Funga Hiyo Biashara

Kama una biashara na una msaidizi au wasaidizi ambao wanakusumbua lakini  unashindwa kuwafukuza, funga hiyo biashara.

Ukiona mtoto au msaidizi wako anakupanda kichwani hataki kutii mamlaka basi hapo jua huna mtoto wala msaidizi.

Kama mmiliki wa biashara unatakiwa kua na maamuzi magumu dhidi ya biashara yako. Umeajiri ndugu au watu wako wa karibu halafu wanafanya vibaya lakini wewe kama mmliki unashindwa kuwafukuza jua hapo huna biashara na bora ufunge hiyo biashara.

Hatua ya kuchukua leo; Kama una biashara na unashindwa kuwafukuza wale wanaoharibu biashara jua hapo huna biashara.

HAKUNA mtu ambaye yuko juu ya biashara hivyo kama mtu anashindwa kufuata mchakato uliowekwa kwenye biashara akae pembeni ili biashara iweze kwenda mbele.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started