Angalia Usalama Wa Fedha Zako

Wako watu ambao wanawekeza kupoteza na wako ambao wanawekeza kupata.Wale wanaowekeza kupata ni wale ambao wanafuatilia kwa karibu sana kile walichowekeza. Wale ambao wanawekeza kupoteza ni wale ambao wanawekeza fedha zao sehemu na kukosa muda wa kuzifuatilia. Nikupe ushauri wa bure rafiki yangu, popote pale ulipowekeza fedha zako hakikisha macho yako, yako pale. Kuwa mtu …

Usikubali Kushindwa Kwenye Kila Kitu

Ndugu mmoja katika maadhimisho ya miaka 50 ya seminari ya maua ambapo walikutana wale wote waliosoma pale alitoa ushuhuda wake kwa uchungu akasema, huwa anamwambia Mungu kila mara nimeshindwa kuwa Padre na hata wito wa ndoa unishinde? Kauli hiyo inamfanya awe imara kwenye ndoa yake licha ya kushindwa kwenye eneo fulani. Rafiki yangu, usikubali kushindwa …

Kuwa Na Vitu Hivi Viwili Na Mambo Mazuri Yanakwenda Kutokea

Wewe ndiyo kiungo namba moja wa kile kinachoendelea kutokea kwenye maisha yako. Iwe unajua au hujui, wewe ndiyo unahusika kwa asilimia 100 na matokeo unayoendelea kupata sasa. Wewe ni mchangiaji namba moja wa matokeo uliyopata, unayopata na utakayoendelea kuyapata. Kwa kulijua hilo, leo nakwenda kukushirikisha mambo mawili ambayo yatakwenda kubadili maisha yako na kukuletea mambo …

Kama Umekosa Hamasa Ya Ndani Nunua Hamasa Ya Nje

Ziko aina mbili za hamasa, moja hamasa ya ndani na pili hamasa ya nje.Hamasa nzuri ni ile hamasa inayotoka ndani yako na hamasa ya nje ni ile inayotoka nje kwa kuangalia wengine wanafanya nini na wewe kuhamasika. Pale unapojikuta umepoteza hamasa juu ya kile unachofanya. Unapaswa kununua hamasa ya nje. Angalia wale ambao wanafanya kile …

Njia Rahisi Ya Kuacha Alama Duniani

Ni nani kati yetu anapenda kufa na kusaulika kabisa? Kila mtu anataka aache alama duniani isiyofutika ili hata vizazi vinavyokuja viweze kujifunza kutoka kwake. Iko njia nyingine rahisi sana ya kuacha alama duniani, kabla sijakuambia ni njia gani nikuulize swali je ni kitu gani kwa sasa unachofanya? KamaKuna kitu unachotoa kwa wengine basi hapo hapo …

Miaka 4 Ya Kuandika Kila Siku

Ilikuwa mwaka 2016 octoba mosi, nilipoanza safari ya kuandika kila siku. Hakika, namshukuru Mungu aliyeniwezesha kufanya yote haya. Kila siku nilikuwa natafuta mfumo, ni namna gani ninaweza kuandika kila siku. Mwandishi Makirita Amani alipoanza safari yake ya kuandika kila siku mwaka 2015 alinivutia na mimi. Ndipo ilipofika mwaka 2016 octoba mosi alipoanzisha Marathon ya kuandika …

Haya Ndiyo Maisha Mazuri Ya Kuishi

Je hayo ndiyo maisha yako halisi unayoishi?Je una furaha na maisha yako?Watu wengi hawaishi maisha mazuri wala kufurahia maisha yao kwa sababu hawajui haswa nini wanataka kwenye maisha yao. Hivi kama hujui kile unachotaka utawezaje kupata kile unachotaka? Mafanikio ya kwanza unayopaswa kuwa nayo ili uishi maisha mazuri ni kuweza kujua nini haswa unataka kwenye …

Kama Ukitengeneza Maana, Utatengeneza Hiki

Iko njia moja ya uhakika ya kupata fedha. Usidanganyike na njia za panya. Watu watakuambia kuna njia rahisi ya kupata fedha, jiulize kama kuna njia rahisi ya kupata fedha kwanini wasiwe nazo wao? Kuna mtu ambaye hana shida ya fedha? Sasa ukiona mtu anakuambia njia rahisi ya kupata fedha, jua wewe ndiyo fedha yenyewe. Ukiona …

Tumia Mbinu Hii Kama Unataka Kujua Uwezo Wa Watu

Kila mmoja wetu Mungu amemwita kuja duniani kwa kusudi fulani. Imani yangu ni kwamba kila mtu ana uwezo mkubwa wa kutenda miujiza ndani yake. Pia, hakuna mtu ambaye hafai kwa lolote. Hakuna mtu anayeweza kuwa kama wewe, ndiyo maana tunaishia kusema, anafanya kama fulani lakini siyo kama fulani. Pengo la mtu linazibwa na mtu mwenyewe. …

Kamwe Usijiambie Kitu Hiki

Siku zote unapaswa kufikiria kile unachotaka kwenye maisha yako na siyo kile usichotaka kwenye maisha yako. Unajua unakuwa unakosea pale ambapo unakuwa unafikiria sana vitu ambavyo huvitaki. Na kawaida ya akili huwa inafanya kile kitu ambacho huwa unakifikiria sana. Kumbe kufikiria kile usichokitaka ni njia ya kujifungulia milango ya nuksi. Akili yako inapaswa kufikiri kile …

Design a site like this with WordPress.com
Get started