Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kosa Moja Ambalo Wauzaji Wengi Wanafanya

Mwandishi na  aliyekuwa  muuzaji  mzuri sana  wa  magari  Joe  Girard,  ambaye  aliingia kwenye  kitabu  cha  maajabu  cha  dunia,  GUINESS,  kama  muuzaji  bora  sana  kuwahi kutokea  hapa  duniani,  anatushirikisha  jinsi gani KILA  MTU,  ANAWEZA  KUUZA CHOCHOTE KWA MTU YEYOTE kupitia kitabu chake cha jinsi ya kuuza chochote kile kwa mtu yeyote. Kupitia mauzo tunapata zawadi mbili, …

Fanya Kazi Masaa Mengi Au Uondoke

Tajiri namba moja duniani Elon Musk hivi karibuni amenunua mtandao wa Twitter. Kwa kuwa huyu Bilionea ni mtu anayeamini kwenye kazi sana, hivyo amewataka wafanyakazi wake wafanye kazi sana. Amewaambia wana machaguo mawili,Moja wafanye kazi masaa mengiMbili au waondoke. Hapa tunajifunza kwamba, kazi ndiye rafiki wa kweli. Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kufanya kazi masaa …

Hii Ndiyo Biashara Inayofanikiwa

Unaweza kufikiria biashara inayofanikiwa ikoje? Hebu pata picha. Biashara inayofanikiwa siyo ile inayokuwa bora, bali ile inayokuwa ya kwanza kwenye akili za wateja. Je, watu wakiwa wanataka huduma unayotoa, huwa wanaifikiria biashara yako? Kama biashara yako haiko kwenye akili za watu ni ngumu kufanikiwa. Kwa chochote kile unachouza, hakikisha watu wanajua unauza nini, watu huwa …

Umuhimu Mkubwa Wa Kuimarisha Mahusiano Yako

Iko hivi rafiki yangu nikupendaye, Kwa chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kwa watu wengine. Mafanikio unayotaka kuyaona kwenye maisha yako, watakaokusaidia kupata ni watu wengine. Kifupi kile tunachotaka tutakipata kupitia watu wengine, watu wanakutegemea ili wafanikiwe kupitia wewe. Unahitaji  kuwa  na  mtandao  wa  watu  ambao  wanaweza  kukusaidia  kwenye  maeneo mbalimbali  na  wewe  pia  …

Njia nzuri Ya Kukabiliana Na Kumbukumbu Zinazokufanya Ulie

Kama kumbukumbu za nyuma zinakufanya ulie, ziandike kwenye karatasi kwa umakini na ukamilifu. Huwa tunapitia mengi, wako ambao wametujeruhi mioyo yetu na kutuachia majeraha moyoni. Wakati mwingine kumbukumbu tunazobeba, zinaweza kuwa mzigo kwetu na unaoturudisha nyuma, tunahitaji kuutua. Sasa kitendo tu cha kuandika zile kumbukumbu, unakuwa umekitua kutoka kwenye akili yako na kinaacha kuwa mzigo …

Fanya Kitu Hiki Muhimu Kwako

Fanya kile ambacho ni muhimu kwako na siyo ambacho ni rahisi kwako. Kwa sababu, kila mtu anataka kukata kona, kila mtu anatafuta njia ya mkato ya mafanikio. Kila mtu anatafuta njia ya kupata fedha bila ya kufanya kazi. Usiwe katika watu hao, wewe fanya kazi halali na upate fedha halali. Usitafute kilicho rahisi, kwa sababu …

Vitu Vya Kuzingatia Kwa Muuzaji

Kitu  cha  kwanza  kinachowasukuma  watu  kununua  ni haiba  ya muuzaji.  Na  haiba  ya  mtu  inatokana  na  tabia  ambazo  mtu  anazo.  Ili kufanikiwa  kwenye jambo  lolote,  unahitaji  kuwa  na  tabia  nzuri  ambazo  zinawafanya  watu  kukubaliana  na wewe.  Kumbuka  ndege  wanaofanana  huruka  pamoja,  hivyo  kuwavutia  watu  wa  aina fulani,  lazima  uwe  kama  wao. Hatua ya kuchukua leo; …

Mambo Mawili Ya Kuzingatia Katika eneo La Fedha

Moja, USICHEZE NA HELA. Kuwa makini na hela zako, zisimamie vizuri na wekeza sehemu salama unayoweza kuifuatilia kwa umakini. Mbili, USIENDE MAHALI NA FEDHA UNAYOTAKA KUTUMIA TU. Kwa kifupi kwenye maisha usiwe na kiasi cha fedha unachohitaji kwa matumizi tu, unahitaji kuwa na kiasi cha fedha kwa ajili ya dharura. Hatua ya kuchukua leo; USICHEZE …

Unakuwa Wa Maana Pale Unapofanya Hiki

Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye maisha unakuwa wa maana pale unapotimiza wajibu wako. Kwenye biashara unakuwa wa maana pale unapotekeleza wajibu wako kwenye biashara. Na ustaarabu wa kwanza kwenye biashara ni kuuza na kama huuzi kwenye biashara basi unapoteza maana. Unapoteza maana kama uko kwenye kazi fulani halafu huifanyii kazi hiyo kazi. Unapoteza maana kwenye mahusiano …

Zifahamu Tabia Mbili Za Watu

Sina uhakika kama itakufaa lakini watu wana tabia kuu mbili nazo ni; Kwanza  watu  ni viumbe  wa  kijamii  kwa  sababu wanawapenda  na  kuwajali  watu  ambao  wapo  ndani ya  kundi moja. Nafikiri hili halina ubishi, binadamu ni watu wa ambao tunajali wale ambao tupo kundi moja. Kwa mfano, shabiki wa timu x atamjali shabiki timu x …