Ukienda Kununua Nguo Sokoni

Kila mmoja wetu hapa ameshawahi kununua nguo ya aina yoyote ile. Ulivyokuwa mdogo wazazi wako walikuwa wanakuchagulia karibu kila kitu. Lakini kwa sasa, hawana tena hiyo nafasi bali wewe ndiyo umekuwa mkurugenzi wa maisha yako ambapo unajichagulia kile unachotaka kufanya. Acha tumchukulie mfano mtu anayekwenda kununua nguo, akifika eneo alipoenda kununua nguo atachukua muda kuchagua …

Katika Biashara Hutakiwi Kuwa Na Kitu Hiki

Kila mtu ni mfanyabiashara kwa asili lakini wengine hawajui namna ya kuongea na mteja. Mtu anamchukulia mteja kama vile mtu wa kawaida tu kwake. Wateja hawatakiwi kuchukuliwa kwa namna ya kawaida, bali wanatakiwa kuheshimiwa kwani wao ndiyo wanafanya biashara yako iwe na uhai, kama hakuna wateja basi hakuna biashara hapo. Wateja ni kama vile gari …

Jinsi Ya Kupata Masaa Ya Ziada Katika Masaa 24 Uliyonayo

Moja ya zawadi ambayo Mungu amempa kila mtu basi ni muda. Tajiri na masikini wote wamepewa muda sawa na kufanya kile anachotaka kufanya. Wote tuna masaa 24 katika siku, hakuna aliye mbele au nyuma na tunapokuja kwenye suala la muda wote tunakuwa sawa. Tofauti yetu inakuja kwenye matumizi ya muda tulionao. Wako ambao wanatumia muda …

Usikubali Anayekuonea Aendelee Kukuonea

Rafiki, Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu. Na kuchukulia ni kitu cha kawaida tu. “Simamia utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi” Waoneshe wale wote mwenye tabia ya kukuonea kwamba huwezi kuonewa kirahisi. Wafundishe adabu na watajifunza kupitia wewe na wataheshimu utu wako. Binadamu huwa wanatabia ya kukuchukulia vile …

Kabla Hujainyoosha Dunia Fanya Hiki

Huwa tunajikuta tunataka kuwa viraja wa dunia. Mama Theresa aliwahi kunukuliwa akisema, kama unataka kubadili dunia, nenda nyumbani kaipende familia yako. Kama unataka kuibadili dunia anza kujibadili wewe mwenyewe kwanza. Nyoosha kwanza maisha yako kabla hujajipa jukumu la kuinyoosha dunia. Tunayo mambo mengi sana ya yakufanya na kama tungekuwa tunayafanyia kazi basi tungekuwa mbali na …

Mbinu Moja Nzuri Ya Kuokoa Gharama

Ni kawaida ya matumizi kuongezeka pale kipato kinapokuwa kimeongezeka. Huwa tunajidanganya kuwa kama mshahara au kipato kikiongezeka basi shida zetu zitakuwa zimepungua. Kipato kinapokuwa kimeongezeka zaidi na matumizi nayo huwa yanaongezeka. Mwanzoni ulipokuwa na kipato kidogo ulikuwa huoni hata matumizi makubwa lakini shida inakuja pale tu kipato kinapoongezeka yanaongezeka matumizi ambayo hata hukuwahi kuyafikiria. Nikupe …

Kuwa Sawa Na Wengine Lakini Siyo Eneo Hili

Unaweza kuwa sawa kama wengine, ukala kile ambacho wengine wanakula, wanakunywa. Unaweza kuvaa kama vile wengine wanavyovaa, kucheza kama wengine wanavyocheza lakini; Kamwe usiwe wa kufikiri sawa na wengine na kuamuliwa kile ambacho unataka katika maisha yako. Unaweza kuwa sawa na wengine katika maeneo mbalimbali lakini siyo kwenye kufikiri, ili uwe wa tofauti lazima ufikiri …

Mafanikio Yote Yanaanza Kitu Hiki

Sisi binadamu tuna asili ya uvivu ndani yetu, miili yetu huwa haipendi sana shida ndiyo maana hata wakati wa kuamka asubuhi kutoka kitandani unakuwa unapata upinzani mkubwa kutoka katika mwili wako. Mwili huwa unataka kile unachotaka, hivyo ukiwa ni mtu wa kuusikiliza mwili utavuna mabua, mwili hauhitaji uwe mtu wa demokrasia bali udikteta. Mafanikio yote …

Je Una Amini Kauli Hii?

Mimi nina amini kauli ya mwandishi na mwanafalsafa Zig Ziglar inayosema; Unaweza kupata kitu chochote kwenye maisha yako kama ukiwasaidia watu wengine vya kutosha kupata kile wanachotaka. Kama unahitaji kupiga hatua ni lazima uwasaidie wengine kupata kile wanachotaka na wewe utapata kile unachotaka. Huwa tunapambana nakuamini kuwa mafanikio yatakuja kwa jeshi la mtu mmoja. Mafanikio …

Hakuna Aliyeamka Na Kujikuta Ana Deni Hili

Kila kitu kinaanza kidogo, huwa tunadharau vitu vidogo kumbe vitu vidogo tunavyovichukulia poa ndiyo vinatuletea madhara makubwa. Hakuna tatizo kubwa bila tatizo dogo. Tatizo lolote kubwa limeanza likiwa dogo. Hata katika tabia, hakuna tabia ambayo unayo leo iliyoshuka kutoka mbinguni kwa siku moja bali tabia ambayo unayo leo ilianza kidogo kidogo na hatimaye leo kuwa …

Design a site like this with WordPress.com
Get started