Jenga Utaratibu Huu Kwenye Maisha Yako

Bado watu wengi hawajijengea utaratibu wa utoaji. Utoaji umekuwa ni changamoto miongoni mwa watu wengi. Utoaji mzuri ni ule ambao mtu anatoa bila kusukumwa na mtu. Hakuna mtu ambaye ni masikini wa kutupwa hana kitu cha kutoa. Hakuna mtu ambaye ni tajiri sana ambaye hana kitu cha kupokea. Jenga utaratibu wa utoaji. Jenga utaratibu wa …

Acha Tabia Hii Mara Moja

Kutoka katika kitabu cha matatizo si matatizo kilichoandikwa na Fr Dr Faustine Kamugisha mwandishi anasema hivi, wakati unateseka uepuke kudhania vibaya wengine. Kwa nini ?Kwa sababu unaowadhania vibaya wapo wanakutetea na kukulinda. Hii imetokana na hadithi ya mama mmoja ambaye alikuwa na mmoja wake mzuri ambaye alikuwa anamtumia kama msaidizi wa kukaa na mwanae. Mbwa …

Ifahamu Siasa Ya Zama Hizi

Ukikutana na watu siku hizi kila mtu utakutana ana matatizo ya kulalamika. Watu wengine wanapokuwa wanapitia magumu wanajikuta wanawachukia wengine na hata kuwadhania vibaya juu ya mapito wanayopitia. Kulalamika ndiyo imekuwa habari ya mjini. Kila mtu ana lalamika na bahati nzuri ni kwamba kila mtu kwa sasa amepewa uwanja wa kulalamika. Mitandao ya kijamii imekuwa …

Kwa Sababu Siyo Muhimu Kwako

Vitu vingi au mambo mengi unayoahirisha kufanya ni kwa sababu siyo muhimu kwako. Hakuna mtu ambaye ni makini anaweza kuthubutu kuahirisha kitu ambacho ni muhimu kwake. Anajua akiahirisha hawezi kupata kile anachotaka. Kwa mfano, unaanzaje kuahirisha kwenda kazini? Ni ngumu kwa sababu unajua kupitia kazi unapata kile unachotaka. Vitu vingi ambavyo huwa unavipotezea vinakuwa siyo …

Usiyanyamazie Mambo Muhimu

Unapoona jambo haliko sawa na ni la muhimu basi, usilinyamazie. Yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako usiyanyamazie kabisa. Lakini kama kitu kipo nje ya uwezo wako wala usijisumbue nacho. Hapa ninataka upambane na yale tu yanayokuhusu na ambayo hayakuhusu waachie wale ambao yanawahusu. Usiyanyamazie mambo muhimu kwa sababu, maisha yetu yanaanza kufikia mwisho …

Vitu Vitatu Vinavyokukwamisha Kupata Kile Unachotaka

Sisi binadamu ni watu wazuri sana wa kutafuta sababu. Tukiona kitu hatuwezi kukosa maoni juu ya kile kitu. Ni rahisi kutafuta sababu kwanini asifanye kuliko kwa nini afanye. Moja ya vitu vinavyowasababisha watu kutokamilisha mambo yao mengi ni hivi hapa vifuatavyo; Moja ni uzembe. Watu wanashindwa kuzalisha matokeo mazuri siyo kwamba hawajui ni kwa sababu …

Haya Ndiyo Mambo Muhimu Ya Kufikiria Kama Unataka Kupata Fedha Zaidi

Ni nani ambaye hapendi kupata fedha zaidi?Hakuna, wote tunapenda kupata fedha zaidi kwani inatusaidia kuendesha maisha yetu ya kila siku hii ni pamoja na kulipa bili mbalimbali. Iko njia rahisi ya kuweza kuzivuta fedha na zikaja kwenye maisha yako. Fuata yafuatayo ile uweze kuvuta fedha na zije kwako. Moja, acha kufikiria yale usiyotaka kwenye upande …

Nitawezaje Kufanya?

Imani ina nguvu ya kukuwezesha wewe kuchukua hatua. Kuna mahali inafikia unajiuliza je, nitawezaje kufanya? Unawezaje kufanya? Ni pale tu wewe unapoweza kukiri imani yako unaweza na kujiaminisha kuwa unaweza bila wasiwasi. Kuamini inawezekana ni jambo zuri sana katika maisha yako. Nitawezaje kufanya inakusaidia kufikiria njia za kuweza kufanikiwa kile unachotaka kufanya. Lakini pale unaposema, …

Mbinu Itakayokusaidia Kuongeza Mauzo

Naomba nianze na kukuuliza swali, je, watu wanajua kile unachofanya? Kile unachouza? Huenda ukawa na bidhaa nzuri sana lakini kama wateja husika hawajui kuhusu wewe ni kazi bure. Wanasema biashara ni matangazo, ili watu waje kununua kwako na wasiende sehemu nyingine hakikisha unaweka kazi ya kutosha kuhakikisha watu wanajua kile unachofanya. Fanya masoko ya kutosha …

Hakuna Malipo Kwenye Hili

Leo nataka uondoke na kitu kimoja muhimu na uende ukafanyie kazi. Kwamba hakuna malipo kwenye wasiwasi. Kumbe basi, tunaweza kusema wasiwasi hauna malipo badala ya kuendelea kuwa na hofu na wasiwasi ishi maisha yako. Hofu na wasiwasi ndiyo unaua zaidi kuliko unavyofikiria. Wasiwasi haukusaidii kutatua tatizo. Bali chukua hatua sahihi juu ya kitu kinachokupa wasiwasi. …

Design a site like this with WordPress.com
Get started