Hakuna watu wanaotujua vizuri zaidi ya sisi wenyewe. Tumekuwa ni viumbe wa kutafuta sababu, kujipiga "saundi" sisi wenyewe pale tu tunapotaka kuahirisha mambo. Kwa mtu ambaye uko hai na mwili wako uko kwenye mwendo kusema huna cha kufanya ni dhambi na ni uvivu mbaya sana.Mtu makini na mwenye thamani atakosaje cha kufanya? Kama huna cha …
Hii Ndiyo Bidhaa Yenye Soko
Karne ya 21 imepoteza bidhaa moja muhimu sana. licha ya watu kufanya kazi, biashara lakini ndani yao hawana, hawauzi bidhaa yenye soko na inayofanya vizuri sokoni. Watu wanapewa kazi lakini wanashindwa kuuza ile bidhaa ambayo inatakiwa na dunia. Tumekuwa tunauza vile tunavyojua sisi ndiyo maana dunia huwa inatupa kile tusichotaka kwa sababu ya kushindwa kuuza …
Hii Ndiyo Kazi Kubwa Ya Wanafalsafa
Sisi binadamu tumekuwa tuna udhaifu sana katika kufanya maamuzi. Tumekuwa tunaongozwa zaidi na hisia kuliko kufikiri kwa akili. Tafiti zinaonesha kuwa hata maamuzi mengi yanayofanywa kila siku watu wanayafanya kwa kutumia hisia na mara nyingi maamuzi ya hisia tunayofanya yanakuja na gharama kubwa baadaye. Huwa tunawaamini sana wataalamu tunapotaka kufanya maamuzi tena eneo ambalo sisi …
Kitu Kinachopatikana Kwa Urahisi
Kama kuna kitu huwa unakipata kiurahisi basi jua thamani yake ni ndogo. Kitu chochote kinachopatikana kwa urahisi thamani yake ni ndogo. Ila kinachopatikana kwa shida thamani yake ni kubwa. Kwa mfano, sukari kwa sasa imekuwa adimu hivyo inapelekea kuwa na thamani kubwa. Ukilinganisha chumvi na sukari utaona kuwa chumvi inapatikana kwa urahisi na wala hujawahi …
Njia Ya Kupata Vitu Vyote Vizuri Duniani
Hivi unaweza kaa chini na kuweka mipango ya kupata vitu vibaya? Vitu vibaya vinakuja vyenyewe pasipo kutafutwa kwa sababu yule anaye tafuta vitu vizuri anavipata lakini yule ambaye hatafuti vizuri havipati kweli anaishia kupata vibaya. Kila kiumbe kinapambana kutafuta kitu kizuri, kwa sababu kitu kizuri kinakuwa kinampa mtu kile ambacho moyo wake unataka. Vitu vizuri …
Hiki Ndicho Kinachogundua Ukweli
Hakuna hata mmoja wetu anayeweza kuhodhi ukweli, yaani kuumiliki na kusema ni wake hivyo aufiche. Ukweli haufichiki, ukweli uko kama moshi, unapika ndani moshi unatoka nje. Tunaweza kuuficha kwa muda tu lakini yuko bwana mmoja anayefichua na kugundua ukweli wote tunaoficha.Anayeweza kuufichua ukweli wa mambo au jambo lolote lile ni muda. Muda unaponya kila kitu …
Uchambuzi Wa Kitabu; UMEIWEKA WAPI TALANTA YAKO? Je umejiajiri, umeajiriwa au huna ajira?
Kitabu hiki kimeandikwa na Albert Nyaluke Sanga na kuchambuliwa na mwandishi Mwl. Deogratius Kessy Mwandishi anaanza na kusema ;πAjira zinafanana na kuweka fedha benki. Unapochukua talanta zako yaani fedha na kwenda kuziweka benki kwa muda maalumu , tafsiri yake ni kwamba unasema, jamani eeh, mwenzenu nina talanta (fedha) hapa lakini sielewi nitazifanyia nini kwa muda …
Kama Maisha Ya Chini Yamekuchosha Amua Kufanya Hiki Leo
Kama maisha ya chini yamekushinda fanya maamuzi ya kwenda juu. Maisha ya juu ni mazuri, hayana foleni unafanya kile unachotaka lakini maisha ya chini hayakupi kile unachotaka siku zote. Utatoka hapo ulipo kwenda juu endapo utafanya maamuzi ya kwenda juu na kuyachukia maisha ya chini. Siku zote kila kitu kinaanzia chini, ni kaburi tu linaanzia …
Continue reading "Kama Maisha Ya Chini Yamekuchosha Amua Kufanya Hiki Leo"
Jionee Hasara Ya Mtu Ambaye Alikataa Kusamehe
Kama uko hai basi msamaha unakuhusu na huwezi kuukwepa. Watu wako bize kufanya kazi lakini kuna vitu vidogo kama kuishi na vinyongo na kutosamehe vinawatesa kiasi kwamba hawafurahii maisha yao. Msamaha ni kuondoa uchungu uliombika ndani ya moyo. Msamaha ni kuondoa uchafu au sumu ndani ya mwili, kwa mfano vipi kama unakula kila siku halafu …
Continue reading "Jionee Hasara Ya Mtu Ambaye Alikataa Kusamehe"
Fedha Hazibadilishi Tabia Za Wanandoa Bali Zinafanya Hiki
Huwa tunatengeneza tabia na kisha tabia zinatutengenezea sisi. Hakuna mtu aliyezaliwa na tabia ambayo anayo sasa ila tabia zote tumejifunza taratibu mpaka leo hii zimetushikilia tunashindwa kuziondoa. Kila mmoja anatabia yake na ndiyo maana wanandoa wakikutana kila mtu anajaribu kumshepu mwenzake katika tabia anayoina yeye ni sahihi. Tabia nzuri ni ile ambayo haiendi kinyume na …
Continue reading "Fedha Hazibadilishi Tabia Za Wanandoa Bali Zinafanya Hiki"