UCHAMBUZI WA KITABU; Hand Book of Epictetus( Misingi Muhimu Ya Falsafa Ya Ustoa)

Unaendeleaje rafiki? nimekuwa sikushiriki uchambuzi hapa kwa muda mrefu na hii ni baada ya kuamua kubadilisha mfumo kama utakua unapenda uchambuzi wa vitabu basi jiunge moja kwa moja katika mimi ni mshindi utakua unapata uchambuzi wa vitabu kila wiki kujiunga na mimi ni mshindi nimezaliwa kushinda bonyeza hapa na pia jiunge katika mfumo wetu wa kupokea makala kupitia email yako na kujiunga bonyeza hapa pia.  karibu sana sasa uendelee kuonja matunda ya uchambuzi wa vitabu kupitia mimi ni mshindi.

Uchambuzi wa Kitabu; Hand book of Epictetus.
Kimeandikwa na kutafsiriwa na Nicholas White.

Utangulizi;

Falsafa ya ustoa ( stoic philosophy) ilianzishwa na mwanafalsafa Zeno wa cytium. Zeno alizaliwa katika mji wa Cyprus kwenye miaka ya 336 kabla hata ya Yesu kuzaliwa yaani B.C.

Lakini shughuli zake za kifalsafa zilikuwa zinafanyika katika mji wa Athens. Falsafa ya ustoa inazaidi ya miaka 500 ambayo umekuwa ni miongoni mwa falsafa bora sana yenye ushawishi na matunda mazuri ya kiharakati.

Miongoni mwa wanafalsafa wengine wa falsafa hii ya ustoa ni ukiachana na Epictetus mwenyewe pia kuna wengine kama vile Seneca, Cicero na Marcus Aurelius aliyekuwa mtawala wa Roma.

Seneca aliishi maisha yake ya hapa duniani pamoja na kuiishi falsafa hii katika karnr ya 5 kabla ya Yesu kuzaliwa mpaka mwaka 65 baada ya Yesu kuzaliwa ( 5. B.c – AD 65).

Na aliyekuwa mtawala wa Roma enzi hizo mwanafalsafa na mstoa marcus Aurelius yeye alizaliwa mwaka 121 – 180 na hapo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wake wa kuendelea kuvuta pumzi hapa duniani.

Yapo mengi ambayo tunaweza kujifunza kupitia falsafa hii ya ustoa kadiri ya mwanafalsafa Epictetus kupitia kitabu hiki.

Zeno mwanzilishi wa falsafa hii ya ustoa anasema maiha ya binadamu yawe kadiri ya sheria ya asili kwanini? Kwa sababu asili huwa haina madhara.

Epictetus alikuwa ni mtumwa kipindi cha mwanzo kabisa ya maisha yake.

Karibu sana mwanamafanikio, nikushirikishe mambo muhimu niliyojifunza kupitia kitabu hiki ;

1. Kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako na kuna mambo ambayo yako nje ya uwezo wako.
Kwa mfano, mambo ambayo yako nje ya uwezo wetu ni yale ambayo hatuwezi kuyadhibiti au kuyatawala kama vile kuzuia mtu asiumwe, asife au kuzuia foleni nk.
Na vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu ni kama vile kudhibiti hisia zetu, mawazo yetu kwa sababu tunauwezo wa kutawala na kudhibiti hisia zetu. Kwahiyo, ukishajua jua hivi na kujijengea falsafa hii kwenye akili yako mambo yanapotokea wala hutakua na wasiwasi nayo kwa sababu utajua kuna yale ambayo unaweza kuyadhibiti na yale ambayo huwezi.

2. Kuwa na Uhuru wa asili (nature free ) ni jambo ambalo liko ndani ya uwezo wetu. Kila mtu ana Uhuru wake kwa mfano, Nelson Mandela licha ya kufungwa gerezani kwa miaka 27 lakini bado alikuwa na Uhuru wake wa kutimiza ndoto yake ya kuwa raisi, Seneca naye alikuwa gerezani lakini bado alikuwa ana Uhuru wake wa kufanya kile anachopenda kama vile yeye alikuwa anapenda kuandika. Hakuna anayeweza kukunyang’anya ule Uhuru wako wa asili wa kufanya kile unachopenda kufanya ndani yako hata uwe wapi hata uwe gerezani.

