Kama Ukitengeneza Maana, Utatengeneza Hiki

Iko njia moja ya uhakika ya kupata fedha. Usidanganyike na njia za panya. Watu watakuambia kuna njia rahisi ya kupata fedha, jiulize kama kuna njia rahisi ya kupata fedha kwanini wasiwe nazo wao? Kuna mtu ambaye hana shida ya fedha? Sasa ukiona mtu anakuambia njia rahisi ya kupata fedha, jua wewe ndiyo fedha yenyewe. Ukiona …

Tumia Mbinu Hii Kama Unataka Kujua Uwezo Wa Watu

Kila mmoja wetu Mungu amemwita kuja duniani kwa kusudi fulani. Imani yangu ni kwamba kila mtu ana uwezo mkubwa wa kutenda miujiza ndani yake. Pia, hakuna mtu ambaye hafai kwa lolote. Hakuna mtu anayeweza kuwa kama wewe, ndiyo maana tunaishia kusema, anafanya kama fulani lakini siyo kama fulani. Pengo la mtu linazibwa na mtu mwenyewe. …

Kamwe Usijiambie Kitu Hiki

Siku zote unapaswa kufikiria kile unachotaka kwenye maisha yako na siyo kile usichotaka kwenye maisha yako. Unajua unakuwa unakosea pale ambapo unakuwa unafikiria sana vitu ambavyo huvitaki. Na kawaida ya akili huwa inafanya kile kitu ambacho huwa unakifikiria sana. Kumbe kufikiria kile usichokitaka ni njia ya kujifungulia milango ya nuksi. Akili yako inapaswa kufikiri kile …

Nguvu Yako Iko Hapa

Usipende kujipa kazi ambazo ziko nje ya uwezo wako. Usitake dunia iende kama vile unavyotaka wewe. Usitake kuwa kiranja wa dunia, utashindwa vibaya. Yaani unataka kila kitu ukitawale na kiende kama vile unavyotaka wewe. Dunia huwa inajiendesha kwa misingi yake yenyewe. Inafanya kile inachotaka hivyo unapaswa kuelewa kuwa kuna vitu viko nje ya uwezo na …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Hawawezi Kubadilisha Kitu Chochote

Kama unahitaji mabadiliko yoyote yale ni lazima ukubali kufanya mabadiliko. Hakuna mabadiliko yoyote bila mabadiliko. Mabadiliko yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Hakuna anayeweza kukwepa mabadiliko kwa namna yoyote ile. Mabadiliko yoyote yanayotokea duniani lazima yatakuathiri tu aidha unataka au hutaki. Hakuna mabadiliko yanayotokea duniani yakakuacha salama. Watu ambao hawawezi kufanya mabadiliko yoyote yale ni wale …

Fanya Kitu Hiki Mwenyewe

Ni kawaida kwa watu wengi huwa hawawezi kufanya kitu bila kusimamiwa. Siyo watu wote wana ile nidhamu ya kujisimamia wao wenyewe. Nidhamu binafsi ni changamoto ndiyo maana hata katika mafanikio watu wanatofautiana sana. Wengi huishia kuahirisha mambo kila siku. Huku wakijipa muda kuwa watafanya kesho au baadaye. Watu wanafanya kitu bila sababu yoyote ile pale …

Ufahamu Mwanzo Wa Upendo

Huwa watu wanapenda kupima upendo wao kwa vitu. Wengi wanatoa upendo ili waweze kupata maslahi fulani. Mtakatifu Agustino, aliwahi kunukuliwa akisema, kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Je wangapi unawapoteza kwa sababu ya upendo wa kipimo? Mwanzo wa upendo wowote ule ni tabasamu. Tunaanza kuonesha upendo kupitia tabasamu letu la ndani. Unapokutana na mtu …

Wasaidie Wengine Na Wewe Utasaidiwa

Kuwa mtu wa kujali maslahi ya wengine na utashangaa na wewe maslahi yako yanaenda vizuri sana. Kama huna fedha wasaidie wengine kupata fedha na wewe utapata fedha. Yaani toa thamani itakayowasaidia wao kupata fedha. Kuwa mtu wa kujitolea kuwaombea wengine katika shida zao. Utajikuta na wewe shida zako zinatatuliwa bila hata kujijua. Unaposumbuka na matatizo …

Walioshindwa Wana kitu Hiki Kimoja

Kiasili, binadamu ni wagumu kukubali kosa. Hata kama amefanya kweli lazima atajitetea kuonesha kwamba siyo yeye aliyehusika bali ni wengine. Kaa ukijua kwamba tatizo lolote ulilopata nawe umechangia kwa namna moja au nyingine. Kuna mambo mengi huwa tunachangia sana kutokea lakini huwa tunaona sisi hatuhusiki bali wengine ndiyo wanahusika kufanya. Unapopata kile ambacho hukutarajia kukipata …

Jinsi Ya Kupata Utulivu Wa Akili

Watu wengi kwa sasa wamevurugwa yaani kifupi watu hawana utulivu wa akili. Akili za watu wengi zimekuwa hazina utulivu. Zimekuwa kama nyani anayeruka tawi hili na kutua lile. Kwenye zama za mafuriko ya taarifa na maarifa ni zama ambazo unapaswa kuwa makini sana maana usipokuwa makini watu wengine watakutumia ili waweze kupata kile wanachotaka. Utulivu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started