Kwa Sababu Umeumia, Haimaanishi Maisha Yataendelea Hivyo

Kila mtu kwenye safari ya maisha hupitia vipindi vigumu. Wakati mwingine ni kupoteza kipato, wakati mwingine ni kushindwa kwenye ndoto ulizokuwa unazifuatilia, wakati mwingine ni kusalitiwa na watu uliowaamini, au hata kupoteza wapendwa.Ni kweli—maumivu hayo huuma, huzuni hujaa moyoni na wakati mwingine mtu huanza kuamini kwamba maisha yote ni mateso na hayana tumaini. Lakini kumbuka …

Kwa Nini Aristotle Alikuwa Analala Chini

Kuna methali ya mafanikio isiyoandikwa: Hakuna sumu kali ya mafanikio kama mafanikio yenyewe.Wengi huanguka si kwa sababu hawajui njia ya kufanikisha, bali kwa sababu baada ya kufanikisha hubadili mtindo wao wa maisha. Kabla ya kupata mafanikio, mtu huishi maisha ya kushambulia – anajifunza kwa bidii, anajaribu vitu vipya, anajituma, anavumilia changamoto, na hatimaye hupata matokeo …

Kanuni Rahisi ya Kufanikiwa

Mara nyingi tunadhani mafanikio yanahitaji kanuni ngumu au fomula ya siri. Lakini ukweli ni kwamba, mafanikio makubwa hujengwa juu ya kanuni rahisi zinazotekelezwa kwa ujasiri na kwa uthubutu wa kila siku. Robin Sharma anatufundisha kanuni moja ya pekee aliyojifunza kwa mwanamuziki mashuhuri wa Jazz, Miles Davis. Miles aliwahi kuwaambia wanamuziki wake: “Msicheze muziki ambao tayari …

Mikakati ya Kuishi Maisha Yenye Utajiri na Utimilifu: Sehemu ya 3

Kwenye makala zilizopita tulianza kujifunza kuhusu mikakati inayoweza kukusaidia kuishi maisha yenye maana, mafanikio na furaha ya kweli. Tuliona kuwa kila mtu anaweza kupanga maisha yake kwa makusudi, badala ya kuishi kwa bahati nasibu. Leo tunaendelea na hatua mbili muhimu ambazo zitakusaidia kuendelea kukua na kufanikisha malengo yako. Hadithi ya Wiki Iliyopita Ili ujue unapokwenda, …

Aina Nane za Utajiri: Sehemu ya 2

Kwenye makala iliyopita tulijifunza kuwa utajiri wa kweli haumaanishi fedha peke yake. Tuliona aina mbili za msingi: Ubobezi binafsi na ushujaa pamoja na afya imara na maisha marefu. Leo tunaendelea na aina nyingine mbili ambazo ni muhimu sana kwa kukupa furaha na kukamilisha maisha yako. Familia na Marafiki Mwisho wa safari ya maisha yako, hutajuta …

Aina Nane za Utajiri: Sehemu ya 1

Watu wengi wanaposikia neno “utajiri”, mara moja akili zao huenda kwenye fedha. Wanafikiria kuwa na akaunti kubwa benki au mali nyingi ndio mwisho wa furaha. Lakini ukweli ni kwamba, fedha ni sehemu ndogo tu ya utajiri. Kuna watu wamepata fedha nyingi sana, lakini bado wakaona maisha yao hayajakamilika. Utajiri wa kweli ni mpana zaidi ya …

Tabia 14 za Mabilionea: Sehemu ya 9 & 10

Tayari tumeshajifunza tabia 8 za awali zinazowatofautisha mabilionea na watu wa kawaida. Leo tunaendelea na tabia nyingine mbili zenye nguvu kubwa: ujuzi wa kuzidisha utajiri na kukataa kukaa na watu hasi. Ujuzi wa Kuzidisha Utajiri Wakati watu wengi wanapata fedha na kuzitumia mara moja kwa vitu visivyo na tija, mabilionea wana mtazamo tofauti kabisa. Hawatumii …

Tabia 14 za Mabilionea: Sehemu ya 7 & 8

Katika sehemu zilizopita tumeshaziona tabia sita zinazowatofautisha mabilionea: kujiamini kupitiliza, kuwa na maono makubwa ya kesho bora, kiu ya uasi, udadisi wa utotoni, kutokujali maoni ya wakosoaji, pamoja na msimamo na ung’ang’anizi. Leo tunaendelea na tabia mbili nyingine muhimu zinazowasukuma kwenye viwango vya mafanikio ambavyo wengi hawawezi kufikia. Kupenda Ushindi na Kuwa Bora Zaidi Mabilionea …

Tabia 14 za Mabilionea: Sehemu ya 5 & 6

Katika makala zilizopita tuliona tabia nne muhimu zinazowatofautisha mabilionea na wengine: kujiamini kupitiliza, kuwa na maono makubwa ya kesho bora, kiu ya uasi na udadisi wa utotoni. Leo tunaendelea na tabia mbili nyingine zinazowaweka mbali zaidi. Kutokujali Maoni ya Wakosoaji Watu wengi hutafuta kukubalika na kupendwa na kila mtu. Kwa sababu hiyo, hujaribu kumridhisha kila …

Tabia 14 za Mabilionea: Sehemu ya 3 & 4

Katika makala zilizopita, tuliona tabia mbili za kwanza zinazowatofautisha mabilionea na wengine: kujiamini kupitiliza na kuwa na maono makubwa ya kesho bora. Leo tunaendelea na tabia nyingine mbili muhimu zinazowasukuma kwenye mafanikio makubwa. Kiu Kubwa ya Uasi Mabilionea hawafuati kundi. Hawakubali kubanwa na mazoea au desturi zilizopo, bali wanasimama kwenye kile wanachoamini. Hawafanyi kilichozoeleka, bali …

Design a site like this with WordPress.com
Get started