Siku Huwa Hazifanani

Kila siku huwa inakuja na mambo yake. Matokeo uliyopata jana huenda leo usiyapate. Hakuna anayeweza kutabiri kesho itakuwaje bali wote huwa tunaishi kwa matumaini tu. Mbinu uliyotumia jana huenda leo isikupe matokeo kama yale ya jana. Hivyo usiishi kwa mazoea. Kwa sababu siku hazigandi zinasogea kila siku. Kila siku unayoipata kwako iwe ni siku ya …

Kitu Cha Kuepuka Kufanya Pale Unapokutana Na Changamoto

Kila mmoja wetu ni rahisi kutoa ushauri kwa wengine pale wanapokutana na changamoto. Lakini ushauri huo huo anaotoa kwa wengine anashindwa kuutumia yeye mwenyewe akiwa na changamoto. Kitu cha kuepuka pale unapokutana na changamoto ni kwamba, usitaharuki. Unapotaharuki unakuwa unajivuruga wewe mwenyewe. Ukitaharuki siyo kwamba utajivuruga wewe mwenyewe, bali pia utawavuruga na wengine pia. Ukikutana …

Hii Ndiyo Njia Bora Ya Kumsaidia Mtu Anayehitaji Msaada Wako

Mpaka mtu amekuja kwako na kukuomba msaada kuwa umsaidie kitu fulani, ujue hana au hajui. Kitu unachokosea ni pale mtu anapokuja kwako na kukuomba umsaidie kitu fulani hajui na wewe unamkosoa na kumwambia yaani hata hiki hujui? Sasa kama mtu angekuwa anajua angeuliza ya nini? Mtu anauliza kwa sababu hajui na anahitaji msaada hivyo mtu …

Malengo Yako Yaendane Na Kitu Hiki

Angalia ukubwa wa malengo yako, na hatua unazoweka je zinaendana? Malengo yako yanatakiwa yaendane na hatua unazochukua. Kama wewe malengo yako ni makubwa unatakiwa uende hatua ya juu zaidi. Itakubidi upunguze vitu ambavyo havina maana kwako, jitoe kafara kwenye yale maeneo unayotaka tu. Kubali kupoteza visivyokuwa muhimu ili upate vile vya muhimu. Kadiri unavyotaka kufika …

Sababu Huwa Hazilipi Bili

Kama wewe ni bingwa wa kulalamika kwenye maisha yako kwa sababu zozote zile nikupe pole. Ukilalamika gharama za maisha zimepanda unafikiri maisha ndiyo yatakuonea huruma? Hata ulalamikeje, sababu huwa hazilipi bili. Huna umeme nyumbani ,ukipeleka sababu kwenye luku umeme utawaka?Vipi simu yako ikiishiwa salio utaweka sababu ili uweze kuitumia kwa mawasiliano? Watoto wanadaiwa ada shuleni, …

Jinsi Ya Kuifanya Dunia Kuwa Safi

Tukitaka dunia iwe na mabadiliko makubwa, basi kila mmoja wetu akazane kufanya kazi yake. Kila mmoja atimize wajibu wake uliomleta hapa duniani. Kila mmoja apambane na ndoto yake, na tutaona maendeleo katika hii dunia. Kuwa ni kufanya, hivyo kuwa vile unavyotaka kuwa. Na dunia itakua safi sana. Mama Theresa enzi za uhai wake aliwahi kusema, …

Kama Hii Siyo Kazi Yako Usiifanye

Siyo kila kazi inaweza kuwa kazi yako. Kila mtu huwa ana kazi yake. Hivyo basi, kama kazi unayofanya ni yako basi fanya kazi yako na kama siyo kazi yako usifanye. Kuna kazi ambayo watu wengi huwa wanajihusisha nayo ambapo wala siyo kazi yao na kazi hiyo ni ya kukopesha. Kama kukopesha siyo kazi yako usijihusishe …

Kitu Cha Kufanya Pale Unapojikuta Akili Imechoka

Mchezo mzima wa maisha yetu uko kwenye akili. Tukiweza kucheza vizuri sana na akili zetu basi tutakua vizuri sana. Kila mtu anachoka pale anapofanya kazi. Akili inakuwa inachoka kufikiri unajihisi uko kwenye mkwamo. Pale unapojikuta akili imechoka, tafuta kitu cha sukari na kitumie. Unaudanganya ubongo wako kwa kuupa kitu cha sukari na baada ya kutumia …

Kuwa Tayari Kupoteza Hiki Hapa Ili Upate Kile Unachotaka

Ni sheria ya asili kuwa, hatuwezi kupata bila kupoteza. Kwa mfano, kama unataka kuvuna mahindi mengi shambani lazima ukubali kufukia chini mbegu ili upate mahindi mengi. Kwenye kila unachotaka kwenye maisha yako, kuna gharama unayopaswa kuilipa.Iwe kwenye kazi, biashara, familia, ndoa, kipaji n.k. Kuwa tayari kupoteza kile ambacho unacho ili uweze kupata kile ambacho huna. …

Jinsi Ya Kuteka Mioyo Ya Watu

Ni kuwa bora kuliko wao.Fanya kile ambacho wao hawawezi kufanya. Wala hawategemi hata wewe kama ungeweza kufanya. Unapoteka mioyo ya watu wanakuwa wanakuheshimu sana. Wanakuona wewe siyo mtu wa kawaida, na huenda wakakuogopa kwa mambo unayofanya. Kama kuna mtu anakusimamia kazi, fanya kwa ubora kuliko anavyotegemea. Kama kuna mtu unamfanyia kazi ifanye kwa ubora zaidi, …

Design a site like this with WordPress.com
Get started