Jinsi Ya Kuepuka Maumivu Ya Fedha Baada Kupoteza Fedha Zako

Ni kawaida watu kupigwa kwenye suala la fedha. Wale wanaotafuta mafanikio ya haraka kwao kupigwa fedha ni jambo la kawaida sana. Wengi wamelizwa na matapeli kwenye eneo la fedha, wengine wameibiwa na kutapeliwa fedha kwa njia ya simu na nk. Baada ya kutapeliwa fedha huwa tunakua na maumivu makubwa sana. Kama tunavyojua tena kutoa pesa …

Dalili Ya Kwanza Inayoonesha Unafanya Makubwa

Mtu pekee ambaye ameshamaliza changamoto zake hapa duniani ni marehemu tu, lakini kama unaishi bado changamoto zitaendelea kuwa na wewe na zitakoma pale tu mwili ukapojitenganisha na roho. Kiukweli, kila mtu kuna changamoto anayopitia katika maisha yake, hata ukiwaona watu wako kimya, wanafurahia usije ukasema kuwa hawana kitu kinachowasumbua, kila binadamua kiasili kuna kitu kinamsumbua. …

Tulia Na Akili Yako Itakupa Jibu

Imeshawahi kukutokea hali fulani ambayo unajikuta umesahau kabisa kitu unachojua? Unailazimisha akili yako ikupe jibu lakini wala haikupi. Wakati mwingine unaweka kitu mahali halafu unajikuta umesahau wapi ulipoiweka lakini baadaye ukikaa ukitulia unakuja kukumbuka. Mara nyingi akili ikitaharuki inakosa ufanisi wake wa kazi. Akili yako itajibu maswali yote kama utajifunza kutulia na kusubiria jibu aliwahi …

Hawa Ndiyo Watu Wanaojenga Ufalme

Unaposikia neno ufalme unapata picha gani?Na picha uliyopata unafikiri ni nani anayehusika kujenga ufalme? Chochote kile unachotaka kutawala hapa duniani unatakiwa uwe na kitu kimoja ambacho ni nguvu. Ufalme wowote ule unajengwa na watu wenye nguvu kwani kama huna nguvu yoyote ile hakuna atakayeweza kukusikiliza. Nguvu ni nyenzo muhimu sana kwa binadamu. Kama huna nguvu …

Kama Huwezi Kufanya, Chukua Hatua Hii

Siyo lazima kufanya kila kitu, na kitu ambacho kimekushinda hakiwezi kuwashinda watu wote bali kutakuwa na mtu ambaye anaweza kukifanya kitu hiko. Kama huwezi kile ambacho huwezi kufanya kaa pembeni waachie wale wanaoweza kufanya na wewe nenda kafanye kile unachoweza kufanya wala usijibe shida wakati kuna mambo ambayo yako ndani ya uwezo wako. Usiseme kitu …

Huwezi Kuzuia Tukio Lisitokee Bali…

Huwa tunapambana na vitu vingine ambavyo viko nje kabisa ya uwezo wetu. Lakini wengine hatulijui hilo. Sisi binadamu tunao ukomo wa vitu hapa duniani, viko vile ambavyo viko ndani ya uwezo na viko vile ambavyo viko nje ya uwezo wetu. Mtu anayependa kitu fulani kisitokee ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wake, kwa mfano, …

Usibinafsishe Majukumu Yako Ya Kifamilia

Leo asubuhi nilivyoamka nilisoma kitabu cha philosophy of happiness kilichoandikwa na mwandishi Avitus Leonard, katika kitabu chake mwandishi alitumia mifano ya viongozi wakubwa duniani wanasemaje kuhusiana na furaha baada ya kuwanukuu wanafalsafa wengi. Basi nikakutana na sehemu ambayo mwandishi amemchagua kiongozi wa kanisa katoliki duniani kama mfano, Papa Francis ameshauri mengi ni namna gani mtu …

Hiki Ndiyo Kitu Ambacho Mtu Akikitafuta Huwa Hakikosi

Waswahili wanasema penye nia pana njia. Wengi wetu tumekuwa na ndoto nzuri lakini tafiti zinasikitisha sana. Licha ya watu wengi kuwa na ndoto ambao wanatimiza ndoto zao ni wachache sana. Sisi binadamu ni wazuri sana katika kutafuta sababu kuliko kutenda kile ambacho tumepanga kufanya. Kitu pekee ambacho mtu akikitafuta huwa hakikosi ni sababu. Mtafuta sababu …

Hii Ndiyo Njia Bora Ya Kumfundisha Mtu

Watu wengi huwa hawapendi kuonekana hawajui, hivyo namna ambayo huwa tunawafundisha watu huwa inasababisha migogoro mingi. Kila mtu huwa anaamini anajua hata kama hayuko sahihi, na kila mtu anapenda kusikilizwa kwa kile anachojua yeye, wakati mwingine usiingie kwenye mabishano ambayo hayakuiingizii hata mia, mwachie mtu nafasi ya kujiona mshindi kwenye kile anachokiamini yeye na mteja …

Kama Huna Sifa Hii, Usifungue Biashara Yoyote Ile

Kiasili kila mtu ni mfanyabiashara, kila mtu kuna kitu huwa anauza kwa mwingine ili awepe kupata fedha ya kuendesha maisha yake. Bila kuuza, huna mauzo utakayopata na mauzo ndiyo yanatupa fedha za kuwalipa wengine na kujilipa sisi wenyewe. Kwa chochote kile unachofanya jua namna ya kuteka hisia za watu ili uweze kuuza kile unachotaka.Watu wanapenda …

Design a site like this with WordPress.com
Get started