Iko hivi rafiki yangu,Kama wewe hujali mambo yako basi jua kabisa hata wale wanaokuzunguka hawatajali sana mambo yako. Huwa watu wa nje wanapata picha kutoka ndani yetu kwanza, wakituona sisi ni watu wa namna fulani basi wanatuchukulia kwa namna ambavyo sisi tupo. Watu wakishakusoma watakuchukulia vile unavyotaka wewe.Wakiona wewe ni mtu unayejali mambo yako, kazi …
Category Archives: Uncategorized
Kama Wengine Wanakosea Hata Wewe Unakosea
Ni kawaida yetu sisi binadamu kujiona kuwa sisi ndiyo tuna stahili zaidi kuliko wengine. Tunapenda kujiona kuwa sisi hatuna makosa bali watu wengine ndiyo wenye makosa.Pale tunapokosea huwa tunamtafuta mtu wa kumlaumu kwanza. Huwa hatupendi kukubali kuonekana sisi ndiyo tunakosea bali wengine ndiyo wanakosea. Kama wengine wanakosea basi na wewe unakosea pia. Tunatakiwa kukubali makosa …
Continue reading “Kama Wengine Wanakosea Hata Wewe Unakosea”
Kinachowafanya watu Wengi Kutoingia Kwenye Biashara Ni Hiki Hapa
Hapo mwanzoni kulikuwa hakuna ajira bali biashara ndiyo ilikuwepo na itaendelea kuwepo kwa sababu asili ya binadamu ni biashara. Ili tuweze kuwa na kipato cha uhakika na kufikia uhuru wa kifedha tunapaswa kila mmoja wetu kuwa na biashara. Biashara ni njia ya kupata kipato bila kikomo. Hata kama umeajiriwa hakikisha unakuwa na biashara ya pembeni …
Continue reading “Kinachowafanya watu Wengi Kutoingia Kwenye Biashara Ni Hiki Hapa”
Pima Kile Unachozalisha
Maisha ambayo hayana thamani, ni maisha ambayo hayana maana kuishi. Alisema mwanafalsafa Socrates. Chochote kile ambacho unafanya, jaribu kukipima kwanza matokeo ya yale unayopata. Unaweza kujiona unalima na unapata faida kumbe huna unachopata, kaa chini pima je kile unachofanya kinakuletea faida? Iko wazi, kama huna faida unayopata kwenye kile unachofanya basi unapata hasara kwenye kile …
Usiupoteze Muda Huu Bure
Mara nyingi huwa tunapoteza muda pale tunapokuwa kwenye foleni, au tunaposubiria kitu fulani au tunapokuwa kwenye gari. Huu ni ule muda ambao umekufa hatuwezi kufanya kazi. Sasa kama wewe uko gari au foleni usikubali muda ukupitie hivi hivi, Bali tumia muda huo kujifunza kwa kusoma kitabu au kusikiliza vitabu vilivyosomwa. Popote pale unapotembea , tembea …
Jinsi Ya Kufanikiwa Kwenye Karne Ya 21
Msingi wa mafanikio uko wazi kadiri ya aliyekuwa mwandishi na mwanafalsafa Zig Ziglar ambaye anasema wasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utafanikiwa kupata kile unachotaka. Katika karne hii ya 21 hakuna muujiza mwingine, naye bilionea wa kichina Jack Ma anaongezea na kusema Kama unataka kufanikiwa kwenye karne ya 21 unatakiwa kuwawezeshe wengine, hakikisha kuwa …
Usalama Wa Mahusiano Yako Ya Ndoa Uko Hapa
Hakuna maisha mafupi hapa duniani kama maisha ya ndoa kwani wote mnakutana mkiwa tayari ni watu wazima. Kama mtatumia maisha ya ndoa yenu kulaumiana na kila mwanandoa kuangalia mabaya ya mwenzake mtakuwa mnavumilia kuishi maisha ya ndoa na siyo kufurahia. Wanandoa ndiyo waamuzi wa mwisho katika mahusiano yao, wao ndiyo wanaamua ni aina gani ya …
Continue reading “Usalama Wa Mahusiano Yako Ya Ndoa Uko Hapa”
Furahia Kile Ambacho Tayari Unacho
Kama umepata nafasi ya kucheka, basi cheka.Furahia kufanya kile ambacho unayo nafasi ya kufanya kwa muda huo. Ukipata nafasi yoyote ile wewe ifurahie kutumia vizuri. Kwa kitendo cha kuifurahia utaweza kuacha alama na kufanya makubwa. Kila kitu kinakuja kwa sababu yake na kikiondoka hakiwezi kurudi tena. Ukifanikiwa kuiona siku mpya basi hakikisha unaiishi vizuri kiasi …
Jilazimishe Tena
Sisi binadamu tumetawaliwa sana na miili yetu. Tunaisikiliza miili yetu na inatuongoza kuamua mambo. Miili yetu kiasili haipendi bughudha, hivyo inapokutana na kitu ambacho kitautesa mwili unapeleka taarifa katika akili ya kukata jambo fulani. Tunatakiwa kuamua mambo yetu kwa njia ya kufikiri na siyo kuupa mwili nafasi, anayeusikiliza mwili wake atakuwa mtumwa wa wengine. Unajua …
Umekubali Mwenyewe Iwe Hivyo
Mara nyingi kile kitu ambacho ni muhimu sana katika maisha yetu huwa tunakipa uzito sana. Lakini kama siyo muhimu tunatengeneza mazingira ya kukichukulia poa. Umekubali mwenyewe kuwa hivyo ulivyo leo. Kwa mfano, kama unasafiri bila hata ya kuweka alamu lazima utaamka tu muda muafaka ili usiachwe na gari na muda mwingine unajikuta hata usingizi huna …