Napata Pesa Lakini Sijui Hata Zinaenda Wapi

Moja ya kauli mbiu ya watu wengi kwenye upande wa fedha ni kwamba, wanapata fedha lakini hawajui zinaenda wapi. Rafiki, kitu chochote ambacho hakipimwi, huwezi kujua kama kinakua au kinakufa. Moja ya changamoto ya watu wengi kwenye fedha ni kutokufanya tathmini za fedha zao.Hawajui fedha zao zinaenda wapi. Ukitaka kujua fedha zako zinaenda wapi, fuatilia …

Hiki Ndiyo Kitu Tulichofundishwa Tu

Katika jamii zetu, imani za kidini ambazo tunaziamini huwa tunafundishwa sana kuomba.Ni vizuri kuomba lakini huwezi kufanikiwa kwa kuishia kuomba tu. Watu wengi sana wanaomba, kitu ambacho ni kizuri kwa sababu huwezi kupata bila kuomba. Hata ukiangalia kwa sasa, watu wanaomba sana kuliko kutafuta.Maandiko yanasema, ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata. Kuomba ni kitu kingine …

Sipendezwi Na Hii Hali

Mtu mmoja alimtembelea mzee mmoja nyumbani kwake.Alimkuta yule mzee anasoma gazeti huku mbwa wake pembeni akiwa analia sana kwa kupiga sauti. Yule mgeni, akamuuliza yule mzee kwa nini mbwa wako analia hivi?Akamjibu kuwa, mbwa wake amekalia msumari ndiyo maana analia. Akamjibu, kwa nini huendi kumtoa? Akamjibu, kama angekuwa anaumia angetoka, hajaumia ndiyo maana yupo pale. …

Makasiriko Ya Nini ?

Rafiki, Kila mtu ana haki ya kutumia kile alichonacho vile anavyotaka ili mradi tu asivunje sheria za asili, nchi na kanuni za maadili. Pale mtu anapokuwa anaishi maisha anayoyataka, hutakiwi kuwa na makasiriko yoyote yale juu yake. Huna haja ya kuwazuia watu wasitumie vile walivyonavyo kwa jinsi wanavyotaka. Wajibu wako namba moja ni kuishi maisha …

Umekamilisha Nini ?

Kwa zama tunazoishi sasa, watu wengi wamekuwa hawakamilishi mambo.Watu wengi wanaanza vitu, lakini kuvikamilisha ndiyo changamoto kubwa. Tumekuwa na ndoto nyingi ambazo mpaka leo hii bado hazijaweza kufanyiwa kazi.Jiulize tu wewe mwenyewe ni mambo mangapi uliyapanga kufanya jana na ni mamgi umefanikiwa kuyakamilisha? Ushindi wowote kwenye maisha upo kwenye ukamilishaji.Kama unataka kupata ushindi, kamilisha kile …

Usipoteze Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Rafiki,Watu wakikupa heshima fulani,Watu wakikupa imani fulani juu yako, Watu wakikuamini na kutarajia kitu fulani kutoka kwako, tafadhali usiwaangushe. Usipoteze kile ambacho tayari watu wanaamini wakija kwako watakupata.Kama unategemewa kwa kitu fulani, usiache kutekeleza hilo kwa uaminifu mkubwa. Ishi katika falsafa ya uaminifu, ahidi na tekeleza. Watu wanakuamini kwa kuzalisha kitu fulani, basi hakikisha wakija, …

Wajali Watu Hawa Hapa

Rafiki, Wote tunajua kwamba maisha yetu yanaendeshwa na gharama.Kila siku gharama za maisha ni nyingi na bila kuwa na fedha ni ngumu kuendesha maisha. Tukiachana na pumzi tunayovuta bure kabisa, vitu vingine vyote vinahitaji kulipiwa bili. Hata ukiumwa na ukiwa huna hela ndiyo hatari zaidi kwa sababu hii pumzi ya bure unayopata ukiumwa na kushindwa …

Jinsi Ubora Unavyopatikana

Rafiki, Ubora siku zote hauji kwa kuweka mikono mifukoni.Ubora hauji kwa kusema, bali ubora unapatikana kwa njia ya kufanya. Huwezi kuwa bora kama hufanyi, huwezi kuwa bora kwa kujifunza na kupanga pekee. Hata kama ungejifunza na kujua kiasi gani, unapoanza kufanya kwa vitendo lazima utakosea. Lakini, kadiri unavyoendelea kufanya, ndivyo unavyozidi kuwa bora zaidi na …

Kichocheo Cha Kukupa Hamasa Ya Kufanya Kila Siku

Rafiki,Sisi binadamu kwa asili ni wavivu. Na kitu ambacho kinatupa uvivu ni kwa sababu ya kukosa msukumo wa kufanya. Yaani ukikosa hamasa na shauku ya kukusukuma kuamka mapema asubuhi ni ngumu kuamka.Safari ya mafanikio ni ngumu, bila kuwa na kitu kinachokusukuma, ni ngumu kutoboa. Leo ninakwenda kukushirikisha kitu ambacho kitakupa hamasa ya kufanya kila siku. …

Usijisahau Wewe Mwenyewe

Rafiki, Watu wengi wanawekeza kazi kwenye kile wanachotaka. Kitu ambacho ni kizuri sana. Lakini, watu hao licha ya kufanya kazi, huwa wanajisahau wao wenyewe. Mtu anafanya kazi lakini anashindwa kujipenda yeye mwenyewe. Yuko radhi awafanyie watu wengine na kisha kujisahau yeye mwenyewe. Hali ya kujisahau inapelekea mtu hata kukosa hamasa ya kuendelea kupambana.Wewe ndiyo mtu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started