3. Kama umeshajua kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako huwezi tena kujiingiza katika upinzani wa akili yako badala yake unatakiwa uwe na utulivu wa akili. Usijisumbue kwa mambo ambayo yako nje ya uwezo wako. Kufanya hivyo ni kutaka kubadili asili na kujipatia msongo wa mawazo.

SOMA;Hii Ndio Faida Ya Kusikiliza Sauti Yako Ya Ndani Na Kuacha Kusikiliza Sauti Za Nje

4. Kama una mbusu mtoto au mke wako sema una mbusu binadamu hata siku wakifanya hutoumia sana na kupoteza utulivu wako wa akili. Wapende wale ambao wako karibu na wewe na waambie unawapenda kweli, wa busu kweli hata siku wakiondoka hutoumia sana kwa sababu uliwatumia vizuri na kutambua thamani yao wakati wako hai.
Changamoto ya leo ni kwamba watu hawavipi thamani vile ambavyo wanavyo sasa, pale inapotokea vimeondoka anakuja kujilaumu na maneno mengi ya laiti ningelijua.

5. Unapotaka kufanya kitu jiulize kwa kujikumbusha kwanza unataka kufanya nini. Kwa kujikumbusha unataka kufanya nini unakuwa unaiandaa akili yako dhidi ya kile unachokwenda kufanya. Kwa mfano, kama unaenda bafuni unajiandaa kabisa kiakili nini unakwenda kufanya bafuni.
Ni muhimu kujiandaa kukabiliana na kila hali kiakili kwa sababu kuna watu wanaoiba, wanaotukana hivyo ni muhimu kujianda kadiri ya tukio husika.

6. Kinachowaumiza watu na kuwafanya wajisikie vibaya ni ile tafsiri au hukumu anayotoa juu ya kile kitu. Kwa mfano, mtu akikutukana vile unavyoanza kutafsiri kwanini anitukane, amenichukuliaje, au ameniona kwa sababu mimi siyo hivi vile au niko hivi. Sasa haya yote ndiyo yanayozaa maumivu ndani mwetu na kuibua hasira lakini tukichukulia kawaida hakuna baya litakalotokea.

7. Pale tunapokuwa hatuko katika utulivu wa akili, tunamsongo wa mawazo tuache kuwalaumu wengine ndiyo wamesababisha sisi tuwe hivyo bali tujilaumu sisi wenyewe ndiyo chanzo.

8. Mtu aliyestarabika hamlaumu mtu yeyote siyo yeye mwenyewe wala mtu mwingine. Watu wasiyo elimika ndiyo wanajilaumu na kuwalalamikia wengine wamemfanyia ubaya.

9. Usifurahie ustaa, ubora, ukuu au hadhi yoyote ambayo siyo yako. Furahia kile kizuri ambacho ni cha kwako. Furahia mwonekano wako na mvuto wako wa asili.

10. Usitafute au kulazimisha mambo au matukio yatokee kama vile unavyotaka wewe badala yake yaache mambo yatokee kama vile yanavyotaka kutokea na maisha yako yataenda vizuri.

11. Ugonjwa huwa unaingilia au kuathiri mwili tu lakini siyo wewe yaani ule utu wako. Ni kitu ambacho huwa kinatokea pasipo kuchagua wewe hivyo na mtazamo huu utaona kila kitu huingiliana na kitu kingine na wala siyo wewe na utu wako utabaki pale pale.

12. Unapokuwa na familia, watoto, mke, mume usiende mbali nao,nenda mbalo lakini hakikisha uko nao bega kwa bega kwenye kile unachofanya ili msije mkaachana nyuma kwenye kile mlichokuwa mnafanya.

13. Ukifikiri na kuchukuliwa kuwa kilicho chako na kisicho chako vyote si vyako basi hakuna kitakachoweza kukuangusha au kukusudia. Hutamlaumu mtu hata hata kuwa na maadui kwa sababu hutamdhuru yeyote.

