Je Unavumilia Hali Hii Hapa?

Tunaalikwa kuwa wavumilivu katika maisha yetu. Lakini siyo kila kitu ni cha kuvumilia kwanini kila kitu siyo cha kuvumilia? Katika maisha ya binadamu kuna mambo ya aina mbili;Moja; haya ni yale mambo ambayo yako ndani ya uwezo wetu.Mbili; haya ni yale mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu Sasa kama jambo lipo ndani ya uwezo …

Je Una Maadui? Kama Huna Maana Yake Umekosa Hiki

Duniani hakuna malaika bali kuna binadamu ambao asili ya binadamu ni kukosea. Hakuna mtu ambaye mwenye akili timamu atatoka hapo alipo na kwenda kumpiga teke mbwa aliyekufa. Ukiona huna maadui maana yake huna unachofanya ni sawa na mbwa aliyekufa hakuna mtu atakayeangaika naye. Je ulishawahi kuona watoto wanakwenda kuhangaika na mti ambao hauna matunda? Mti …

Je Umesikia Hiki?

Ni kawaida katika jamii yetu tunayoishi kukutana na mengi kwa sababu panapokuwa na wengi pia pana mengi. Iko tabia moja ambayo hata wewe umeshawahi kuisikia, mtu anakuja kwako anakuambia umesikia kitu fulani? Dalili ya mtu mwenye umbea na ambaye hana uhakika na kile anachosema ni ataanza na nimesikia moja mbili tatu. Unakuta mtu hana uhakika …

Mshukuru Mungu Hata Kwa Kuwa Na Zawadi Hii

Tunavyo vitu vingi sana vya kushukuru, karibu kila kitu tulichonacho hatuna budi kushukuru na nikisema nivitaje itakua ni litania(orodha)ndefu sana. Kila binadamu amepewa uwezo wa akili, wa kutambua zuri na baya. Utashi huu tuliopewa ndiyo unatufanya sisi kuwa viumbe bora kuliko wengine. Leo kupitia makala hii, tunakwenda kujifunza zawadi ambayo tunapaswa kushukuru kwa kuwa nayo …

Nyote Njema Huonekana Hata Jioni

Siyo kila siku nyota njema itaonekana asubuhi tu. Mambo yanabadilika sana kiufupi siyo rahisi kutabiri kila kitu na kikatokea sawa. Hakuna mtabiri wa uhakika katika haya maisha kwani yale tunayotabiri ni kama kubashiri tu lakini kuamua matokeo gani ya utabiri ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako. Wakati mwingine unaanza siku yako vizuri, huku …

Bila Nidhamu Hizi Huwezi Kuthubutu

Kinachotufanya tusipige hatua kubwa ni nidhamu tu.Wanaofanikiwa ni wale ambao wana nidhamu kwenye kile wanachofanya. Unatakiwa kuwa na nidhamu ya kazi, fanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu na zalisha ubora.Toa thamani kubwa na jua kuwa kazi ndiyo rafiki wa kweli ambaye hatoweza kukuangusha pale unapokuwa na shida.Watu ni rahisi kukuangusha lakini kazi haiwezi …

Kama Usipowaambia Watu Unauza Nini, Hawawezi Kujua Hili

Wanasema biashara ni matangazo. Ukitaka kuuza kitu lazima ukitengenezee mazingira ya kutaka kukiuza kwa mfano, una bidhaa ya mchele na unataka watu wanunue inabidi utoe mchele wa sampo uweke mahali panapoonekana na uwaambie watu kuwa unauza mchele, lakini ukiwaambia watu unauza mchele halafu umeuweka ndani hakuna anayeuona hakuna atakayejua. Kama usipowaambia watu unauza nini watu …

Jinsi Ya Kujitafuta Wewe Mwenyewe

Huwa tunakua bize kuwatafuta wengine, tunataka kujua mambo ya wengine yakoje lakini tunasahau sana kutafuta kujua mambo yetu binafsi. Baba wa falsafa mwanafalsafa Socrates aliwahi kunukuliwa akisema, ukitaka kujitafuta wewe mwenyewe, jifikirie kuhusu wewe mwenyewe. Hatuwezi kujua matatizo yetu ya ndani kama tusipojitafuta sisi wenyewe. Tutajua mengi kuhusu sisi wenyewe pale tutakapojitafuta kwa kujifikiria sisi …

Kama ulianguka Jana Fanya Kitu Hiki Leo

Ni kawaida yetu sisi binadamu kuanguka katika mengi, lakini kuanguka siyo sababu ya sisi kuendelea kuwa chini. Kama vile ilivyo dunia, inatupa usiku na mchana nasi tunatakiwa kuishi hivyo. Pale unapokuwa umeanguka unapaswa kunyanyuka juu. Usiendelee kukomaa na hapo chini bali nyanyuka juu. Kama jana ulianguka , unachotakiwa kufanya ni leo kuamka. Kila mtu anaanguka, …

Design a site like this with WordPress.com
Get started