Mtu Wa Kumwepuka Kumwambia Matatizo Yako

Mpendwa rafiki,

Unapokuwa na changamoto unahitaji kuchagua mtu makini sana wa kumshirikisha kwa sababu siyo kila mtu ni wa kumshirikisha matatizo yako. kuna watu wengine ukiwaambia mambo yako ni kama vile umemwambia  upepo na kama tunavyojua upepo kazi yake ni kupeperusha vitu hivyo hautakuwa na ustaimilivu wa kuzuia mambo.

JIPATIE NAKALA YA KITABU HIKI KWA SHILINGI ELFU TANO TU,KUPATA KITABU HIKI WASILIANA NAMI KWA 0717101505/0767101504 AU BONYEZA HAPA

Kuna watu ukiwaambia mambo yako ni umeanika mambo yako yote hadhari, siyo watu wote ni waaminifu kuna watu kukaa na jambo hawawezi yaani akisikia kitu tu anakuwa kama vile anawashwa au amebanwa na haja hivyo anahitaji kwenda kujisaidia kukaa nayo hawezi. Kama unamjua bata jamii ya ndege vile anavyoshindwa kujizuia haja yake yeye sehemu yoyote tu anaachia haja yake.

SOMA; Jinsi Ya Kujipunguzia Matatizo Kwenye Maisha Yako

Mwandishi mmoja aliwahi kusema nusu ya watu unaowaeleza matatizo yako hawatajali kabisa, unajua ni kwanini? Na wao wana matatizo yao yanayowasumbua.  Katika hao nusu wanaojali labda wale watakaochukua hatua hata ya kukupa nafasi ya kukusikiliza na kufikiria kuhusu matatizo yako, nusu watafurahi kwamba una matatizo hayo. Japo wataonesha kukuonea huruma lakini mioyoni mwao watafurahia una matatizo.

Katika wale ambao hawatafurahia changamoto zako, nusu hawatakuwa na namna yoyote ya kukusaidia wataishia kukuambia pole au pengine mambo yataenda vizuri. Kwahiyo, kila mmoja wetu anapokuwa anachangamoto anatakiwa kutafuta mtu makini na mwaminifu atakayeweza kukusikiliza na watu hawa ni wachache sana katika jamii yetu ambao wanauwezo wa kukusaidia kwenye matatizo yoyote unayokuwa nayo.

Kabla hujamwambia mtu matatizo yako jiulize ni yupi kweli anaweza kukusikiliza na kukusaidia kweli. Usikimbilie tu kuanika mambo yako hadharani kwa sababu watu wengi wana matatizo yao hivyo na wewe ukienda kuwaeleza juu ya matatizo yako wataishia tu kukuonea huruma wengine watafurahia una matatizo na kupata nafasi ya kutangaza habari zako.

SOMA; Mtu Pekee Unayepaswa Kuambatana Naye Katika Safari yako Ya Kutafuta Mafanikio

Hatua ya kuchukua leo, hakikisha unakuwa na mtu makini mwenye uwezo wa kukusaidia na kukusikiliza. Usiwe na akili ya kuanika mambo yako katika mitandao ya kijamii na kuomba ushauri hapo ndipo utakpoweza kupotea kabisa. Katika zama hizi za taarifa watu wengi wamekuwa ni watu wa kuanika kila kitu wanachofanya katika mtandao wa kijamii hivyo epuka uteja huo kwani utakugharimu. Washauri wa kweli hawapatikani kwenye mitandao ya kijamii kwani siku hii mtandao imekuwa ni kama vijiwe hivyo huwezi kupata watu makini watakaokusikiliza.

Kwahiyo, ni bora kukaa na matatizo yako na kuyatatua taratibu kuliko kuelezea upepo mambo yako. upepo wanaweza kuwa ni wale watu ambao siyo makini ni wale ambao ni mapepe wakiambia jambo hawatulii  wanatafuta watu wa kwenda kuwapasha habari.

MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana 

 

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started