Jifunze Kumsikiliza Mtu Huyu Na Utapiga Hatua Kubwa

Unakwama wapi? Ni rahisi kufanyia kazi maoni ya watu wengine na kusahau kufanyia kazi maoni yako binafsi. Watu wengi wanajali maoni ya wengine kuliko kujali maoni yao. Ni kawaida ya watu wengi kuishi maisha ya watu wengine na kusahau kuishi maisha ya ndoto zao. Wengi hawafuati mioyo yao. Kama kila mtu angekuwa anafuata moyo wake …

Hawa Ndiyo Watu Ambao Uko Nao Katika Kipindi Cha Mpito

Maisha ya wanandoa huwa wanaanza wakiwa wawili na baadaye wanabarikiwa kupata watoto. Ila baada ya muda watoto wote wataondoka na kuwaacha nyie wawili kama mlivyo. Kama uko kwenye ndoa, mpende mwenza wako maana utakua naye maisha yako yote mpaka pale kifo kitakapowatenganisha. Usigawe upendo wako wote kwa watoto ukifikiri maisha yako yote utakua nao na …

Hiki Ndiyo Kitu Kinachowatawala Watu Wengi

Ni rahisi watu kusema kwa mdomo na kujivunia kuwa wao hawana hofu. Hofu inaendesha dunia kuliko hata unavyofikiria kwenye maisha yako. Kila siku hofu inawafanya watu washindwe kwenda kule wanakotaka kwenda. Ni vitu vingapi umeshindwa kuvifanya kwa sababu ya hofu? Na ukiangalia sababu kubwa ni hofu labda ya kuogopa kushindwa. Unakuwa unaogopa endapo ukijaribu na …

Kama Unataka Jambo Lako Lifanyike

Watu wengi kwa sasa wamekuwa na mambo mengi na kama unategemea wakusaidie kufanya jambo fulani usipokuwa karibu nao ni rahisi kutokufanya. Kama unataka watu wafanye kile unachotaka. Kwanza wafuatilie. Watu wana mambo mengi, usipowakumbusha na kuwa nao karibu hawatafanya kile ulichowataka kufanya. Binadamu wana asili ya kufanya jambo fulani mpaka wasimamiwe. Wapate mtu wa kuwawajibisha …

Hii Ndiyo Dalili Inayoonesha Kuwa Umesimama Kwa Kitu Fulani

Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill enzi za uhai wake aliwahi kunukuliwa akisema; umekuwa na maadui? Vizuri. Hii ina maana ya kwamba umesimama kwa kitu fulani kwenye maisha yako. Kama unaona una maadui wengi basi jua kabisa umekuwa na maadui hao kwa sababu umesimama kwa kitu fulani kwenye maisha yako. Churchill anakupongeza kwa …

Hiki Ndicho Kinachowatofautisha Wafuasi Na Viongozi

Aliyekuwa mkurugenzi na mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Jobs aliwahi kunukuliwa akisema; Kinachowatofautisha kati ya wafuasi na viongozi ni ugunduzi. Hutakiwi kuwa kiongozi mfuasi bali unatakiwa kuwa kiongozi mgunduzi. Kila siku unatakiwa ujifunze namna ya kuongoza. Usipokuwa wa kujifunza maana yake umechagua kuwa mfuasi na hii maana yake ni kuwa hutoweza kugundua kitu …

Ukiwa Na Ujasiri Huu, Utapata Kile Unachotaka

Siyo kwamba wale wanaofanikiwa kwenye kitu fulani ni wajanja sana au wana bahati sana kuliko wengine. Wana nguvu moja ambayo ndiyo inawasaidia kupata kile wanachotaka. Unapata kile unachotaka kwenye maisha kama umekuwa na ujasiri wa kuomba kile unachotaka.Watu wengi huwa hawana ujasiri wa kuomba kile wanachotaka. Wanaishia kuongea tu kwa mdomo. Shabaha yangu ya kukuandikia …

Hii Ndiyo Kanuni Ambayo Huwa Haishindwi

Ili kupata kile unachotaka, anza kwanza kutoa kile ulichonacho. Haijalishi ni kikubwa au kidogo wewe anza kutoa na wanapopokea wengine na wewe ndiyo utapokea. Usidharau chochote kile ulichonacho. Wewe tafuta watu ambao wanaweza kunufaika na wewe kwa kile ulichonacho. Wafanyie kile unachotaka, kisha watake wakulipe. Hiyo ndiyo kanuni ya asili ambayo haijawahi kushindwa. Kama unatoa …

Hiki Ndiyo Kitu Kichungu Duniani Lakini Matunda Yake Ni Matamu

Sehemu pekee ambayo unaweza kuona nyota ni kwenye giza. Kila kitu kina faida yake kama ukikitumia vizuri. Wako wanaochukia giza lakini bila giza huwezi kuona nyota za angani. Wale wanaochukia giza ni sawa na wale wanaochukia changamoto kwenye maisha yao. Wakati mwingine, jifunze kutokana na kila unachokutana nacho. Mwanafalsafa Aristotle enzi za uhai wake aliwahi …

Eti Ni Kweli Huwezi Kuishi Bila Yeye?

Huwa unapenda kujidanganya kwamba huwezi kuishi bila kitu fulani. Muda mwingine unaenda mbali zaidi kwamba huwezi kuishi bila ya watu wako wa karibu ulionao sasa kwenye mahusiano.Huwa unapenda kujidanganya kwamba huwezi kuishi bila wao je ni kweli? Hayo yote ni uwongo, kitu pekee ambacho huwezi kuishi bila hicho ni pumzi tu. Unaweza kuishi vizuri tu …

Design a site like this with WordPress.com
Get started