Rafiki yangu nikupendaye, Njia ya kujenga uaminifu zaidi kwa watu ni kwa njia ya kutimiza ahadi. Unapoahidi kitu, timiza kama ulivyoahidi na siyo kuja na visingizio. Kwa kila ahadi unayotimiza,unajenga uaminifu zaidi kwa watu. Siyo kujenga uaminifu, lakini pia kuaminika, kuheshimika kiasi cha kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wale unaohusiana nao. Timiza ahadi unazojiwekea …
Fanya Kilicho Sahihi
Rafiki Kwenye maisha ukitafuta umaarufu bila kutoa thamani utaupata kweli lakini utaupoteza muda siyo mrefu. Njia nzuri ya kupata umaarufu ni kutoa thamani kupitia kile ulichochagua kufanya. Unaweza ukashangaa wale ambao wanafanya vitu visivyo sahihi na kupata umaarufu wa ghafla kama vile tunavyoona kwenye mitandao ya kijamii yanayoendelea. Usije ukashawishika hata siku moja kufanya vitu …
Kwani Watu Wanasemaje?
Rafiki yangu nikupendaye, Kwenye haya maisha jitahidi sana usiwe mjinga. Kwa sababu watu wanaendesha maisha yao kwa sababu ya ujinga fulani ulikuwa nao. Sehemu yoyote ukienda, kama hakuna mtu wa KUTAPELIWA, basi wewe ndiyo utatapeliwa. Unapaswa kuwa makini sana. Ni aibu kwa mtu makini ambaye unapata maarifa mazuri na chanya halafu ukaendelea kuwa kama wengine. …
Jinsi Ya Kupata Fedha Za Kuwekeza
Rafiki, Kama unataka kwenda kununua kitu fulani huwa unajua kabisa bei yake ni kiasi fulani. Unapoenda kununua kitu hicho, hakikisha unaomba punguzo la bei. Dai punguzo la kitu chochote kile unachotaka kununua na ukipata hilo punguzo kile kiasi unachopata kwenye punguzo, nenda kakiwekeze. Kwa mfano, ulijiandaa kwenda kununua simu ya laki mbili na nusu na …
Haya Ndiyo Mambo yanayozalisha matokeo makubwa
Mwandishi Robin Sharma anatukumbusha msingi mkuu wa ushujaa ambao amekuwa anafundisha kwa muda mrefu na kutaka kila mtu aukariri; hatua ndogo ndogo zinazochukuliwa kwa msimamo kila siku bila kuachwa ndiyo zinazozalisha matokeo makubwa sana. Kumbe basi, mambo yanayozalisha matokeo makubwa ni yale mambo madogo madogo ambayo tunayadharau. Unataka kupata mafanikio makubwa, ila jua hayatakuja mara …
Continue reading "Haya Ndiyo Mambo yanayozalisha matokeo makubwa"
Kufika Muda Kamili Ni Kuchelewa
Kama umepanga kwenda sehemu yoyote ile, kufika muda kamili ni kuchelewa. Ili uweze kujenga ushawishi kwa watu na kuaminika, jitahidi kufika sehemu kabla ya muda mliopanga. Fika nusu saa kabla au dakika 15 kabla ya kukutana na mtu.Utamaduni wa watu wengi kwa hapa Tanzania ni kuchelewa kufika sehemu husika kwa muda uliopangwa. Wewe usiwe hivyo. …
Kiburi Cha Mafanikio
Watu wengi wakifanikiwa huwa wanakuwa na kiburi cha mafanikio na kusahau mchango wa bahati kwenye mafanikio yao. Tambua mchango wa bahati. Ukiwa mnyenyekevu na kutambua mchango wa bahati, kiburi cha mafanikio hakitakuangusha. Mafanikio huwa yanadanganya sana na ndiyo maana wengi huanguka vibaya baada ya kufanikiwa. Hiyo inatokana na kiburi ambacho watu wanakipata wanapofanikiwa, kwa kuona …
Pata Ushindi Ndiyo Uamini
Rafiki, Usiamini kitu kwa sababu tu kila mtu anakiamini, pata ushahidi ndiyo uamini.Siyo kila kitu ambacho watu wengi wanakiamini ndiyo sahihi. Kuwa mtu wa kuthibitisha wewe mwenyewe na siyo kutegemea watu wengi. Ishi kwa falsafa hii, amini lakini, thibitisha. Kuthibitisha ndiyo kupata ushindi. Kama inafanya kazi au haifanyi utajua kwa kuthibitisha. Waache watu waamini vile …
Kukubali Majukumu Yako
Rafiki, Kuna watu wa aina mbili hapa duniani, wapo watu ambao wanayakubali majukumu yao na kuchukua hatua. Na wapo watu ambao wanayakataa kabisa majukumu yao na kutafuta sababu kwa nini hawawezi kuchukua hatua.Kumbuka, ni rahisi kukimbia majukumu yako lakini ni ngumu kukimbia matokeo yake. Mafanikio hayajawahi kwenda kwa mtu yeyote ambaye siyo wa kukubali majukumu. …
Kuwa Imara Zaidi
Rafiki, Pale yasiyotegemewa yanapotokea kwa watu, huwa wengine wanavurugwa kabisa au wengine wanaimarika kabisa. Mambo usiyoyategemea yakitokea, yanakuwa yanawaacha watu katika matokeo haya matatu. Moja, kuvunjika moyo na kukata tamaa kabisa. Hapa mtu anaanguka kabisa kiasi cha kushindwa kurudi tena kwenye mapambano. Mbili, ni kuwa mstahimilivu. Hapa mtu anarudi tena kwenye mapambano licha ya kuwa …