Jinsi Ya Kung’arishwa Na Mawimbi Ya Maisha

Kama maisha ni shule, basi changamoto ndiyo darasa lenyewe. Dunia huwa inatupa mafunzo kila kukicha kupitia yale tunayokutana nayo.Dunia inatupa mafunzo ambayo yanatuwezesha kukua, kubadilika na kuamsha madhumuni yako makubwa hapa duniani. Huwezi kufeli katika haya maisha kama uko tayari kujifunza. Kama ambavyo vyombo ili vitakate huwa vinasuguliwa na stili waya. Kusuguliwa kule na stili …

Kama Unajifunza Sana Na Hupati Matokeo Unayotaka Shida Yako Iko Hapa

Vuta picha tokea umeanza kujifunza mpaka leo umeshajifunza vingapi? Angalia yale uliyojifunza yanaendana na mafanikio uliyonayo? Kuna wale watu ambao wananunua vitabu na kulipia maarifa mbalimbali. Wanajifunza kweli lakini, cha ajabu wanaishia kuwa na maisha ya kawaida. Wewe unafikiri shida iko wapi? Kwanini upate maarifa ya kuwa bora na ufanane na mtu ambaye hana maarifa …

Jihamasishe Kwa Mafanikio Unayopata

Kuna njia mbili za hamasa, moja adhabu na mbili ni zawadi. Ukiwachukua watu wawili na mmoja umhamasishe kwa njia ya zawadi atafanya vizuri sana, atajituma kuhakikisha anapata zawadi yake. Lakini, njia ya adhabu huwa haimsukumi mtu kufanya jambo na kama unataka kuwapoteza watu wahamasishe kwa njia ya adhabu lakini zawadi inafanya vizuri sana. Kwa mfano, …

Angalia Usalama Wa Fedha Zako

Wako watu ambao wanawekeza kupoteza na wako ambao wanawekeza kupata.Wale wanaowekeza kupata ni wale ambao wanafuatilia kwa karibu sana kile walichowekeza. Wale ambao wanawekeza kupoteza ni wale ambao wanawekeza fedha zao sehemu na kukosa muda wa kuzifuatilia. Nikupe ushauri wa bure rafiki yangu, popote pale ulipowekeza fedha zako hakikisha macho yako, yako pale. Kuwa mtu …

Usikubali Kushindwa Kwenye Kila Kitu

Ndugu mmoja katika maadhimisho ya miaka 50 ya seminari ya maua ambapo walikutana wale wote waliosoma pale alitoa ushuhuda wake kwa uchungu akasema, huwa anamwambia Mungu kila mara nimeshindwa kuwa Padre na hata wito wa ndoa unishinde? Kauli hiyo inamfanya awe imara kwenye ndoa yake licha ya kushindwa kwenye eneo fulani. Rafiki yangu, usikubali kushindwa …

Kuwa Na Vitu Hivi Viwili Na Mambo Mazuri Yanakwenda Kutokea

Wewe ndiyo kiungo namba moja wa kile kinachoendelea kutokea kwenye maisha yako. Iwe unajua au hujui, wewe ndiyo unahusika kwa asilimia 100 na matokeo unayoendelea kupata sasa. Wewe ni mchangiaji namba moja wa matokeo uliyopata, unayopata na utakayoendelea kuyapata. Kwa kulijua hilo, leo nakwenda kukushirikisha mambo mawili ambayo yatakwenda kubadili maisha yako na kukuletea mambo …

Kama Umekosa Hamasa Ya Ndani Nunua Hamasa Ya Nje

Ziko aina mbili za hamasa, moja hamasa ya ndani na pili hamasa ya nje.Hamasa nzuri ni ile hamasa inayotoka ndani yako na hamasa ya nje ni ile inayotoka nje kwa kuangalia wengine wanafanya nini na wewe kuhamasika. Pale unapojikuta umepoteza hamasa juu ya kile unachofanya. Unapaswa kununua hamasa ya nje. Angalia wale ambao wanafanya kile …

Njia Rahisi Ya Kuacha Alama Duniani

Ni nani kati yetu anapenda kufa na kusaulika kabisa? Kila mtu anataka aache alama duniani isiyofutika ili hata vizazi vinavyokuja viweze kujifunza kutoka kwake. Iko njia nyingine rahisi sana ya kuacha alama duniani, kabla sijakuambia ni njia gani nikuulize swali je ni kitu gani kwa sasa unachofanya? KamaKuna kitu unachotoa kwa wengine basi hapo hapo …

Miaka 4 Ya Kuandika Kila Siku

Ilikuwa mwaka 2016 octoba mosi, nilipoanza safari ya kuandika kila siku. Hakika, namshukuru Mungu aliyeniwezesha kufanya yote haya. Kila siku nilikuwa natafuta mfumo, ni namna gani ninaweza kuandika kila siku. Mwandishi Makirita Amani alipoanza safari yake ya kuandika kila siku mwaka 2015 alinivutia na mimi. Ndipo ilipofika mwaka 2016 octoba mosi alipoanzisha Marathon ya kuandika …

Haya Ndiyo Maisha Mazuri Ya Kuishi

Je hayo ndiyo maisha yako halisi unayoishi?Je una furaha na maisha yako?Watu wengi hawaishi maisha mazuri wala kufurahia maisha yao kwa sababu hawajui haswa nini wanataka kwenye maisha yao. Hivi kama hujui kile unachotaka utawezaje kupata kile unachotaka? Mafanikio ya kwanza unayopaswa kuwa nayo ili uishi maisha mazuri ni kuweza kujua nini haswa unataka kwenye …

Design a site like this with WordPress.com
Get started