Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Natumaini uko vizuri na pole kwa changamoto mbalimbali unazopitia na kumbuka kuwa changamoto ndiyo zitakuimarisha.
Rafiki leo ninakwenda kukushirikisha nini maana ya kuongea lugha yako, hivi karibuni nimetoa kitabu kiitwacho Ongea Lugha yako ni kitabu kizuri na cha aina yake hivyo wewe kama rafiki yangu nakualika sana chukua hatua ukisome.

Inawezekana hapo ulipo unajiuliza hivi kwani Deo anasema niongee lugha yangu kwani mimi siongei lugha yangu? Nidyo unaongea lugha yako lakini siyo lugha hii ninayomaanisha ambayo unatumia kuwasilina na watu wengine. Kwanza kabisa jina la kitabu cha Ongea Lugha yako ni jina lililokaa kifashii zaidi ambalo linasadifu mambo mazuri ninayokwenda kukushirikisha hapa.
Kwanza kabisa ukiangalia ganda la nje la kitabu kwa kuchambua vizuri kifasihi unaweza kupata picha au maana halisi iliyokusudiwa na mwandishi. Jina la kitabu na ganda la nje ya kitabu kinasadifu maana halisi ya mwandishi alichokusudia kwa kuichambua vizuri kifashii zaidi. Ganda la nje la kitabu linaonesha watu wa tatu, wawili wakiwa wamekaa wanafanya kazi na mmoja anashangaa wenzake wakifanya kazi. Kuongea lugha yako ni kusikiliza sauti yako ya ndani inataka nini, na habari njema ni kwamba sauti yako ya ndani ndiyo mafanikio yako. Kwahiyo, mtu mmoja hajajua anawaangalia wenzake wakiongea lugha zao hivyo yeye amesimama akiongea lugha za watu wengine.
Na habari mbaya ni kwamba huwezi kuongea lugha yako kama hujasikiliza sauti yako ya ndani. Huwezi kujua kusudi la maisha yako hapa duniani kama hujasikiliza sauti yako ya ndani inataka nini au umeitwa wapi. Kuongea lugha yako ni kusikiliza sauti ya ndani inataka nini, kuongea luhga yako ni kufanya kile unachokipenda na kuongea lugha yako ni kujua kusudi lako hapa duniani kwa sababu hujazaliwa bure tu yaani kwa bahati mbaya bali umezaliwa kwa makusudi. Watu ambao bado hawajasiliza sauti zao za ndani huwa wanaendelea kuteseka kwa sababu kuna kitu kinawatafuna ndani yao na mpaka ukisiliza sauti yako ya ndani ndiyo nafsi yako itatulia itaacha kukusumbua.
SOMA; Ifahamu Nguvu Ya Kusikiliza Sauti Yako Ya Ndani
Inawezekana kazi unayoifanya siyo lugha yako, inawezekana umeajiriwa kumbe kuajiriwa siyo lugha yako. Watu wengi ndoto zao zinazimika kama mshumaa kwenye upepo kwa sababu ya kutosikiliza sauti zao za ndani zinawaambia nini sasa ukishasikiliza sauti yako ya ndani ndiyo mwanzo sasa wa kuongea lugha yako. kumekuwa na malalamiko ya watu wengi katika kazi wanazofanya kwa sababu watu hao wanaongea lugha ambazo siyo zao laiti kama kila mtu angesikiliza sauti yake ya ndani basi leo dunia ingekuwa sehemu salama sana.
Watu wengi wanaongea lugha za wengine na siyo lugha zao. Wewe kama umeajiriwa unaongea lugha ya mwajiri wako kwa sababu yeye aliamua kusikiliza sauti yake ya ndani na kuifanyia kazi mpaka leo hii wewe unanufaika. Matunda ya vitu vyote unavyoviona hapa duniani au watu wote wenye mafanikio makubwa kabisa hapa duniani ni wale walioamua kusikiliza sauti zao za ndani na kujua Mungu amewaita wapi hivyo na kuchagua hiyo kama lugha yao. Ukiona unapata shida katika kazi yako na huipendi hiyo siyo lugha yako unapaswa kukaa chini na kusikiliza lugha yako na kuongea lugha yako.
Rafiki nakualika nunua na usome kitabu cha ongea lugha yako ambacho utajifunza mambo mengi ukiachana na hili la kujua kusudi la maisha yako. kitabu kimesheni kila kitu katika maisha ya mwanadamu na nimechambua kwa mifano ya vitabu mbalimbali vya rejea ambapo ukisoma utafurahi sana na wewe utaanza kuonge lugha yako ndiyo maana kina kurasa 298 na kuongea lugha ya mwengine ni utumwa rafiki yangu. Kitabu kinapatikana kwa shilingi elfu tano tu 5000/= na kipo katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy. Jinsi ya kukipata tuma pesa kwa mpesa , tigo pesa na eatel money kupitia moja ya namba hizi 0717101505/0767101504. Halafu baada ya kutuma tuma email yako nitakutumia kitabu au tuma namba yako ya wasapu au telegram hii ni kwa yule ambaye hana email na anapenda kukipata kitabu hiki.
Nakutakia kila la heri rafiki yangu.
Ni mimi rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504
Asante sana.
Leave a comment