Kwenye vitu vingi vina ukomo wake. Hata maisha yetu tunayoishi yana ukomo wake. Hata tunaposafiri kutoka eneo moja kwenda lingine tunakuwa tunajua kabisa mwisho wetu ni wapi. Lakini katika safari ya ubora hakuna kikomo. Ubora hauna kikomo. Hakuna mahali utakuja kusema kwa sasa nimefikia mwisho wa ubora wa kile ninachofanya. Ubora wowote ule unaofanya jua …
Category Archives: Uncategorized
Msamiati Wa Kuuvunja Katika Eneo Lako La Fedha
Fedha huwa haina kikomo. Hata ukiangalia idadi ya watu duniani ni ndogo kuliko fedha zilizopo. Ukomo wa fedha unauweka wewe mwenyewe na wala si mtu mwingine. Na leo tunakwenda kujifunza ni kwa namna gani tunakwenda kuuvunja msamiati unaokuletea ukomo wa kifedha. Kuanzia leo ukiwa na shida ya kiwango kikubwa cha fedha usiende kusema siwezi kuzipata …
Continue reading “Msamiati Wa Kuuvunja Katika Eneo Lako La Fedha”
Ifahamu Sifa Inayodumu Milele
Kila mmoja wetu ana sifa. Lakini sifa tulizonazo zinatofautiana kadiri ya mtu. Hebu jiulize wewe una sifa gani ambazo zitadumu milele?Watu wakitaja jina lako kitu cha kwanza wanapata sifa gani kutoka kwako? Nilipokuwa nasoma kitabu cha Yoshua Bin Sira nilijifunza kuwa maisha mema yana siku zake na sifa njema yadumu milele. Kumbe basi, sifa njema …
Hii Ndiyo Rasilimali Muhimu Kwenye Malezi Ya Watoto
Karibu kila familia ina mtoto na kama haina basi inatazamia kuwa na mtoto. Kwenye malezi ya watoto wazazi au walezi huwa wanakutana na changamoto mbalimbali. Ubaya ni pale umepatwa na tatizo halafu huna fedha ya kutatua tatizo linalokukabili. Changamoto nyingine kwenye malezi siyo changamoto bali ni ukosefu wa fedha. Kama tatizo la mtoto linaweza kutatuliwa …
Continue reading “Hii Ndiyo Rasilimali Muhimu Kwenye Malezi Ya Watoto”
Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kama Unataka Kuanza Biashara
Pale unapoanza biashara yoyote ile biashara yako inakuwa haina tofauti na mtoto mchanga kwani inahitaji uwepo wako sana. Biashara ni kama mtoto mchanga, kama unavyoelewa mtoto mchanga anavyomhitaji mama yake ndivyo ilivyo katika biashara siku za mwanzo. Itahitaji muda wako;Biashara yako itakuwa kama mtoto wako hapo mwanzoni itakuhitaji muda wako mwingi usipojitoa haswa kwenye biashara …
Continue reading “Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Kama Unataka Kuanza Biashara”
Asiyehusika Atoke Nje
Huwa tunajeruhiana katika mengi. Muda mwingine huwa tunawakwaza wengine pasipo hata sisi kujua kadiri ya mienendo yetu ya maisha. Kila mmoja wetu ana majeraha yake ya moyo, ambayo akikaa chini na akikumbuka mapito aliyopita anahisi kupatwa na uchungu na kupelekea kulia. Usifiche hisia pale unapohisi kupatwa na uchungu unapokumbuka mapito uliyopita. Unapohisi kulia lia kabisa …
Hii Ndiyo Faida Ya Kukutana Na Mtu Yeyote Yule
Natumaini ulishawahi kusafiri, ulishawahi kwenda kwa rafiki yako na maeneo mengi uliyotembelea hukubaki kama ulivyokuwa hapo awali. Mara nyingi pale unapokutana na mtu mwingine au unapoenda sehemu huwa unajifunza kitu cha kwenda kukifanyia kazi kwenye maisha yako. Kila mtu unayekutana naye anakuwa na kitu cha kukufundisha na hii ndiyo faida kubwa ya kukutana na mtu …
Continue reading “Hii Ndiyo Faida Ya Kukutana Na Mtu Yeyote Yule”
Jenga Utaratibu Huu Wa Kihistoria Kwenye Maisha Yako
Hakuna juhudi yoyote utakayoiweka na kwenda bure. Asili huwa inatabia ya kulipa juhudi ya kila mtu hata kama hujalipwa leo ila utalipwa tu. Juhudi ya mtu huwa haipotei hata siku moja hivyo endelea kuweka juhudi na iko siku dunia itakupa kile unachotaka kwenye maisha yako. Watu wengi wanaofanikiwa sana ni wale watoaji. Wale wanaotoa juhudi …
Continue reading “Jenga Utaratibu Huu Wa Kihistoria Kwenye Maisha Yako”
Jinsi Ya Kupunguza Uwezekano Wa Kushindwa
Hakuna mtu ambaye hashindwi katika maisha yake. Kila mtu anashindwa. Lakini anayeshindwa zaidi ni yule mtu anayeshindwa na kuishia kukatia tamaa pale pale bila kuendelea. Katika safari ya mafanikio hakuna kushindwa bali kuna kujifunza hivyo unaposhindwa unakua unajifunza. Je namna gani unavyoweza kupunguza uwezekano wa kushindwa kwenye chochote kile unachofanya? Jawabu; unaweza kupunguza uwezekano wa …
Continue reading “Jinsi Ya Kupunguza Uwezekano Wa Kushindwa”
Usikubali Siku Yako Ipite Bila Kupata Ushindi Wowote Ule
Hakuna anayelala na kujua kesho yake itakuwaje, licha ya kuamini mambo yatakuwa mazuri lakini hili ni jambo ambalo liko nje kabisa ya uwezo wetu. Hatuwezi kujua leo tutakutana na changamoto gani, hivyo basi pale tu unapoamka hakikisha unajihakikishia ushindi ili siku yako isiende bure.Yako mambo mengi ambayo unaweza kujihesabia ushindi kabla hujaenda kuwatumikia wengine. Kwa …
Continue reading “Usikubali Siku Yako Ipite Bila Kupata Ushindi Wowote Ule”