Kama Unaona Elimu Ni Ghali, Jaribu Hiki Hapa

Kuna msemo mmoja unaosema kwamba kama unafikiri elimu ni ghali sana jaribu ujinga. Ukiona vya elea ujue vimeundwa. Kumbe basi, kila kitu kizuri tunachokiona ujue kimefanyiwa kazi. Kama hutaki kupata vizuri basi tumia vibaya. Hapa ndiyo ule msemo unakuja kama unafikiri elimu ni ghali sana jaribu ujinga. Watu huwa hatuko tayari kulipia gharama ya vile …

Fanya Kazi Hii Kwanza Kabla Hujaanza Majukumu Mengine

Akili zetu huwa hazipendi vitu vigumu kabisa, akili huwa inapenda vitu virahisi na haijisumbui kwenye vitu vigumu. Usishangae kuona watu wengi wakiahirisha vitu vigumu na kufanya vitu vyepesi. Pale unapokuwa na kazi mbili moja rahisi na nyingine ngumu wewe utachagua kuanza na ipi? Watu wengi watachagua rahisi na matokeo yake ile ngumu wanakuja kuiahirisha kufanya. …

Ni Wakati Wake Wa Kukirudisha Kwa Wenyewe

Huwa tunajidanganya kwamba sisi ni wa miliki wa milele wa vile ambavyo tunavyo kumbe siyo. Sisi ni wa miliki wa muda tu wa vile ambavyo tunavyo. Kwa mfano, ni wangapi wanaendesha magari na siyo yao? Wanaazima au kukodi lakini inapofikia muda analirudisha kwa mwenyewe, aliyeomba au kukodi hawezi kujimilikisha gari hilo bali anajua amepewa kwa …

Hiki Ndiyo Kitu Ambacho Ukipata Asubuhi Kinakwenda Kubadili Siku Yako Nzima

Huwa unaianzaje siku yako? Je unainza siku yako kwa kuangalia simu yako kujua nani amekutafuta na nini kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii? Au unainza siku yako kwa kusali, kufanya mazoezi, kusoma kitabu, kuandika, kusikiliza vitabu vilivyosomwa vinavyokupa hamasa ya kwenda kufanya kazi? Au pengine unainza siku yako kwa kusikiliza uchambuzi wa magazeti, kusikiliza BBC, taarifa …

Jinsi Ya Kuwa Mtu Wa Tofauti Katika Karne Ya 21

Iko njia rahisi sana ya kuwa mtu wa tofauti katika jamii unayoishi.Dunia ya leo, tumezoea kuwaona watu wakiishi maisha ya kawaida yaani maisha ya kimazoea ambayo hayawapi makubwa wala hata hayawasaidii kulipa bili. Kama unaishi maisha ya kimazoea ambayo hayakusaidii hata kulipa bili hayo siyo maisha, wengi wanaishi maisha ya kimazoea kwa sababu hawataki kufanyia …

Hawa Ndiyo Watu Adimu Katika Jamii Yetu

Siku hizi watu wanaoanzisha vitu ni wengi, watu wanaongea ni wengi na wengi huwa wanajidanganya kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni wafanyaji wazuri lakini kuna kitu huwa wanakikosa. Katika jamii yetu, tunawakosa watu wanaoanzisha kitu na kukimaliza. Kiufupi katika jamii yetu tumewakosa watu adimu ambao ni wamalizaji wa kazi wanazoanza kuzifanya. Siku hizi watu wanakuwa …

Huyu Ndiye Mtu Unayemsahau Pale Unapopata Fedha

Iko kanuni kuu moja ya kupata uhuru wa kifedha na utajiri. Kanuni ambayo wale waliotajirika imewasaidia na hata wewe mwenyewe ukiitumia itakusaidia pia. Yuko mtu ambaye huwa unamsahau sana pale unapopata fedha ambaye ni wewe mwenyewe. Ukipata fedha unawalipa watu wote kasoro wewe mwenyewe. Ukipata fedha tu, baada ya muda mfupi unaanza kumlipa mtu anayekuuzia …

Tafadhali; Ukiwa Na Njaa Usifanye Mambo Haya

Natumaini unaelewa ni namna gani ukiwa na njaa jinsi miili yetu inavyokuwa. Unapokuwa na njaa akili yako huwa hakuna inachowaza zaidi ya chakula. Tukiwa na njaa huwa hatubaki salama hata kidogo. Ndiyo maana leo nakusihi sana rafiki yangu ukiwa na njaa usifanyemaamuzi yoyote yale mpaka pale utakapokuwa umeshiba. Tukifanya maamuzi tukiwa na njaa lazima maamuzi …

Kuwa Makini Na Watu Hawa Wawili

Hakuna kipindi ambacho unapaswa kuwa makini kama hiki, wewe ni mtu ambaye unawindwa zaidi hata ya swala porini. Wanaokuwinda unaishi nao na muda wowote usipokuwa makini wanakuumiza vibaya. Kwenye kila ufanyalo uwe makini na upunguze matatizo yasiyokuwa na ulazima. Leo ninakwenda kukushirikisha watu wawili unaopaswa kuwa nao makini kwenye maisha yako. Moja, kuwa makini na …

Hiki Ndicho Kinachopelekea Kuiona Kazi Yako Ni Mbaya Au Nzuri

Katika msingi wa falsafa ya ustoa, falsafa ya kuishi kanuni za asili na kudhibiti hasira inatualika kuwa asili huwa haina kitu kibaya wala kizuri. Kama asili haina kitu kibaya wala kizuri sana nini kinachopelekea watu kuona vitu vibaya na vingine vizuri? Jawabu;Kitu kinachopelekea watu kuona vitu vibaya na vizuri ni mitazamo waliyonayo watu juu ya …

Design a site like this with WordPress.com
Get started