Usibinafsishe Majukumu Yako Ya Kifamilia

Leo asubuhi nilivyoamka nilisoma kitabu cha philosophy of happiness kilichoandikwa na mwandishi Avitus Leonard, katika kitabu chake mwandishi alitumia mifano ya viongozi wakubwa duniani wanasemaje kuhusiana na furaha baada ya kuwanukuu wanafalsafa wengi. Basi nikakutana na sehemu ambayo mwandishi amemchagua kiongozi wa kanisa katoliki duniani kama mfano, Papa Francis ameshauri mengi ni namna gani mtu …

Hiki Ndiyo Kitu Ambacho Mtu Akikitafuta Huwa Hakikosi

Waswahili wanasema penye nia pana njia. Wengi wetu tumekuwa na ndoto nzuri lakini tafiti zinasikitisha sana. Licha ya watu wengi kuwa na ndoto ambao wanatimiza ndoto zao ni wachache sana. Sisi binadamu ni wazuri sana katika kutafuta sababu kuliko kutenda kile ambacho tumepanga kufanya. Kitu pekee ambacho mtu akikitafuta huwa hakikosi ni sababu. Mtafuta sababu …

Hii Ndiyo Njia Bora Ya Kumfundisha Mtu

Watu wengi huwa hawapendi kuonekana hawajui, hivyo namna ambayo huwa tunawafundisha watu huwa inasababisha migogoro mingi. Kila mtu huwa anaamini anajua hata kama hayuko sahihi, na kila mtu anapenda kusikilizwa kwa kile anachojua yeye, wakati mwingine usiingie kwenye mabishano ambayo hayakuiingizii hata mia, mwachie mtu nafasi ya kujiona mshindi kwenye kile anachokiamini yeye na mteja …

Kama Huna Sifa Hii, Usifungue Biashara Yoyote Ile

Kiasili kila mtu ni mfanyabiashara, kila mtu kuna kitu huwa anauza kwa mwingine ili awepe kupata fedha ya kuendesha maisha yake. Bila kuuza, huna mauzo utakayopata na mauzo ndiyo yanatupa fedha za kuwalipa wengine na kujilipa sisi wenyewe. Kwa chochote kile unachofanya jua namna ya kuteka hisia za watu ili uweze kuuza kile unachotaka.Watu wanapenda …

Njia Pekee Ya Kuwafanya Watu Wakupe Kile Unachotaka

Mafanikio yoyote yale tunayotaka kwenye maisha yetu tayari yako kwa wengine. Chochote tunachofanya tunawategemea wengine ili nasi tuweze kufanikiwa. Kumbe basi, kama tunataka kufanikiwa kwenye kile unachofanya anza kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka. Mwanasaikolijia Sigmund Freud aliwahi kunukukiwa akisema kile ambacho watu wanakifanya kinasukumwa na tamaa mbili, ngono na ukuu. Mwanafalsafa John Dewey anasema hitaji …

Usiache Kufanya Kama Unaweza

Usikubali kuishi maisha ambayo hayana maana ndani kwako, maisha mazuri ni yale ya kuishi kusudi la maisha yako. Changamoto kubwa iko katika kujua kusudi la maisha yako, na hili ndilo linawafanya watu wengi mpaka wanakufa bila kujua haswa nini wanataka kwenye maisha yao. Kwenye kitabu cha Ongea Lugha Yako, sikiliza sauti yako ya ndani ndiyo …

Usiogope Kuuliza Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Kuuliza siyo ujinga. Unapokuwa una safari kwenda sehemu usiyojua yaani wewe unakuwa mgeni huwezi kuona aibu wala kuogopa kuuliza.Lazima utauliza ili usije ukapotea lakini pia uweze kufika kule unakotaka kufika. Unapokuwa hujui kitu, usiogope kuuliza kitu. Hakuna mtu anayejua kila kitu, hivyo unapomuuliza mtu atakujibu kama kipo ndani ya uwezo wake.Na mara nyingi watu wanapenda …

Usimchinje Ng’ombe Wako Kwa Oda Ya Maini

Ni watu wa chache sana wanaishi maisha wanayotaka kwa sababu wengi hawaishi vile wanavyotaka bali wanaishi vile wanavyotaka wengine. Je hayo maisha unayoishi ndiyo maisha yako halisi? Huwa tunaigiza maisha yetu mchana lakini ikifika usiku huwa tunakutana na sisi wenyewe tunajiona kabisa ni watupu na kile tunachofanya siyo sahihi. Utaweza kuwadanganya watu wote lakini huwezi …

Tatizo Lako Liko Hapa

Kama unapata maarifa ya kukuwezesha kuwa bora basi unatakiwa kuwa bora kweli. Usipokuwa bora utakua huna tofauti kabisa na yule mtu ambaye hajifunzi. Kwa chochote kile unachojifunza jaribu kubadilika hata watu unaoishi nao waone kweli una kitu cha tofauti ndani yako. Tatizo lako ni kwamba uko hivyo ulivyo kwa sababu ya kutochukua hatua sahihi. Kwa …

Hii ndiyo Njia rahisi kuliko zote duniani za kuwa tajiri

Wote tunajua kuwa ni jinsi gani fedha ilivyokuwa muhimu kwenye maisha yetu. Inatusaidia kuendesha maisha yetu na kulipa bili mbalimbali. Fedha ni muhimu kweli na hilo halina ubishi hata kidogo. Kila mtu anatamani awe na uhuru wa kifedha wa kumwezesha kufanya kile anachotaka na watu wengi hawana uhuru wa kifedha na dalili moja wapo ya …

Design a site like this with WordPress.com
Get started