Nguvu Yako Iko Hapa

Usipende kujipa kazi ambazo ziko nje ya uwezo wako. Usitake dunia iende kama vile unavyotaka wewe. Usitake kuwa kiranja wa dunia, utashindwa vibaya. Yaani unataka kila kitu ukitawale na kiende kama vile unavyotaka wewe. Dunia huwa inajiendesha kwa misingi yake yenyewe. Inafanya kile inachotaka hivyo unapaswa kuelewa kuwa kuna vitu viko nje ya uwezo na …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Hawawezi Kubadilisha Kitu Chochote

Kama unahitaji mabadiliko yoyote yale ni lazima ukubali kufanya mabadiliko. Hakuna mabadiliko yoyote bila mabadiliko. Mabadiliko yalikuwepo, yapo na yataendelea kuwepo. Hakuna anayeweza kukwepa mabadiliko kwa namna yoyote ile. Mabadiliko yoyote yanayotokea duniani lazima yatakuathiri tu aidha unataka au hutaki. Hakuna mabadiliko yanayotokea duniani yakakuacha salama. Watu ambao hawawezi kufanya mabadiliko yoyote yale ni wale …

Fanya Kitu Hiki Mwenyewe

Ni kawaida kwa watu wengi huwa hawawezi kufanya kitu bila kusimamiwa. Siyo watu wote wana ile nidhamu ya kujisimamia wao wenyewe. Nidhamu binafsi ni changamoto ndiyo maana hata katika mafanikio watu wanatofautiana sana. Wengi huishia kuahirisha mambo kila siku. Huku wakijipa muda kuwa watafanya kesho au baadaye. Watu wanafanya kitu bila sababu yoyote ile pale …

Ufahamu Mwanzo Wa Upendo

Huwa watu wanapenda kupima upendo wao kwa vitu. Wengi wanatoa upendo ili waweze kupata maslahi fulani. Mtakatifu Agustino, aliwahi kunukuliwa akisema, kipimo cha upendo ni kupenda bila kipimo. Je wangapi unawapoteza kwa sababu ya upendo wa kipimo? Mwanzo wa upendo wowote ule ni tabasamu. Tunaanza kuonesha upendo kupitia tabasamu letu la ndani. Unapokutana na mtu …

Wasaidie Wengine Na Wewe Utasaidiwa

Kuwa mtu wa kujali maslahi ya wengine na utashangaa na wewe maslahi yako yanaenda vizuri sana. Kama huna fedha wasaidie wengine kupata fedha na wewe utapata fedha. Yaani toa thamani itakayowasaidia wao kupata fedha. Kuwa mtu wa kujitolea kuwaombea wengine katika shida zao. Utajikuta na wewe shida zako zinatatuliwa bila hata kujijua. Unaposumbuka na matatizo …

Walioshindwa Wana kitu Hiki Kimoja

Kiasili, binadamu ni wagumu kukubali kosa. Hata kama amefanya kweli lazima atajitetea kuonesha kwamba siyo yeye aliyehusika bali ni wengine. Kaa ukijua kwamba tatizo lolote ulilopata nawe umechangia kwa namna moja au nyingine. Kuna mambo mengi huwa tunachangia sana kutokea lakini huwa tunaona sisi hatuhusiki bali wengine ndiyo wanahusika kufanya. Unapopata kile ambacho hukutarajia kukipata …

Jinsi Ya Kupata Utulivu Wa Akili

Watu wengi kwa sasa wamevurugwa yaani kifupi watu hawana utulivu wa akili. Akili za watu wengi zimekuwa hazina utulivu. Zimekuwa kama nyani anayeruka tawi hili na kutua lile. Kwenye zama za mafuriko ya taarifa na maarifa ni zama ambazo unapaswa kuwa makini sana maana usipokuwa makini watu wengine watakutumia ili waweze kupata kile wanachotaka. Utulivu …

Hii Ndiyo Safari Endelevu

Kwenye vitu vingi vina ukomo wake. Hata maisha yetu tunayoishi yana ukomo wake. Hata tunaposafiri kutoka eneo moja kwenda lingine tunakuwa tunajua kabisa mwisho wetu ni wapi. Lakini katika safari ya ubora hakuna kikomo. Ubora hauna kikomo. Hakuna mahali utakuja kusema kwa sasa nimefikia mwisho wa ubora wa kile ninachofanya. Ubora wowote ule unaofanya jua …

Msamiati Wa Kuuvunja Katika Eneo Lako La Fedha

Fedha huwa haina kikomo. Hata ukiangalia idadi ya watu duniani ni ndogo kuliko fedha zilizopo. Ukomo wa fedha unauweka wewe mwenyewe na wala si mtu mwingine. Na leo tunakwenda kujifunza ni kwa namna gani tunakwenda kuuvunja msamiati unaokuletea ukomo wa kifedha. Kuanzia leo ukiwa na shida ya kiwango kikubwa cha fedha usiende kusema siwezi kuzipata …

Ifahamu Sifa Inayodumu Milele

Kila mmoja wetu ana sifa. Lakini sifa tulizonazo zinatofautiana kadiri ya mtu. Hebu jiulize wewe una sifa gani ambazo zitadumu milele?Watu wakitaja jina lako kitu cha kwanza wanapata sifa gani kutoka kwako? Nilipokuwa nasoma kitabu cha Yoshua Bin Sira nilijifunza kuwa maisha mema yana siku zake na sifa njema yadumu milele. Kumbe basi, sifa njema …

Design a site like this with WordPress.com
Get started