Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usimwambie Mtu, Nimekuambia Wewe Tu

Ni maneno ambayo watu huyatumia kujihakikishia usalama pale wanapotoa jambo lao kwa watu wengine. Usijidanganye kwamba ukimwambia mtu hivyo ndiyo mambo yatakuwa safi bali ndiyo kama vile umemwambia fanya. Kama una jambo lako na unataka watu wasijue ni bora usiseme kabisa kuliko kusema halafu unamwambia nimekuambia wewe tu lakini usimwambie mtu mwingine.Wimbo unakuwa ni mmoja …

Huenda Hujafanya Jukumu Lako Vizuri

Dunia itakuwa sehemu salama kwa kila mmoja wetu endapo kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake. Matatizo mengi yanayotokea ni watu kushindwa kutimiza majukumu ipasavyo. Ukishindwa kutimiza wajibu wako jua kwamba unawaumiza wengine. Kila mmoja wetu anamtegemea mtu mwingine ili maisha yake yaende. Endapo unasitisha kile unachofanya basi unakuwa siyo tu kufanya dhambi lakini unaifanya dunia …

Mbinu Nzuri Ya Kutumia Pale Unapoona Umetingwa Na Mambo Mengi

Ukiona umebanwa na una mambo mengi ya kufanya huku muda wako ukiwa mchache unapaswa kufanya yafuatayo; Moja, futa yale yote yasiyo na tija kwako. Watu wengi wanasema wako bize lakini kwenye mambo ambayo hayana tija kwao. Jiulize, hicho kinachokufanya uwe bize kinaleta fedha mfukoni? Kama jibu ni ndiyo, endelea kukifanya lakini kama jibu ni hapana, …

Kitu Cha Kwanza Kuangalia Kabla Hujamsaidia Mtu

Pata picha unatoka nje ya nyumba yako unaona moshi unatoka mahali na ukakimbilia kuondoa moshi huo, kawaida hutazuia moshi kuendelea kutoka kwa sababu kwa akili za kawaida kabisa penye moshi, chini pana moto. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye watu, unapomwona mtu yupo kwenye matatizo, jua kuna kitu kimesababisha. Sasa ukikimbilia kumsaidia kumsaidia mtu kuondokana na …

Licha Ya Madhaifu Yako, Bado Wewe Ni Mtu Muhimu Sana

Rafiki yangu nikupendaye, Pamoja na madhaifu yako, bado wewe ni muhimu. Moja ya mambo yanayopelekea tusijijali sana ni kwa sababu tunajijua sisi wenyewe kuliko mtu mwingine anavyotujua, kuliko tunavyowajua watu wengine. Sasa inapotokea pale tunapojikumbusha madhaifu yetu, mabaya ambayo tumewahi kufanya huko nyumaz tunajiona tunastahili mateso na hivyo kutokujijali kama tunavyowajali wengine. Tunakuwa tunajiona sisi …

Jinsi Mabadiliko Yanavyokuua

Ray Norda anasema ukisababisha mabadiliko, unakuwa kiongozi wa mabadiliko, unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa. Na pale unapokabiliana na mabadiliko, unapona kwenye Mabadiliko hayo. Lakini pia mabadiliko hayatakupoteza. Ila ukiyapinga mabadiliko, mabadiliko yanakuua na yanakupoteza kabisa. Hatua ya kuchukua leo; popote pale ulipo, kuwa chanzo cha mabadiliko na mara zote utakua mbele na kufanikiwa. Kitu …

Maisha Gani Haya?

Kwako rafiki yangu, Usikubali kuishi maisha ambayo hayana maana hapa duniani. Usikubali kuishi bila kujifunza, unapojifunza unapata hekima ya kukuwezesha kufanya maamuzi. Usikubali kufanya kazi pasipo kuwekeza wala kuweka akiba. Uwekezaji unakuza utajiri wako na akiba inakulinda wakati unauhitaji wa fedha. Usikubali mtu akupite kwenye kazi, kubali watu wakupite maeneo yote lakini usikubali upitwe katika …

Ondoa Dhana Hii Kwako

Kiasili hakuna kitu kibaya wala kizuri. Kila kitu kipo kadiri ya mtazamo wako. Mtazamo uliokuwa nao leo ndiyo unakufanya uwe hivyo ulivyo leo. Una mtazamo gani juu ya utajiri, kazi, biashara, mahusiano n.k? Ondoa dhana hii kwamba, nimeumizwa, na hakuna atakayeweza kukuumiza. Unaumizwa kwa sababu wewe umejenga hiyo dhana kwamba umeumizwa. Hakuna anayekuumiza, ila kinachokuumiza …

Epuka Tabia Hii Kwenye Mahusiano Yako

Kiasili kila binadamu anapenda kusifiwa. Kila binadamu anapenda kuonekana anathaminiwa. Kitu ambacho kinavuruga mahusiano yetu na wale tunaohusiana nao ni kukosoa. Kwa mtu yeyote yule unayehusiana naye, ukitaka kuboresha mahusiano yenu, iwe ni ya kazi, biashara, ndoa na nk msifie na usimkosoe. Wapende na wachukulie watu kama walivyo. Tafadhali kazi yako isiwe ya kukosoa bali …

Hujisukumi Kwa Sababu Huna Kitu Hiki

Kwa sababu huna kitu kinachokusukuma kufanya. Watu wengi wanaondoa uvivu, uzembe kama kuna kitu kinawasukuma ndani yao kufanya. Kama huna sababu inayokusukuma ya nini kujitesa? Ila ukiwa na sababu unakuwa unajisukuma kweli na huoni tena mateso bali unaona mateso ndiyo njia ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Mtu mmoja alikuwa na hali mbaya sana …