa

Rafiki, Watu wengi ambao hawajajipata kwenye maisha huwa wanatabia ya kutaka kuishi kama wale ambao wamejipata. Ambaye amejipata, anaishi vile anavyotaka. Changamoto ya watu ambao hawajajipata, wanaiga maisha ya watu ambao tayari wamejipata. Hii inapelekea wengi kurudi nyuma, badala ya kwenda mbele. Kama hujajipata, usiigize maisha, ishi uhalisia wako. Maisha ya kuigiza kama umejipata kumbe …

Design a site like this with WordPress.com
Get started