Huyu Pekee Yake Anatosha

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha kuna kupata na kukosa. Huwa kuna wakati tunatamani mambo yetu yaende kama vile tulivyopanga lakini dunia haiko hivyo. Unakuwa na mawazo mazuri ya kitu fulani, unaamua kuwashirikisha watu na wanakuambia ufanye watakuunga mkono. Lakini, wale ambao walikuaambia watakuunga mkono unashangaa wanaenda kinyume na wewe. Pale unapoona hakuna mtu anayekuunga mkono, …

Jinsi Ya Kupunguza Makosa Mwaka 2025

Rafiki yangu nikupendaye, Ufanye mwaka huu uwe bora kwako kwa kutofanya makosa yale yale uliyofanya mwaka jana.Kwa sababu, ujinga ni kufanya mambo yale yale kwa mtindo ule ule huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Ili upate matokeo ya tofauti, unapaswa kufanya kitu cha tofauti kabisa kwenye maisha yako. Na siyo kurudia yale yale uliyokuwa unayafanya …

Wale Ambao Hawakuamini Wafanyie Kitu Hiki

Rafiki yangu nikupendaye, Kila mmoja wetu huwa kitu fulani anafanya. Huenda katika eneo ulilopo, watu wanakuamini kwa kile unachofanya au hawakuamini kwa sababu ya uzoefu wako. Huenda una uwezo mzuri sana ndani yako, lakini wale watu ambao wanataka huduma yako, wanashindwa kukuamini kwa sababu ya uzoefu wako. Wafanyabiashara wanapoanza kazi wanapitia changamoto ya kutokuaminika. Wanunuaji …

Kama Bado Unaishi

Waswahili wanasema, usimtukane mamba kabla hujavuka mto. Usicheke matatizo ya wengine kama bado uko hai. Kwa sababu kile ambacho kimetokea kwa wengine, kinaweza kukutokea hata wewe. Hakuna ambaye yuko salama kwenye haya maisha.Mara zote ishi kwa tahadhari ili kukabiliana na kila hali. Kama bado unaishi, wasaidie wale ambao wanapitia changamoto fulani kwenye maisha yao. Mwimbaji …

Ukiwa Mstaarabu Kwenye Maisha Hutoboi

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha ukiwa mstaarabu sana hutoboi kwa sababu ustaarabu utakuzuia kufanya vitu vingi na hata kuona aibu fulani. Kwa mfano, wewe kama muuzaji, utajiona mstaarabu kumwambia mteja anunue kile unachouza. Una mdai mtu, unaogopa kumwambia akulipe, hivyo unakuwa mstaarabu na kukaa kimya. Kuna watu ambao wanapaswa wakamilishe kitu fulani ili uweze kukamilisha …

Kabla Hujaenda Kasi Hakikisha Hiki Kwanza

Rafiki yangu nikupendaye, Kila mtu anapenda kwenda mbele. Ni lengo la kila mmoja wetu. Hakuna mtu anayeamka na kusema leo ninataka kurudi nyuma. Kwenye maisha yako, kama unataka kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma ni kwa kujifanyia tathmini. Ukitaka kujua unaenda mbele, ni pale unapokuwa haurudi nyuma. Kabla hujafanya maamuzi ya kwenda kasi, kwanza …

Kuwa Mtu Wa Namna Hii Mwaka 2025

Rafiki yangu nikupendaye, Mungu aliumba dunia na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana kwa kutamka.Vivyo hivyo, mwaka huu mpya unaoanza leo, ukawe mwaka wa kujitamkia matashi mema. Jitamkie heri haijalishi Utakutana na magumu gani mbeleni, lakini jitamkie mazuri, hakuna njia isiyokuwa na kona. Kazi yako kubwa ni kubariki watu katika siku hii ya leo.Anza kujibariki wewe …

Hukosi Kitu Cha Kushukuru

Rafiki yangu nikupendaye, Kama uko hai mpaka siku ya leo, ni zawadi nzuri ya kushukuru Mungu. Kama hata mipango yako haijaenda vile ulivyokuwa unataka, lakini hukosi Kitu cha kushukuru. Leo unapoumaliza mwaka 2024, fanya zoezi la kuandika mambo ya kushukuru kwenye maisha yako ndani ya mwaka huu. Mwaka 2024, umekuwa mwaka wa namna gani kwako.Yapi …

Kama Huna Hichi Kitu Usiongee Kabisa

Rafiki yangu nikupendaye, Mmoja wa mwanafalsa wa Ustoa anatushauri kwamba, kama watu wanakusema juu ya kitu fulani, kama ni kweli badilika. Na kama siyo kweli endelea na maisha yako. Naye baba wa falsafa Plato aliwahi kunukuliwa akisemaWerevu huongea kwa sababu wana kitu cha kuongea, ila wapumbavu huongea kwa sababu inabidi waseme kitu. Wakati wowote unapotaka …

Kama Siyo Sahihi Usifanye

Rafiki yangu nikupendaye, Njia nzuri kuishi falsafa au asili ni kuishi katika msingi ambao ninakwenda kukupendekezea hapa. Msingi huo ni, kama kitu siyo sahihi usifanye. Na kama kitu siyo kweli usiseme. Pale tu unapofanya kitu, jiulize tu je, hiki ninachofanya ni sahihi? Kama ni sahihi fanya na kama siyo sahihi usifanye. Kila mmoja wetu amepewa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started