Kuhakikisha Siyo Ujinga

Amini lakini thibitisha. Ndiyo kauli mbiu unayopaswa kuwa nayo mara zote kwenye maisha yako. Kuhakikisha siyo ujinga bali ni ujanja. Umakini wa mtu unapimwa kwenye kuhakikisha jambo alilofanya kama ni sahihi au siyo sahihi. Ukiandika ujumbe, kabla hujatuma kwa mtu, hakikisha kwanza, hakiki vizuri kile ulichoandika na namna nzuri ya kuhakikisha ni kwa kusoma kwa …

Usiangamie Zama Hizi

Rafiki, Hakuna zama za ushindi kama zama hizi. Hakuna zama ambazo zinaweza kukuwezesha wewe kuwa yule unayemtaka kama zama hizi. Zama hizi ukisema umeshindwa, umeshindwa mwenyewe kwa sababu hutaki tu. Lakini, kwa mtu ambaye anataka kitu, kuna kila sababu za kumwezesha kushinda. Kwenye kitabu cha dini, wanasema watu wangu, wanaangamia kwa kukosa maarifa. Usikubali kuangamia …

Kama Haijakulipa LeoItakulipa Lini?

Rafiki yangu nikupendaye, Kama kuna kitu chochote unafanya, usiwe na wasiwasi kuna siku kitakuja kukulipa. Watu huwa wanakata tamaa mapema pale wanapoona, uwekezaji waliouweka haujaweza kuwalipa. Kama haijakulipa leo, itakulipa kesho. Uwekezaji wowote ule unaofanya kwenye maisha yako, utakulipa, wala usiwe na wasiwasi.Uwekezaji ni suala la muda. Hivyo kile unachofanya au ulichowekeza kitakuja kukulipa tu. …

Usiamini sana kile ambacho Hakipo Mkononi mwako

Mara zote kuwa na imani na kile ambacho tayari unacho. Usiweke mategemeo sana kwa vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako. Kwa mfano, usiweke mategemeo kwa mtu ambaye unamdai. Mtu akikuambia kesho atakuletea fedha, hata usiiweke akilini na kuipangia bajeti. Mara zote pangia bajeti kile ambacho tayari umekishika mkononi mwako. Usitegemee yajayo, tumia kwa uangalifu …

Maamuzi Yoyote Yana Gharama

Rafiki, Kama huendi mbele maana yake unarudi nyuma. Na kama hurudi nyuma basi unaenda mbele.Hakuna kusimama, ni aidha unaenda mbele au unarudi nyuma. Uko hapo ulipo sasa kwa sababu ya maamuzi uliyofanya huko nyuma. Hivyo basi, kwa maamuzi yoyote utakayofanya au uliyowahi kufanya lazima yana gharama ndani yake. Hakuna maamuzi yoyote yale yawe ni mazuri …

Mfahamu Mtu Ambaye Hana Changamoto Duniani

Rafiki yangu nikupendaye, Wakati unapitia changamoto fulani fulani kwenye maisha yako, unaweza kuona kama vile dunia ina kisirani na wewe.Huku ukiwaangalia wengine jinsi walivyo kwa nje, unaweza kusema kama wao hawana changamoto ila wewe tu ndiyo dunia inakuandama. Lakini, ukija katika uhalisia, hakuna mtu ambaye hana changamoto hapa duniani.Kila mmoja wetu ana changamoto fulani anayopitia …

Epuka Mambo Haya

Rafiki, Kuna mambo mengine yanatokea katika maisha yetu na wasababishaji wakubwa ni sisi wenyewe. Vitu ambavyo unapaswa kuvifanyia kazi mara kwa mara ni ; Uvivu, mara zote epuka uvivu. Uvivu ni mbaya na unaepukwa kwa kufanya kazi. Uzembe, mara zote epuka kuwa mzembe.Uzembe wako binafsi unaleta madhara kwako binafsi lakini pia hata kwa watu wengine …

Kama Umeamka Na Huna Malengo Fanya Hiki Hapa

Rafiki, Kuna msemo mmoja unasema ,Kama umeamka na huna malengo ya siku, rudi kitandani ukalale. Mtu anayejitambua lazima awe ana malengo ya siku. Kabla hajatoka nyumbani kwenda kuwatumikia wengine, lazima kwanza awe ana malengo yake binafsi. Kwa nini ni muhimu kuwa na malengo binafsi? Kwa sababu, malengo binafsi ndiyo ushindi wako wa siku unaopaswa kuupambania.Usipokuwa …

Haraka Ya Kukamilisha Mambo

Rafiki, Kila mmoja huwa ana malengo yake. Na malengo mengine huwa yanachukua muda na mengine hayachukui muda na hii ina tegemea na aina ya malengo husika. Kwenye kukamilisha malengo, watu huwa wanafanya kukamilisha malengo haraka hasa yale yanayohitaji fedha. Pale mtu anapotaka kukamilisha malengo haraka, anajikuta hana hela na mwisho anakimbilia kukopa. Watu wanakuwa wanajiingiza …

Rudi Kazini

Rafiki, Kuna wakati tunafanya vizuri na hata sisi wenyewe tunafurahi kwa kazi nzuri ambayo tumefanya.Siyo tu sisi wenyewe, lakini pia hata wale waliotuzunguka wanapenda kutupongeza kwa yale mazuri tuliyofanya. Ni kitu kizuri kufanya hivyo kwao kama kutimiza wajibu wa kibinadamu. Wakati mwingine sifa zinaweza zikakulewesha na kupata kiburi.Ukajikuta unaanguka chini. Kwa sababu kile kilichokupandisha ndicho …

Design a site like this with WordPress.com
Get started