14. Chochote kinachotokea kwako jiulize je unauwezo wa kukabiliana nacho. Kama huwezi achana nacho.

15. Kamwe usiseme umepoteza bali sema nimerudisha. Ardhi yako imechukuliwa sema umerudisha, mtoto au mke wako amekufa hujapoteza bali umewarudisha kwa sababu chochote ambacho unacho sasa umeazimwa kwa muda.

16. Weka umakini kwenye kile unachofanya na achana na vingine.

17. Kama unataka kufanya maendeleo acha watu wakuone mjinga, usichanganyikiwe kuhusiana na mambo ya nje, endelea kufanya mpaka siku watashangaa umefanya makubwa na hawatakusumbua.

18. Ni ujinga kutaka watoto au mke wako na marafiki wako kuishi milele. Ni kulazimisha mambo ya nje ya uwezo wako kuwa ndani ya uwezo wako.

19. Ukimkuta mtu amehuzunika juu ya kuondokewa na na mtu wake wa Karibu au amepoteza mali yake, mpe pole, mtie moyo kwa huzuni yake lakini usikubali akuingize kwenye matatizo au huzuni zake kwani atakuharibia utulivu wako wa akili.

20. Kumbuka wewe ndiyo mhusika mkuu wa filamu ya maisha yako. Wewe ndiyo mwandishi au mchezaji wa filamu hiyo unayetaka iweje. Wewe ndiyo wa kuirefusha au kuifanya iwe ndefu.uamuzi ni wako kuvaa uhusika unaotaka kuucheza.

21. Usikubali furaha yako itawaliwe na vitu. Siku ambayo vitu hivyo vitaondoka utapata sana shida na kuumia.

22. Kumbuka kile kinachokuumiza pale mtu anapokutukana siyo tusi bali tafsiri yako juu ya lile tusi ndicho kinakufanya uumie. Chelewa kutafsiri ja utajitawala mwenyewe.

23. Kama umechagua kuishi falsafa, jiandae kuhdhihakiwa. Kila mtu atasema lake maoni ya watu yatakuwa mengi. Lakini mwishoni watakuja kuvutiwa na wewe na kuomba uwasaidie namna falsafa yako itakavyoweza kuwasaidia kama wewe na kuwa bora.

24. Ni rahisi kuyaona mambo yakitokea kwa wengine lakini siku yakija kukutokea kwako utaona ni magumu. Kwa mfano mtu akiuguliwa unaweza ukaona ni kawaida tu, au mtu akifiwa unaweza ukaona ni kawaida ila siku yakikufikia na wewe utaona uzito wake.
Ni rahisi kuyaona kwa wengine lakini usiombe yakufikie kwako.

25. Kama ikitokea unaanza kufanya mambo ili kumfurahisha mtu au watu basi, ni dhahiri kabisa umepoteza mpango ja maisha yako.

26. Ukiona mambo yanaenda vizuri furahia kwa uzuri uliopata na kama no mabaya usiwe na hasira usikasirike kwa sababu hujapata kile unachotaka.

27. Usijisunbue kupata haki sawa kwenye kitu ambacho wala hujashiriki kukitafuta.

30. Usitake heshima ambayo bado hujalipia gharama yake. Ukiona hata mwenzako anaheshimiwa jua kabisa kuna gharama amelipia hivyo na wewe kuwa tayari kulipa ili upate kile unachotaka.

31. Kwa asili huwa hakuna baya linalotokea duniani.

32. Kwa kila tendo jifunze nini kinapelekea kutokea kwa hicho kitu. Kwa mfano, unataka kushinda katika mashindano ya olimpiki jifunze na zingatia mwongozo wa nini kinapelekea mtu kupata ushindi.

33. Kuwa na nidhamu, zingatia mlo kamili na epuka vitu vya sukari.

34. Hakuna mtu anayekuumiza labda mwenyewe upende kuumizwa. Kila kitu kipo ndani ya uamuzi wako ni wewe ndiyo unaruhusu kuumizwa au la.

