Wafanyabiashara wengi huwa wanajua njia pekee ya kukubalika na mteja ni kumsema vibaya mshindani wake.
Baadhi ya wafanyabiashara huwa wanachukiana na hata kujenga uadui kabisa hasa zaidi pale anapoona mteja wake ameenda kupata huduma sehemu nyingine au mshindani wake anauza zaidi au anapata wateja zaidi.
Kumekuwa hakuna habari njema dhidi ya washindani tunaofanya nao biashara moja.
Hatupaswi kuishi kiadui, mteja ni kama ndege anatua mti aupendao kikubwa wewe kama muuzaji ni kutengeneza mazingira ambayo yatamteka mteja na kuwa wako.
Lakini,lipo somo kubwa tunalopaswa kujifunza kuhusu mteja anapokuuliza juu ya mshindani wako unapaswa kufanya nini?
Mteja anapouliza kuhusu mshindani wako, unachopaswa kufanya ni kuwasifia.
Wengi wanaamini kwamba kuwakandia washindani ndiyo njia ya kuwashawishi wateja.
Wateja wanakuamini zaidi pale unaposifia na kusema maneno mazuri kuhusu washindani wako.
Hatua ya kuchukua leo; usiwaseme vibaya washindani wako pale mteja anapouliza kuhusu washindani wako.
Badala ya kuwakandia washindani wako, wasifie kwa yale mazuri wanayofanya na hata mteja atakuamini zaidi kuliko kumsemea mabaya.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog