Waondoe Watu Hawa Kwenye Orodha Yako

Rafiki, Dunia inaendeshwa kwa misingi ya nipe nikupe, nikune nikukune. Hivyo basi, wewe unataka kupata kitu fulani, hakikisha na wewe unatoa kitu fulani ili ukipate. Usitegemee kupokea kama hutoi. Kuna aina ya watu ambao una husiana nao, wako wako kama kupe tu. Ni watu ambao wanapenda kupokea kutoka kwako lakini ni wagumu kutoa. Waondoe wote …

Kama Inafanya Kazi

Kama inafanya kazi, rudia tena kuifanyia kazi.Ndiyo, rudia tena kuifanyia kazi. Kama umekutana na kitu chochote kile ambacho kinafanya kazi rudia tena kwa kufanya zaidi ili upate matokeo. Tunakuwa na mbinu mbalimbali za kutusaidia katika maisha yetu, pale unapokutana na kitu ambacho kinafanya kazi, shukuru na endelea kukifanyia kazi zaidi. Kwa mfano, wewe kama ni …

Jua Hiki Ili Usipigwe Hela

Rafiki, Iko hivi, udhaifu wako ndiyo mtaji kwa wengine.Udhaifu wako ndiyo unawapa watu fedha. Na katika hali ya kawaida, kila mtu ana udhaifu wake.Na hakuna kitu kizuri kama kujua udhaifu wako uko wapi ili uweze kujidhibiti au kukabiliana nao. Jua udhaifu wako uko wapi ili watu wasitumie udhaifu wako kupiga hela. Unachopaswa kujua ni wapi …

Kama Unajua Unapokwenda, Dunia Itakupisha

Rafiki, Kabla hujaanza safari ya mafanikio makubwa, unaweza kuona mambo ni rahisi. Lakini, mambo siyo rahisi kama unavyofikiria. Pals unapopanga kufanikiwa na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako, ndipo vikwazo vya kila aina vinaibuka. Na dunia inafanya kwa nini? Dunia inafanya hivyo kwa sababu ni njia ya kukupima kama kweli umejitoa kufanikiwa au unazingua tu. …

Napata Pesa Lakini Sijui Hata Zinaenda Wapi

Moja ya kauli mbiu ya watu wengi kwenye upande wa fedha ni kwamba, wanapata fedha lakini hawajui zinaenda wapi. Rafiki, kitu chochote ambacho hakipimwi, huwezi kujua kama kinakua au kinakufa. Moja ya changamoto ya watu wengi kwenye fedha ni kutokufanya tathmini za fedha zao.Hawajui fedha zao zinaenda wapi. Ukitaka kujua fedha zako zinaenda wapi, fuatilia …

Hiki Ndiyo Kitu Tulichofundishwa Tu

Katika jamii zetu, imani za kidini ambazo tunaziamini huwa tunafundishwa sana kuomba.Ni vizuri kuomba lakini huwezi kufanikiwa kwa kuishia kuomba tu. Watu wengi sana wanaomba, kitu ambacho ni kizuri kwa sababu huwezi kupata bila kuomba. Hata ukiangalia kwa sasa, watu wanaomba sana kuliko kutafuta.Maandiko yanasema, ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata. Kuomba ni kitu kingine …

Sipendezwi Na Hii Hali

Mtu mmoja alimtembelea mzee mmoja nyumbani kwake.Alimkuta yule mzee anasoma gazeti huku mbwa wake pembeni akiwa analia sana kwa kupiga sauti. Yule mgeni, akamuuliza yule mzee kwa nini mbwa wako analia hivi?Akamjibu kuwa, mbwa wake amekalia msumari ndiyo maana analia. Akamjibu, kwa nini huendi kumtoa? Akamjibu, kama angekuwa anaumia angetoka, hajaumia ndiyo maana yupo pale. …

Makasiriko Ya Nini ?

Rafiki, Kila mtu ana haki ya kutumia kile alichonacho vile anavyotaka ili mradi tu asivunje sheria za asili, nchi na kanuni za maadili. Pale mtu anapokuwa anaishi maisha anayoyataka, hutakiwi kuwa na makasiriko yoyote yale juu yake. Huna haja ya kuwazuia watu wasitumie vile walivyonavyo kwa jinsi wanavyotaka. Wajibu wako namba moja ni kuishi maisha …

Umekamilisha Nini ?

Kwa zama tunazoishi sasa, watu wengi wamekuwa hawakamilishi mambo.Watu wengi wanaanza vitu, lakini kuvikamilisha ndiyo changamoto kubwa. Tumekuwa na ndoto nyingi ambazo mpaka leo hii bado hazijaweza kufanyiwa kazi.Jiulize tu wewe mwenyewe ni mambo mangapi uliyapanga kufanya jana na ni mamgi umefanikiwa kuyakamilisha? Ushindi wowote kwenye maisha upo kwenye ukamilishaji.Kama unataka kupata ushindi, kamilisha kile …

Usipoteze Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Rafiki,Watu wakikupa heshima fulani,Watu wakikupa imani fulani juu yako, Watu wakikuamini na kutarajia kitu fulani kutoka kwako, tafadhali usiwaangushe. Usipoteze kile ambacho tayari watu wanaamini wakija kwako watakupata.Kama unategemewa kwa kitu fulani, usiache kutekeleza hilo kwa uaminifu mkubwa. Ishi katika falsafa ya uaminifu, ahidi na tekeleza. Watu wanakuamini kwa kuzalisha kitu fulani, basi hakikisha wakija, …

Design a site like this with WordPress.com
Get started