35. Kila mtu yuko sahihi kadiri ya mtazamo wa imani yake. Hivyo ukimweshimu mtu kadiri ya imani yake naye atakuheshimu pia.

36. Jijengee tabia ambayo utaifuata ukiwa wewe mwenyewe na ukiwa na watu. Huu ndiyo ule uadilifu mwenyewe sasa yaani unaishi kile unachosema uwe gizani au kwenye mwanga uwe peke yako au kwenye watu.

37. Kuwa kimya muda mwingi, ongea pale unapotakiwa kuongea tu tena kwa maneno machache

38. Kwenye vile vitu vinavyotokea tu na hususani kuhusiana na watu ongea bila kulaumu, kusifia au kulinganisha. Bali chepuka kwa kujenga hoja zako mwenyewe.

39. Epuka kufanya kiapo isipokuwa sehemu au mazingira yanayoruhusu kiapo.

40. Usicheke sana kwenye mambo makubwa.

41. Ikitokea uko miongoni mwa wageni usiongee.

42. Kuwa hivyo ulivyo na usijiingize kwenye mapenzi kabla ya ndoa. Na kama uko katika ndoa fanya yale tu unayoruhusiwa kufanya kwenye ndoa.

43. Mtu akija kukuripotia kuwa fulani na fulani wamesema mabaya juu yako wala usimjibu. Lakini kutomjibu tayari umeshamjibu.

44. Unapokwenda kumuona mtu nyumbani kwake jiweke mawili kumpata au kumkosa. Ukienda na ukimkosa hutoumia sana kwani ulishjiandaa kiakili.

45. Kama unajua umefanya kitu bora kwanini sasa unahofia wale watakaokuja kukukosoa umefanya vibaya.

SOMA; Uchambuzi Wa Kitabu; Mambo Muhimu Niliyojifunza Kutoka Katika Kitabu Cha Princiles(Misingi 210 Katika Maisha Na Kazi)

46. Ukimwona mtu anakufanyia ubaya, anakuongelea mabaya, anakuumiza kumbuka kuwa imani yake inamtuma kufanya hivyo kwa sababu na yeye alifanyiwa au anafanyiwa hivyo.
Hivyo basi, anaona akikufanyia hivyo ni sehemu ya maisha yake na anaona kawaida tu kwake.

47. Kila kitu kinaupacha wake, kuna mazuri na mabaya yake, kuna faida na hasara zake.

48. Usiseme kuwa wewe ni mwanafalsafa. Na usiongee kwa wale ambao siyo wanafalsafa. Bali unatakiwa kuishi misingi ya falsafa lakini siyo kujitangaza kwa watu. Watu watakujua kwa matendo yako kwa mfano, katika chakula usimfundishe mtu jinsi ya kula bali wewe kula vile ambavyo mtu anatakiwa kula.

50. Usijikweze au kujitangaza kuwa mimi ni tajiri kuliko wewe, mimi ni bora kuliko wewe, mimi ninamali kuliko wewe, mimi ninazungumza vizuri kuliko wewe na tabwe nyingine nyingi za kutaka kujinesha.
Unatakiwa usijionyeshe kama wewe una mali au una uwezo fulani.

51. Usihukumu.

52. Usifanye maonyesho yaani show off. Kama umefanya kitu huna haja ya kumwambia kila mtu.

53. Kama unataka kujifundisha wewe mwenyewe kupitia magumu au kujipa nidhamu ya kitu fulani fanya hivyo kwa ajili yako na si kwa ajili ya wengine au watu wa nje.

55. Jifunze asili na uifuate asili.

Haya ni machache kati ya mengi niliyojifunza kupitia kitabu hiki cha falsafa ya ustoa.

Natumaini kila mmoja wetu atakwenda kuiishi falsafa hii katika maisha yake ya kila siku. Kuishi falsafa hii haingiliani na imani yako ya kidini wala kupingana.

MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana 

Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
07171101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com/ kessydeo@mtaalamu.net
http://www.mtaalamu.net/kessydeo
Asante sana.

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

  1. Unknown's avatar

2 Comments

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started